The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Flashback:
Kumbuka hili ni Shauri la kikatiba Na. 7300 lililofunguliwa na mawakili Maduhu William, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Lengo la shauri hili ni kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea, vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu mmojawao akiwa mahabusu mteja wao Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA (T)...
Leo baada wadaiwa kuwa wamewasilisha viapo vyao kinzani, Shauri limeanza kusikilizwa rasmi kwa Tundu Lissu kuwadodosa walalamikaji ili kuthibitisha uhalali wa madai yao kisheria....
Wa kwanza kudodoswa na Tundu Lissu ni mlalamikaji Na. 1 Wakili William Maduhu. Fuatilia dodoso hii na Kisha re - Examination ya mawakili wa upande wa walalamikiwa - Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bwana Jela wa Gereza la Ukonga na Kamishina wa Magereza..
Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
Part 2.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Nenda ukurasa wa 27 angalia defence counsels angalia jina la Kulwa Maduhu na Paul Kisabo kama hayapo?
Wakili Maduhu: Yapo majina ya hao mawakili.
Mhe. Lissu: Ukurasa wa 40 kwenye huo mwenendo wa Kisutu angalia upande wa corum useme kama Paul Kisabo na Kulwa Maduhu.
Wakili Maduhu: Wapo wote wawili.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kuna utaratibu wowote wa kisheria wa unaopaswa kuufuata kumuona mteja?
Wakili Maduhu: Hakuna utaratibu wowote wa kisheria zaidi ya kuonesha kitambulisho tu cha uwakili.
Mhe. Lissu: Haya Maneno ya Bwana jela kuwa sijakutambulisha ni maneno ya bure tu?
Wakili Maduhu: Kabisa maneno ya bure kabisa.
Mhe. Lissu: Unazifahamu kanuni za maadili za mawakili?
Wakili Maduhu: Nazijua ndio.
Mhe. Lissu: Je kwa kanuni hizi wakili anaruhusiwa kumuonesha makubaliano yake na mteja mtu anayeitwa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Duty to confidentiality hairuhusu. Kwahiyo siruhusiwi kabisa kutoa siri za mteja wangu.
Mhe. Lissu: Sasa unasemaje kuhusu hizi habari za Bwana Jela kuwa sijakutambulisha kwake?
Wakili Maduhu: Hizo ni kauli za bure kabisa. Mimi silazimiki kufanya hivyo. Nina miaka 6 ya uwakili kwa sasa huo utaratibu haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 41 hadi 43 wa proceedings za Kisutu. Soma Tar. 16/06 sema kama mahakama ya Kisutu haikuandika malalamiko yangu kuhusu mawakili wangu kunyimwa kuniona.
Wakili Maduhu: Ni kweli malalamiko yapo.
Mhe. Lissu: Ni kwamba nilikuwa nazuiwa kuonana na mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Kweli yapo hapa
Mhe.Lissu: Kwamba ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa magereza?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa yapo yote kwenye hizi kurasa za mambo ya Kisutu.
Mhe. Lissu: Pia kuna malalamiko specific kuwa kitendo hicho cha mimi kuninyima nisionane na mawakili wangu ni kinyume na sheria na kanuni za kimataifa?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Nikalalamika kuwa naishi na wafungwa waliohukumiwa kifo? Na natendewa sawa na watu hao?
Wakili Maduhu: Kweli kabisa ulisema.
Mhe. Lissu: Baada ya hayo nilisema nitajiwakilisha mwenyewe kwasababu sitaki mawakili wangu waje kulaumiwa bure?
Wakili Maduhu: Ni kweli ulisema hivyo na ikawa hivyo.
Mhe. Lissu: Ulipoamua kujiwakilisha mwenyewe nilisema waendelee kunisahuri na kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea. Nilisema hivyo?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze toka siku hiyo tar. 16/05/2026 hadi leo mmeendelea kunipa ushauri wa kisheria na kunipa nyaraka Gerezani?
Wakili Maduhu: Ni kweli tumeendelea kufanya kazi hiyo.
Mhe. Lissu: Je una kumbukumbu za kilichotokea Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo lilipofika Mahakama kuu niliwaeleza waheshimiwa majaji kuwa nina mawakili wanaonisaidia kwa research na ushauri.
Wakili Maduhu: Ni sahihi ulisema.
Mhe. Lissu: Naomba nimuonyeshe proceedings za Mahakama Kuu. Tuambie from page 4 to 6 wambie majaji kama huo mwenendo unaonesha niliwaambia Majaji wa Mahakama kuu nina mawakili ambao wananisaidia na nikaomba waingizwe kwenye column.
Wakili Maduhu: Nimeona ndio.
Mhe. Lissu: Na Katuga alipinga ombi langu hilo.
Wakili Maduhu: Ni sahihi naona hapa.
Mhe. Lissu: Mahakama ikasema hatutawaingiza kwenye corum lakini mawakili wako waendelee kukusaidia?
Wakili Maduhu: Naona iko hapa.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni kweli sio tu Kisutu hata Mahakama kuu hii inakutambua wewe na wenzako kama mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Part 3
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe.Lissu: Nenda kwenye supplementary affidavit ya wajibu maombi wa 3 ya Tarehe 12/05 anasema kuwa wewe na Paul Kisabo hampo kwemye orodha ya mawakili niliyowasilisha kwake?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Amewasilisha SUPP 1 kwenye supplimentary affidavit na anasema hakuna jina la Kulwa maduhu na Paul Kisabo. Sasa angalia hiyo annexure SUPP 1 na uwaeleze majaji kama maneno yake haya ni ya kweli?
Wakili Maduhu: Kwenye SUPP 1 hayapo.
Mhe. Lissu: Je pamoja na wewe na Paul Kisabo kutokuwepo kwenye orodha hii mmewahi kuja kuniona gerezani na kuongea na mimi?
Wakili Maduhu: Ni sahihi tumewahi kuja na kama mara tatu nimewahi kuingia na kuja kukuona.
Mhe.Lissu: Katika hizo mara tatu zote je ulijiandikisha pale magereza kabla ya kuniona na ukaonesha kitambulisho chako?
Wakili Maduhu: Sahihi nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu: Je wewe ni mtunzaji wa hizo kumbukumbu za watu wanaoingia na kutoka Gereza la Ukonga?
Wakili Maduhu: Sio mimi kabisa. Ni Bwana Jela huyo hapo amekaa kwenye kiti ndio kazi yake. Anamuonesha kwa kidole chake.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama jina lako lipo kwa watu waliotembelea gereza?
Wakili Maduhu: Ndio tar. 28/10 jina langu lipo lakini hii siku sikumuona niliambiwa sitaweza kumuona. Na mara tatu zote nilizowahi kumuona hizo nyaraka hazijaletwa na Bwana Jela. Mkuu wa Gereza yani.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 2 angalia hiyo nyaraka halafu useme item no. 10 aliyekuja ambae ni Paul Kisabo ameoneshwa jina lake na shida yake wameandika shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Namuona hapa ndio yupo.
Mhe. Lissu: Tarehe 30/09 angalia jina la kwanza hapo la watu waliotembelea Gerezani ni akina nani?
Wakili Maduhu: Jina ni la Paul Kisabo.
Mhe. Lissu: Je yupo kwenye ile orodha ya kwanza ya watu niliowatambulisha kwa mujibu wa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Kule hayupo.
Mhe. Lissu: Kumbe hayupo kule na magereza walimruhusu aingie?
Wakili Maduhu: Ndio kabisa
Mhe. Lissu: Nenda sasa SUPP 3 na yenyewe. Majina ya mawakili unaowaona na wataje.
Wakili Maduhu: Andrew Mathew Chima na Nashon Nkungu.
Mhe. Lissu: Hao mawakili walikuja kuniona mimi?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe.Lissu: Huyo Andrew aliyekuja kuniona ni mmoja wao au sio mmoja wao kwenye ile orodha aliyosema Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hayumo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 5 sasa kwenye hicho kielelezo ni register book ya Gereza la Ukonga. Pembeni imeandikwa SUPP 5 ukurasa unaofuata unaonesha entry ya Tar. 07/05 mwaka jana kuna mtu wa kwanza kabisa anaitwa Nashon Nkungu kazi yake ni wakili amekuja kumuona Mahabusu Tundu Lissu. Shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kwanini aliruhusiwa kuja kuniona huyo Nashon.
Wakili Maduhu: kwasababu ni wakili wako.
Mhe. Lissu: Tarehe inayofuata aliruhusiwa tena kuingia?
Wakili Maduhu: Ndio anaonekana hapa kwenye ukurasa unaofuata. Kwenye kurasa kadhaaa. Ukurasa wa 9 na tarehe 28/07 alikuwa mtu wa kwanza kuja kukuona.
MheLissu: Tar. 24/12 jina namba 2 ni Nashon Nkungu tena?
Wakili Maduhu: kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Kisabo je yupo au hayupo?
Wakili Maduhu: Na Kisabo nae yupo kabisa.
Mhe. Lissu: 04/03/2026 mtu wa pili Nashon Nkungu aliruhusiwa kuja kuniona?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Part 4
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Twende Annexure SUPP 6 angalia Tarehe 12/12/2025 mtu wa pili ameandikwa Paul Emanuel Kilasa Kisabo na yeye alikuja kuniona na akaruhusiwa?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa Mawakili wangu aliyekatazwa kuja kuniona ni wewe peke yako?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa tuje kwenye sababu za kukukatalia wewe kuja kuniona. Soma Annexure SUPP 3 entry ya Tar. 28/10/2025 je siku hiyo ulikwenda Gereza la Ukonga na Wakili mwenzako Gaston Garubindi?
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Nenda kwenye SUPP 1 ile orodha na wambie majaji kama Gaston Garubindi yupo kwenye hiyo orodha?
Wakili Maduhu: Jina lake ni namba 3.
Mhe. Lissu: sasa angalia hiyo nyaraka sawasawa imeandika mambo mengi kule mwisho kuna maoni ya OC ni officer in charge yaani BWANA JELA.
Ameandika maoni yake kuwa aruhusiwe kumuona ambae yupo kwenye orodha ya mawakili. Na huyo mwingine asiruhusiwe kwasababu hayupo kwenye hiyo orodha.
Wakili Maduhu: Niliambiwa toka hapa haupo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Je kuna Wakili mwingine ameandikiwa maoni ya namna hiyo kwenye orodha ya mawakili wangu kuwa asinione hayupo kwenye majina niliyompa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hakuna wakili mwingine.
Mhe. Lissu: Je kuna utaratibu wa kisheria kuhusu mambo haya?
Wakili Maduhu: nimekutana nao ukonga. Haujawahi kuwepo.
Mhe. Lissu: Kwani wewe una makosa gani ya Bwana Jela wa Ukonga?
Wakili Maduhu: Sifahamiani nae sijui nilichomkosea.
Mhe. Lissu: Wakati umeruhusiwa kuja kuniona Juma Mwaibako ndio alikuwa anakaimu ukuu wa gereza?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe. Lissu: Huyu aliyekuzuia ni Andrew Shabani ndio aliyekuzuia?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe una tatizo la ngozi? Albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Kwenye hili Taifa kuna ubaguzi wa watu wenye albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa Wakili aliyezuiwa ni wewe mwenye albinism?
Wakili Maduhu: Ni mimi peke yangu ndio nimekataliwa by implication.
Mhe. Lissu: ulipenda uwe albino?
Wakili Maduhu: Sikupenda. Ila ndio nimebaguliwa hivyo.
Mhe. Lissu: Nilisema naomba samahani.
Shahidi ametoa machozi na kuumia sana juu ya vitendo hivi. Watu wameumia sana hapa Mahakamani wanaofuatilia kesi hii. Matendo haya ni ya kinyama sana.🥹
Mhe. Lissu: Niliandika orodha ya pili na kuwaongeza wewe na Kisabo kwenye hiyo orodha ya pili. Niliwaongeza wewe na Kisabo na hatimaye Kisabo akaanza kuruhusiwa na wewe ukaendelea kuzuiwa kuingia.
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Nikaandika orodha nyingine na kuwaongeza Wakili Deogratias Mahinyila, Dickson Matata na mawakili wengine kwenye hiyo orodha ya pili.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Anayetunza hizo nyaraka ni Mjibu maombi wa tatu ambae ni Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama mawakili ambao hawapo kwenye hiyo orodha na wameruhusiwa kuja kuniona.
Neema Saruni
Denis Luwis
Nyaronyo Kichere
Unafahamu kama wameruhusiwa kuja kuniona na hawapo kwenye orodha ya mawakili waliokuja kunitembelea.
Wakili Maduhu: Nafahamu ndio.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli kwamba mara ya kwanza mlipokuja kuniona hatukuonana ana kwa ana bali mlipelekwa kwenye chumba chenye ukuta wa kioo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo msingeweza kunipa mkono mkasema Mwenyekiti Pole?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na namna pekee ya mawasiliano kwa siku hiyo ilikuwa ni simu upande wenu na upande wangu?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Part 5
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Kama kulikuwa na simu ambazo tulitumia kuongea je uwezekaano wa mazungumzo yetu kuwa recorded upo au haukuwepo?
Wakili Maduhu: Ulikuwepo mkubwa sana maaana mazungumzo yote huwa yanarekodiwa kupitia hizi simu ziwe za kawaida au mapolisi.
Mhe. Lissu: Soma kanuni za magereza sasa. Hizi hapa. Soma reg. 13 kama askari magereza anaruhusiwa mazungumzo ya wakili na mteja wake ambae ni mfungwa?
Wakili Maduhu: harusiwi kabisa kusikiliza. Anatakiwa kukuona tu na sio kukusikiliza.
Mhe. Lissu: sasa hawa wanasikiliza kwa ajili ya nini? Umbea au nini?
Wakili Maduhu: Nafikiri utakuwa ni umbea wao sio sheria kabisa.
Mhe. Lissu: Twende kwenye Sheria ya Magereza, Sura ya 58 nenda kifungu cha 8 sema kama kinazungumzia wajibu wa kisheria wa Bwana jela.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa mujibu wa kifungu hicho Bwana Jela ana wajibu wa kusimamia maaskari wake kutekeleza sheria hii?
Wakili Maduhu: Ndio wajibu wake.
Mhe. Lissu: Je anaweza kupuuza sheria ya magereza na kanuni za magereza na kuleta mambo yake anayoyajua mwenyewe?
Wakili Maduhu: Hana mamlaka hayo kabisa. Sheria ndio inapaswa kufuatwa.
Mhe. Lissu: Je Mkuu wa Gereza huyu Bwana Jela ametekeleza sheria ya magereza?
Wakili Maduhu: Hajafanya hivyo kabisa.
Mhe. Lissu: Ukiachana na ile siku tuliyoongea kwa simu lakini amra zingine mbili nilipoonana na wewe tulikutana admission ofisi ambayo ikoje?
Wakili Maduhu: Kuna meza tatu zote zina maaskari wa magereza wamekaa wanasikiliza na wewe ukiletwa unaambatana na maaskari wengine wa magereza wawili watatu. Kwahiyo wote hawa wanasikiliza kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hiyo sio kinyume na sheria?
Wakili Maduhu: Ni kinyume kabisa na Sheria wanayosikiliza hayawahusu. Wangetaka kusikiliza wangesoma uwakili wasiwe maaskari magereza. Wangezungumza na mahabusu na wafungwa kama mawakili. Huu mwingine ni umbea kwakweli.
Mhe. Lissu: Haya nakurudishia kanuni za usimamizi wa magereza. Je kanuni ya 31(3)(a) mfungwa anayepaswa kuangaliwa usiku na mchana na maaskari wasiopungua wawili ni mfungwa aliyehukumiwa kifo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa. Hakuna mfungwa mwingine yeyote anayepaswa kufanyiwa hivyo.
Mhe. Lissu: Je mimi ni mfungwa?
Wakili Maduhu: Wewe sio mfungwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je natendewa sawa na mfungwa wa kifo kwa hiki nilichosema au kinachoendelea?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa unatendewa hivyo na hawa Mabwana.
Mhe. Lissu: Sasa turudi kwenye Supplimentary affidavit ya mjibu maombi wa tatu ambae ni BWANA JELA. Sasa nataka usome maoni ya officer in charge kwa kila wakili anayekuja Ukonga. Anza na SUPP 2 soma hayo maoni ya huyu Bwana. Amesema SIMAMIA MAZUNGUMZO HAYO.
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu anamsomea majina ya mawakili wengi waliomtembelea na maoni ya Bwana Jela anasema simamia mazungumzo yao. Kila mahali Bwana Jela anasema simamia mazungumzo hayo, Hakikisha unashuhudia hayo mazungumzo. 😂😂
Mhe. Lissu: Soma hapo Nashon Nkungu maoni ya Mkuu wa Gereza yanasemaje?
Wakili Maduhu: Simamia mazungumzo yao kwa karibu sana. Fuatilia wanachozungumza.
Mhe. Lissu: Kwahiyo maoni yake kwa mawakili wangu kila wanapokuja ni kutaka mazungumzo yasimamiwe na maafisa usalama wa magereza, wanasheria wa magereza pia.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa wapo mawakili wa serikali huwa wanatembelea gerezani pia?
Wakili Maduhu: Ni sahihi
Mhe. Lissu: Twende SUPP 4 kuna maafisa waliotoka NPS mamlaka ya mashitaka. DPP yaani. Tar. 09/11/2025 kuna mtu anaitwa Debora Mushi anatokea NPS, Mwingine Carolina Nana na wengine wengi. Sema maoni ya Bwana Jela yalikuwa ni nini?
Wakili Maduhu: Maoni yao anasema WASIKILIZWE KWA UTARATIBU.
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Duuh sasa mawakili binafsi neno utaratibu halijasemwa kokote lakini hawa wa Serikali neno Utaratibu ndio limewekwa. Haya soma pia kokote walipokuja mawakili wa serikali pameandikwaje?
Wakili Maduhu: Wasikilizwe na wapewe nafasi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kuna ubaguzi kati ya mawakili wa serikali na mawakili binafsi?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Ubaguzi wa aina hii unaruhusiwa kwa sheria za Tanzania?
Wakili Maduhu: Hauruhusiwi kabisa kabisa.
Mhe. Lissu: Mawakili waliotendewa hivi ni zaidi ya mawakili 36 ukiachana na wakwangu ni mawakili wa watu wengine pia.
Wakili Maduhu: Kwa kiasi kikubwa mawakili wote tunatendewa huo unyama.
Mhe. Lissu: Annexure A3 ni hukumu ya Jaji Mkwizu ya Tar. 11/07/2025 haya malalamiko ya kuingiliwa mawasiliano kati ya mawakili wangu sikuyafikisha mahakamani ya yakatolewa maamuzi na mahakamu kuu.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na malalamiko haya yanahusiana na ukiukwaji wa kanuni ya 13 ya uendeshaji wa Magereza?
Wakili Maduhu: sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Licha ya maelekezo hayo ya Jaji Mkwizu kwamba watekeleze sheria je ulitekelezwa na magereza?
Wakili Maduhu: Haukutekelezwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je mambo haya niliyaeleza pia kule Kisutu kuhusu mawasiliano yangu?
Wakili Maduhu: Sahihi. Hata hapa Mahakama Kuu ukisema hayo Mahakama kuu kwenye kesi yako ya uhaini.
Mhe Tundu Lissu: Kwahiyo malalamiko yangu nimeyawasilisha kwa watu wanaotambulika kisheria.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Twende annexure A4 kwamba kikosi kazi kinachoshughulikia watu wanaofungwa hovyo hovyo cha umoja wa mataifa mimi nimetajwa na kesi yangu kwasababu kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimepelekewa malalamiko yangu na wamesema haya mambo yakomeshwe? Kweli au si kweli.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hawa ambao hawataki kutii sheria akiwemo Bwana Jela wakati kuna mwongozo wa umoja wa mataifa?
Wakili Maduhu: Sijui wanataka waambiwe na nani hawa.
Mhe. Lissu: au wanataka twende kwa Mungu tufe ndio tutapata hiyo haki yetu?
Wakili Maduhu: Nafikiri hatujakosea kuja hapa mahakamani.
Mhe. Lissu: Nimemaliza mimi.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola na yeye anataka kumuuliza swali Wakili Maduhu william.
Anasimama Lissu anasema hilo jambo hawakuomba.
Jaji anasema Stanley Kalokola na wewe uulize hayo maswali yako.
Wakili wa Serikali Kalokola: Wewe ni Wakili.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Una uzoefu wa miaka mingapi?
Wakili Maduhu: Miaka 6.
Wakili wa Serikali Kalokola: Respondent wa nne nae mmemshitaki hapa? Ambae ni Lissu.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: kuna mahali kokote ulililalamikia suala hili kwa Jaji Mkwizu?
Wakili Maduhu: Halipo.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulibaguliwa kwasababu ya rangi yako kuna muhali umesema kwenye kiapo chako?
Wakili Maduhu: Siwezi kuwa na uhakika.
Wakili wa Serikali Kalokola: Onesha uliposema asikilizwe?
Wakili Maduhu: ameonesha maeneo matatu.
Wakili wa Serikali Kalokola: ulitembelea magereza mara nyingi na je jina lako lipo kuonesha uliandikwa jina?
Wakili Maduhu: niliandikwa mara tatu tu baada ya hapo sikuwahi kuandikwa tena licha ya kwenda.
Wakili wa Serikali Kalokola: Je waliokuwa wanakusikiliza ni akina nani?
Wakili Maduhu: Mkuu wa gereza na wenzake walikuwa wananisikiliza. Surveilance ya kufa mtu.
Wakili wa Serikali Kalokola; Ni hayo tu Waheshimiwa majaji.
Wakili Maduhu William amemaliza kuhojiwa sasa muda unaangaliwa kama unatosha. Tayari saa 10 na nusu kwahiyo Wakili wa Serikali ameomba waahirishe tuanze kesho asubuhi.
