Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyekuwa na miaka miwili na miezi sita, mkazi wa Kitongoji cha Mbale Kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera amekutwa amefariki na mwili wake umefungwa kwenye mfuko (Sandarusi) huku ukiwa hauna baadhi ya viungo.
Akizungumzia tukio hilo Katibu Tawala Wilaya ya Muleba Benjamin Mwikasyege amesema kuwa mwili huo umekutwa umetelekezwa kwenye karavati yenye maji ya barabara ya Makongora, Kijiji cha Malele.
Aidha ameongeza kuwa mwili wa marehemu umechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini walio tekeleza tukio hilo.
Asimwe Novath aliibwa nyumbani kwao Mei 30 mwaka huu, baada ya mama yake kukabwa na watu wasio julikana usiku wa saa 2:30 kisha mtoto huyo kuchukuliwa ambapo amekuwa akitafutwa hadi mwili wake ulipopatikana leo Juni 17, 2024, katika Kijiji cha Malele kata Ruhanga wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Pia soma:
- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualibino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi
- Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli