Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo
Watu wa Kanda ya Ziwa mnazingua sana na hizi imani zenu za kishirikina, za kuua watu wenye ulemavu wa ngozi.
Sasa mtoto mdogo kama huyo mnamtoa uhai wake kwa sababu tu ya imani ya kipuuzi!!

Halafu ni kwa nini uchaguzi unapokaribia, ndiyo haya mauaji yanaibuka kwa kasi? Acheni ushetani wenu nyinyi. ☹️
 
Muleba, kagera

Hizo imani zimeshaanza kuwaingia 🙌🏾🙌🏾

Mungu amrehemu marehemu na waliotenda, Mungu awalipe sawa na inavyowastahili
 
Hivi kweli jamani unaanzaje kumkata mtoto mikono? Na sijui walimkata akiwa hai au walimuua kwanza?

Mungu atawalipa sawasawa na walichokifanya, nimeumizwa sana.

Najua umeumia. Ila kusema Mungu atawalipa ni unajidanganya

Ukweli imani juu ya Mungu na dini ni sababu kuu ya mauaji ya huyu mtoto albino.

Biblia na quran ndio chanzo cha yote haya.

Mtu yoyote anaeamini Mungu wa kwenye Biblia ama Mungu wa kwenye Quran yupo maana yake anaamini na uchawi upo pia.

Na hao hao wanaoamini uchawi ndio wanayoyafanya haya.

Mtu ambaye haamini uwepo wa Mungu anakuwa haamini na uwepo wa uchawi pia. Hivyo hawezi kuua albino maana anajua uchawi na waganga ni usanii tu.

Nchi ambazo haziamini biblia wala quran huwezi kukuta huu ujinga.

Japan, korea, china huwezi kukuta huu ujinga wa kuamini uchawi na waganga wa kienyeji
 
Mtoto Asimwe Novarti mwenye ulemavu wa ngozi (albino) aliyeibwa Mei 30 mwaka huu na watu wasiojulikana katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba, amekutwa ameuawa na kisha mwili wake kufungwa kwenye sandarusi na kutelekezwa kwenye moja ya kalavati huku baadhi ya viungo vya vyake vikiwa vimenyofolewa.

Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba, Benjamin Mwikasyege amesema mwili ulikutwa umefungwa kwenye mfuko kabla kuchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mtoto Asimwe Novarti aliyekuwa na miaka miwili aliibwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana ambao walifika na kudai wanahitaji msaada kutoka kwa mama wa familia hiyo ambaye baada ya kutoka ndani ili kutoa msaada walimkaba na kisha kutokomea na mtoto huyo.

Chanzo: azamtvtz

Na kuna Mbunge mmoja najua kwa Jimbo lake lilivyo Gumu na Tamu Kiuchumi asipotenda hii Dhambi hatorejea ng'o.
 
Hii adhab ianze kutekelezwa kwa makosa kama haya, haiwezekani haya mambo mpaka karne hii yanaendelea
Marais wetu sijui ni unafiki au ni shida gani, kama wanaona ni ngumu kutoa ridhaa hii hukumu itekelezwe basi waombe sheria zibadilishwe ili watu kama hawa wanyongwe haraka haraka.

Adhabu pekee inayomstahili mtu aliyetoa maisha ya mwingine kinyama kiasi hiki ni kifo tu, sio kukaa jela maisha.
 


Mtoto Asimwe Novath mwenye ualbino Mkazi wa Kitongoji Mbale Kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera amekutwa amefariki na mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza Katika eneo la tukio Katibu Tawala wilaya ya Muleba Benjamin Mwikasyege amesema kuwa mwili huo umekutwa umetelekezwa kwenye karavati yenye maji ya barabara ya Makongora, Kijiji cha Malele na watu wasiojulikana.

Aidha ameongeza kuwa mwili wa marehemu umechukuliwa ili kuhifadhiwa zikiwa zinasubiriwa taratibu za mazishi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini walio tekeleza tukio hilo.

Nao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelaani kitendo hicho na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali sana wale wote waliohusika endapo watabainika

Asimwe Novath aliibwa nyumbani kwao Mei 30 mwaka huu baada ya mama yake kukabwa na watu wasio julikana usiku wa saa 2:30 na mwili wake kupatikana leo Juni 17 katika Kijiji cha Malele kata Ruhanga wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Pia Soma:
- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualibino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi

- Mtoto Asimwe Novath aliyekuwa na miaka miwili na miezi sita akutwa amefariki na mwili kufungwa kwenye mfuko
 
Back
Top Bottom