Majaji wanasema tukutane kesho J'4 tarehe 21/7/2026 saa tatu asubuhi.
Soma pia: Lissu afikishwa mahakamani leo, ulinzi waimarishwa
Soma pia: Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna wa Magereza na Mkuu wa Gereza kuu la Ukonga
Na soma pia:
Kumbuka hili ni Shauri la kikatiba Na. 7300 lililofunguliwa na mawakili Maduhu William, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Lengo la shauri hili ni kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea, vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu mmojawao akiwa mahabusu mteja wao Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA (T)...
Leo baada wadaiwa kuwa wamewasilisha viapo vyao kinzani, Shauri limeanza kusikilizwa rasmi kwa Tundu Lissu kuwadodosa walalamikaji ili kuthibitisha uhalali wa madai yao kisheria....
Wa kwanza kudodoswa na Tundu Lissu ni mlalamikaji Na. 1 Wakili William Maduhu. Fuatilia dodoso hii na Kisha re - Examination ya mawakili wa upande wa walalamikiwa - Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bwana Jela wa Gereza la Ukonga na Kamishina wa Magereza..
===================
Part 1Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
=====================
Part 2.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Nenda ukurasa wa 27 angalia defence counsels angalia jina la Kulwa Maduhu na Paul Kisabo kama hayapo?
Wakili Maduhu: Yapo majina ya hao mawakili.
Mhe. Lissu: Ukurasa wa 40 kwenye huo mwenendo wa Kisutu angalia upande wa corum useme kama Paul Kisabo na Kulwa Maduhu.
Wakili Maduhu: Wapo wote wawili.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kuna utaratibu wowote wa kisheria wa unaopaswa kuufuata kumuona mteja?
Wakili Maduhu: Hakuna utaratibu wowote wa kisheria zaidi ya kuonesha kitambulisho tu cha uwakili.
Mhe. Lissu: Haya Maneno ya Bwana jela kuwa sijakutambulisha ni maneno ya bure tu?
Wakili Maduhu: Kabisa maneno ya bure kabisa.
Mhe. Lissu: Unazifahamu kanuni za maadili za mawakili?
Wakili Maduhu: Nazijua ndio.
Mhe. Lissu: Je kwa kanuni hizi wakili anaruhusiwa kumuonesha makubaliano yake na mteja mtu anayeitwa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Duty to confidentiality hairuhusu. Kwahiyo siruhusiwi kabisa kutoa siri za mteja wangu.
Mhe. Lissu: Sasa unasemaje kuhusu hizi habari za Bwana Jela kuwa sijakutambulisha kwake?
Wakili Maduhu: Hizo ni kauli za bure kabisa. Mimi silazimiki kufanya hivyo. Nina miaka 6 ya uwakili kwa sasa huo utaratibu haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 41 hadi 43 wa proceedings za Kisutu. Soma Tar. 16/06 sema kama mahakama ya Kisutu haikuandika malalamiko yangu kuhusu mawakili wangu kunyimwa kuniona.
Wakili Maduhu: Ni kweli malalamiko yapo.
Mhe. Lissu: Ni kwamba nilikuwa nazuiwa kuonana na mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Kweli yapo hapa
Mhe.Lissu: Kwamba ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa magereza?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa yapo yote kwenye hizi kurasa za mambo ya Kisutu.
Mhe. Lissu: Pia kuna malalamiko specific kuwa kitendo hicho cha mimi kuninyima nisionane na mawakili wangu ni kinyume na sheria na kanuni za kimataifa?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Nikalalamika kuwa naishi na wafungwa waliohukumiwa kifo? Na natendewa sawa na watu hao?
Wakili Maduhu: Kweli kabisa ulisema.
Mhe. Lissu: Baada ya hayo nilisema nitajiwakilisha mwenyewe kwasababu sitaki mawakili wangu waje kulaumiwa bure?
Wakili Maduhu: Ni kweli ulisema hivyo na ikawa hivyo.
Mhe. Lissu: Ulipoamua kujiwakilisha mwenyewe nilisema waendelee kunisahuri na kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea. Nilisema hivyo?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze toka siku hiyo tar. 16/05/2026 hadi leo mmeendelea kunipa ushauri wa kisheria na kunipa nyaraka Gerezani?
Wakili Maduhu: Ni kweli tumeendelea kufanya kazi hiyo.
Mhe. Lissu: Je una kumbukumbu za kilichotokea Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo lilipofika Mahakama kuu niliwaeleza waheshimiwa majaji kuwa nina mawakili wanaonisaidia kwa research na ushauri.
Wakili Maduhu: Ni sahihi ulisema.
Mhe. Lissu: Naomba nimuonyeshe proceedings za Mahakama Kuu. Tuambie from page 4 to 6 wambie majaji kama huo mwenendo unaonesha niliwaambia Majaji wa Mahakama kuu nina mawakili ambao wananisaidia na nikaomba waingizwe kwenye column.
Wakili Maduhu: Nimeona ndio.
Mhe. Lissu: Na Katuga alipinga ombi langu hilo.
Wakili Maduhu: Ni sahihi naona hapa.
Mhe. Lissu: Mahakama ikasema hatutawaingiza kwenye corum lakini mawakili wako waendelee kukusaidia?
Wakili Maduhu: Naona iko hapa.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni kweli sio tu Kisutu hata Mahakama kuu hii inakutambua wewe na wenzako kama mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
=======================
Part 3
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe.Lissu: Nenda kwenye supplementary affidavit ya wajibu maombi wa 3 ya Tarehe 12/05 anasema kuwa wewe na Paul Kisabo hampo kwemye orodha ya mawakili niliyowasilisha kwake?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Amewasilisha SUPP 1 kwenye supplimentary affidavit na anasema hakuna jina la Kulwa maduhu na Paul Kisabo. Sasa angalia hiyo annexure SUPP 1 na uwaeleze majaji kama maneno yake haya ni ya kweli?
