Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo
Mtoto Asimwe Novath mwenye ualbino Mkazi wa Kitongoji Mbale Kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera amekutwa amefariki na mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza Katika eneo la tukio Katibu Tawala wilaya ya Muleba Benjamin Mwikasyege amesema kuwa mwili huo umekutwa umetelekezwa kwenye karavati yenye maji ya barabara ya Makongora, Kijiji cha Malele na watu wasiojulikana.

Aidha ameongeza kuwa mwili wa marehemu umechukuliwa ili kuhifadhiwa zikiwa zinasubiriwa taratibu za mazishi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini walio tekeleza tukio hilo.

Nao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelaani kitendo hicho na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali sana wale wote waliohusika endapo watabainika

Asimwe Novath aliibwa nyumbani kwao Mei 30 mwaka huu baada ya mama yake kukabwa na watu wasio julikana usiku wa saa 2:30 na mwili wake kupatikana leo Juni 17 katika Kijiji cha Malele kata Ruhanga wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Pia Soma:

- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualibino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi



- Mtoto Asimwe Novath aliyekuwa na miaka miwili na miezi sita akutwa amefariki na mwili kufungwa kwenye mfuko
Why multiple threads?

Ili tupoteze focus?
 
Marais wetu sijui ni unafiki au ni shida gani, kama wanaona ni ngumu kutoa ridhaa hii hukumu itekelezwe basi waombe sheria zibadilishwe ili watu kama hawa wanyongwe haraka haraka.

Adhabu pekee inayomstahili mtu aliyetoa maisha ya mwingine kinyama kiasi hiki ni kifo tu, sio kukaa jela maisha.
Inabidi kwanza kujitoa kwenye mikataba ya kimataifa inayohusiana na zinazoitwa "haki za binadamu".Hayo mambo ya kupiga vita hukumu ya kifo yanaanzia huko.

Sasa niambie nchi yako inaweza?Vitu vinavyoitwa misaada au mikopo au ushirikiano na nchi zenye ukwasi katika nyanja muhimu,vyote huwa vinaambatana na masharti.

Mojawapo ni hilo linaloitwa "haki za binadamu".Kichaka cha haki za binadamu kimeficha mambo mengi sana,ushoga ukiwemo.
 
Hapa wapumbavu wa utajiri walihamia kweny ulawiti , sasa wamerudi rasmi kweny kuua albino hawa dawa yao inachemka.
 
Najua umeumia. Ila kusema Mungu atawalipa ni unajidanganya

Ukweli imani juu ya Mungu na dini ni sababu kuu ya mauaji ya huyu mtoto albino.

Biblia na quran ndio chanzo cha yote haya.

Mtu yoyote anaeamini Mungu wa kwenye Biblia ama Mungu wa kwenye Quran yupo maana yake anaamini na uchawi upo pia.

Na hao hao wanaoamini uchawi ndio wanayoyafanya haya.

Mtu ambaye haamini uwepo wa Mungu anakuwa haamini na uwepo wa uchawi pia. Hivyo hawezi kuua albino maana anajua uchawi na waganga ni usanii tu.

Nchi ambazo haziamini biblia wala quran huwezi kukuta huu ujinga.

Japan, korea, china huwezi kukuta huu ujinga wa kuamini uchawi na waganga wa kienyeji
Mkuu uganga upo kila sehemu hata huko China, Japan na South Korea unapopasemea... Tena uganga wao ni hatari.. Jaribu hii APP (KAYSA) ipo playstore.. Inaweza kukuambia mambo ya mbeleni mi niiliifuta maana sikutaka ukweli
 
Upo sawa. Hizo takataka zinafaa zichomwe moto kwenye incinerator.
Sio moto tu wakatwe taratibu kuanzia kucha hadi utosini na iwe hadharani ili watu wajifunze kwa kweli inasikitisha sana
Hapa nawaza huyo mtoto walimuua kwanza au walimkata viungo akiwa hai
 
Back
Top Bottom