Wakili Maduhu: Kwenye SUPP 1 hayapo.
Mhe. Lissu: Je pamoja na wewe na Paul Kisabo kutokuwepo kwenye orodha hii mmewahi kuja kuniona gerezani na kuongea na mimi?
Wakili Maduhu: Ni sahihi tumewahi kuja na kama mara tatu nimewahi kuingia na kuja kukuona.
Mhe.Lissu: Katika hizo mara tatu zote je ulijiandikisha pale magereza kabla ya kuniona na ukaonesha kitambulisho chako?
Wakili Maduhu: Sahihi nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu: Je wewe ni mtunzaji wa hizo kumbukumbu za watu wanaoingia na kutoka Gereza la Ukonga?
Wakili Maduhu: Sio mimi kabisa. Ni Bwana Jela huyo hapo amekaa kwenye kiti ndio kazi yake. Anamuonesha kwa kidole chake.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama jina lako lipo kwa watu waliotembelea gereza?
Wakili Maduhu: Ndio tar. 28/10 jina langu lipo lakini hii siku sikumuona niliambiwa sitaweza kumuona. Na mara tatu zote nilizowahi kumuona hizo nyaraka hazijaletwa na Bwana Jela. Mkuu wa Gereza yani.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 2 angalia hiyo nyaraka halafu useme item no. 10 aliyekuja ambae ni Paul Kisabo ameoneshwa jina lake na shida yake wameandika shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Namuona hapa ndio yupo.
Mhe. Lissu: Tarehe 30/09 angalia jina la kwanza hapo la watu waliotembelea Gerezani ni akina nani?
Wakili Maduhu: Jina ni la Paul Kisabo.
Mhe. Lissu: Je yupo kwenye ile orodha ya kwanza ya watu niliowatambulisha kwa mujibu wa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Kule hayupo.
Mhe. Lissu: Kumbe hayupo kule na magereza walimruhusu aingie?
Wakili Maduhu: Ndio kabisa
Mhe. Lissu: Nenda sasa SUPP 3 na yenyewe. Majina ya mawakili unaowaona na wataje.
Wakili Maduhu: Andrew Mathew Chima na Nashon Nkungu.
Mhe. Lissu: Hao mawakili walikuja kuniona mimi?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe.Lissu: Huyo Andrew aliyekuja kuniona ni mmoja wao au sio mmoja wao kwenye ile orodha aliyosema Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hayumo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 5 sasa kwenye hicho kielelezo ni register book ya Gereza la Ukonga. Pembeni imeandikwa SUPP 5 ukurasa unaofuata unaonesha entry ya Tar. 07/05 mwaka jana kuna mtu wa kwanza kabisa anaitwa Nashon Nkungu kazi yake ni wakili amekuja kumuona Mahabusu Tundu Lissu. Shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kwanini aliruhusiwa kuja kuniona huyo Nashon.
Wakili Maduhu: kwasababu ni wakili wako.
Mhe. Lissu: Tarehe inayofuata aliruhusiwa tena kuingia?
Wakili Maduhu: Ndio anaonekana hapa kwenye ukurasa unaofuata. Kwenye kurasa kadhaaa. Ukurasa wa 9 na tarehe 28/07 alikuwa mtu wa kwanza kuja kukuona.
MheLissu: Tar. 24/12 jina namba 2 ni Nashon Nkungu tena?
Wakili Maduhu: kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Kisabo je yupo au hayupo?
Wakili Maduhu: Na Kisabo nae yupo kabisa.
Mhe. Lissu: 04/03/2026 mtu wa pili Nashon Nkungu aliruhusiwa kuja kuniona?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
===================
Part 4
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Twende Annexure SUPP 6 angalia Tarehe 12/12/2025 mtu wa pili ameandikwa Paul Emanuel Kilasa Kisabo na yeye alikuja kuniona na akaruhusiwa?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa Mawakili wangu aliyekatazwa kuja kuniona ni wewe peke yako?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa tuje kwenye sababu za kukukatalia wewe kuja kuniona. Soma Annexure SUPP 3 entry ya Tar. 28/10/2025 je siku hiyo ulikwenda Gereza la Ukonga na Wakili mwenzako Gaston Garubindi?
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Nenda kwenye SUPP 1 ile orodha na wambie majaji kama Gaston Garubindi yupo kwenye hiyo orodha?
Wakili Maduhu: Jina lake ni namba 3.
Mhe. Lissu: sasa angalia hiyo nyaraka sawasawa imeandika mambo mengi kule mwisho kuna maoni ya OC ni officer in charge yaani BWANA JELA.
Ameandika maoni yake kuwa aruhusiwe kumuona ambae yupo kwenye orodha ya mawakili. Na huyo mwingine asiruhusiwe kwasababu hayupo kwenye hiyo orodha.
Wakili Maduhu: Niliambiwa toka hapa haupo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Je kuna Wakili mwingine ameandikiwa maoni ya namna hiyo kwenye orodha ya mawakili wangu kuwa asinione hayupo kwenye majina niliyompa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hakuna wakili mwingine.
Mhe. Lissu: Je kuna utaratibu wa kisheria kuhusu mambo haya?
Wakili Maduhu: nimekutana nao ukonga. Haujawahi kuwepo.
Mhe. Lissu: Kwani wewe una makosa gani ya Bwana Jela wa Ukonga?
Wakili Maduhu: Sifahamiani nae sijui nilichomkosea.
Mhe. Lissu: Wakati umeruhusiwa kuja kuniona Juma Mwaibako ndio alikuwa anakaimu ukuu wa gereza?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe. Lissu: Huyu aliyekuzuia ni Andrew Shabani ndio aliyekuzuia?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe una tatizo la ngozi? Albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Kwenye hili Taifa kuna ubaguzi wa watu wenye albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa Wakili aliyezuiwa ni wewe mwenye albinism?
Wakili Maduhu: Ni mimi peke yangu ndio nimekataliwa by implication.
Mhe. Lissu: ulipenda uwe albino?
Wakili Maduhu: Sikupenda. Ila ndio nimebaguliwa hivyo.
Mhe. Lissu: Nilisema naomba samahani.
Shahidi ametoa machozi na kuumia sana juu ya vitendo hivi. Watu wameumia sana hapa Mahakamani wanaofuatilia kesi hii. Matendo haya ni ya kinyama sana.🥹
Mhe. Lissu: Niliandika orodha ya pili na kuwaongeza wewe na Kisabo kwenye hiyo orodha ya pili. Niliwaongeza wewe na Kisabo na hatimaye Kisabo akaanza kuruhusiwa na wewe ukaendelea kuzuiwa kuingia.
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Nikaandika orodha nyingine na kuwaongeza Wakili Deogratias Mahinyila, Dickson Matata na mawakili wengine kwenye hiyo orodha ya pili.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Anayetunza hizo nyaraka ni Mjibu maombi wa tatu ambae ni Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama mawakili ambao hawapo kwenye hiyo orodha na wameruhusiwa kuja kuniona.
Neema Saruni
Denis Luwis
Nyaronyo Kichere
Unafahamu kama wameruhusiwa kuja kuniona na hawapo kwenye orodha ya mawakili waliokuja kunitembelea.
Wakili Maduhu: Nafahamu ndio.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli kwamba mara ya kwanza mlipokuja kuniona hatukuonana ana kwa ana bali mlipelekwa kwenye chumba chenye ukuta wa kioo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo msingeweza kunipa mkono mkasema Mwenyekiti Pole?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na namna pekee ya mawasiliano kwa siku hiyo ilikuwa ni simu upande wenu na upande wangu?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
======================
Part 5
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Kama kulikuwa na simu ambazo tulitumia kuongea je uwezekaano wa mazungumzo yetu kuwa recorded upo au haukuwepo?
Wakili Maduhu: Ulikuwepo mkubwa sana maaana mazungumzo yote huwa yanarekodiwa kupitia hizi simu ziwe za kawaida au mapolisi.
Mhe. Lissu: Soma kanuni za magereza sasa. Hizi hapa. Soma reg. 13 kama askari magereza anaruhusiwa mazungumzo ya wakili na mteja wake ambae ni mfungwa?
Wakili Maduhu: harusiwi kabisa kusikiliza. Anatakiwa kukuona tu na sio kukusikiliza.
Mhe. Lissu: sasa hawa wanasikiliza kwa ajili ya nini? Umbea au nini?
Wakili Maduhu: Nafikiri utakuwa ni umbea wao sio sheria kabisa.
Mhe. Lissu: Twende kwenye Sheria ya Magereza, Sura ya 58 nenda kifungu cha 8 sema kama kinazungumzia wajibu wa kisheria wa Bwana jela.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa mujibu wa kifungu hicho Bwana Jela ana wajibu wa kusimamia maaskari wake kutekeleza sheria hii?
Wakili Maduhu: Ndio wajibu wake.
Mhe. Lissu: Je anaweza kupuuza sheria ya magereza na kanuni za magereza na kuleta mambo yake anayoyajua mwenyewe?
Wakili Maduhu: Hana mamlaka hayo kabisa. Sheria ndio inapaswa kufuatwa.
Mhe. Lissu: Je Mkuu wa Gereza huyu Bwana Jela ametekeleza sheria ya magereza?
Wakili Maduhu: Hajafanya hivyo kabisa.
Mhe. Lissu: Ukiachana na ile siku tuliyoongea kwa simu lakini amra zingine mbili nilipoonana na wewe tulikutana admission ofisi ambayo ikoje?
Wakili Maduhu: Kuna meza tatu zote zina maaskari wa magereza wamekaa wanasikiliza na wewe ukiletwa unaambatana na maaskari wengine wa magereza wawili watatu. Kwahiyo wote hawa wanasikiliza kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hiyo sio kinyume na sheria?
Wakili Maduhu: Ni kinyume kabisa na Sheria wanayosikiliza hayawahusu. Wangetaka kusikiliza wangesoma uwakili wasiwe maaskari magereza. Wangezungumza na mahabusu na wafungwa kama mawakili. Huu mwingine ni umbea kwakweli.
Mhe. Lissu: Haya nakurudishia kanuni za usimamizi wa magereza. Je kanuni ya 31(3)(a) mfungwa anayepaswa kuangaliwa usiku na mchana na maaskari wasiopungua wawili ni mfungwa aliyehukumiwa kifo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa. Hakuna mfungwa mwingine yeyote anayepaswa kufanyiwa hivyo.
Mhe. Lissu: Je mimi ni mfungwa?
Wakili Maduhu: Wewe sio mfungwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je natendewa sawa na mfungwa wa kifo kwa hiki nilichosema au kinachoendelea?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa unatendewa hivyo na hawa Mabwana.
Mhe. Lissu: Sasa turudi kwenye Supplimentary affidavit ya mjibu maombi wa tatu ambae ni BWANA JELA. Sasa nataka usome maoni ya officer in charge kwa kila wakili anayekuja Ukonga. Anza na SUPP 2 soma hayo maoni ya huyu Bwana. Amesema SIMAMIA MAZUNGUMZO HAYO.
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu anamsomea majina ya mawakili wengi waliomtembelea na maoni ya Bwana Jela anasema simamia mazungumzo yao. Kila mahali Bwana Jela anasema simamia mazungumzo hayo, Hakikisha unashuhudia hayo mazungumzo. 😂😂
Mhe. Lissu: Soma hapo Nashon Nkungu maoni ya Mkuu wa Gereza yanasemaje?
Wakili Maduhu: Simamia mazungumzo yao kwa karibu sana. Fuatilia wanachozungumza.
Mhe. Lissu: Kwahiyo maoni yake kwa mawakili wangu kila wanapokuja ni kutaka mazungumzo yasimamiwe na maafisa usalama wa magereza, wanasheria wa magereza pia.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa wapo mawakili wa serikali huwa wanatembelea gerezani pia?
Wakili Maduhu: Ni sahihi
Mhe. Lissu: Twende SUPP 4 kuna maafisa waliotoka NPS mamlaka ya mashitaka. DPP yaani. Tar. 09/11/2025 kuna mtu anaitwa Debora Mushi anatokea NPS, Mwingine Carolina Nana na wengine wengi. Sema maoni ya Bwana Jela yalikuwa ni nini?
Wakili Maduhu: Maoni yao anasema WASIKILIZWE KWA UTARATIBU.
========================
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Duuh sasa mawakili binafsi neno utaratibu halijasemwa kokote lakini hawa wa Serikali neno Utaratibu ndio limewekwa. Haya soma pia kokote walipokuja mawakili wa serikali pameandikwaje?
Wakili Maduhu: Wasikilizwe na wapewe nafasi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kuna ubaguzi kati ya mawakili wa serikali na mawakili binafsi?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Ubaguzi wa aina hii unaruhusiwa kwa sheria za Tanzania?
Wakili Maduhu: Hauruhusiwi kabisa kabisa.
Mhe. Lissu: Mawakili waliotendewa hivi ni zaidi ya mawakili 36 ukiachana na wakwangu ni mawakili wa watu wengine pia.
Wakili Maduhu: Kwa kiasi kikubwa mawakili wote tunatendewa huo unyama.
Mhe. Lissu: Annexure A3 ni hukumu ya Jaji Mkwizu ya Tar. 11/07/2025 haya malalamiko ya kuingiliwa mawasiliano kati ya mawakili wangu sikuyafikisha mahakamani ya yakatolewa maamuzi na mahakamu kuu.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na malalamiko haya yanahusiana na ukiukwaji wa kanuni ya 13 ya uendeshaji wa Magereza?
Wakili Maduhu: sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Licha ya maelekezo hayo ya Jaji Mkwizu kwamba watekeleze sheria je ulitekelezwa na magereza?
Wakili Maduhu: Haukutekelezwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je mambo haya niliyaeleza pia kule Kisutu kuhusu mawasiliano yangu?
Wakili Maduhu: Sahihi. Hata hapa Mahakama Kuu ukisema hayo Mahakama kuu kwenye kesi yako ya uhaini.
Mhe Tundu Lissu: Kwahiyo malalamiko yangu nimeyawasilisha kwa watu wanaotambulika kisheria.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Twende annexure A4 kwamba kikosi kazi kinachoshughulikia watu wanaofungwa hovyo hovyo cha umoja wa mataifa mimi nimetajwa na kesi yangu kwasababu kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimepelekewa malalamiko yangu na wamesema haya mambo yakomeshwe? Kweli au si kweli.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hawa ambao hawataki kutii sheria akiwemo Bwana Jela wakati kuna mwongozo wa umoja wa mataifa?
Wakili Maduhu: Sijui wanataka waambiwe na nani hawa.
Mhe. Lissu: au wanataka twende kwa Mungu tufe ndio tutapata hiyo haki yetu?
Wakili Maduhu: Nafikiri hatujakosea kuja hapa mahakamani.
Mhe. Lissu: Nimemaliza mimi.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola na yeye anataka kumuuliza swali Wakili Maduhu william.
Anasimama Lissu anasema hilo jambo hawakuomba.
Jaji anasema Stanley Kalokola na wewe uulize hayo maswali yako.
Wakili wa Serikali Kalokola: Wewe ni Wakili.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Una uzoefu wa miaka mingapi?
Wakili Maduhu: Miaka 6.
Wakili wa Serikali Kalokola: Respondent wa nne nae mmemshitaki hapa? Ambae ni Lissu.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: kuna mahali kokote ulililalamikia suala hili kwa Jaji Mkwizu?
Wakili Maduhu: Halipo.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulibaguliwa kwasababu ya rangi yako kuna muhali umesema kwenye kiapo chako?
Wakili Maduhu: Siwezi kuwa na uhakika.
Wakili wa Serikali Kalokola: Onesha uliposema asikilizwe?
Wakili Maduhu: ameonesha maeneo matatu.
Wakili wa Serikali Kalokola: ulitembelea magereza mara nyingi na je jina lako lipo kuonesha uliandikwa jina?
Wakili Maduhu: niliandikwa mara tatu tu baada ya hapo sikuwahi kuandikwa tena licha ya kwenda.
Wakili wa Serikali Kalokola: Je waliokuwa wanakusikiliza ni akina nani?
Wakili Maduhu: Mkuu wa gereza na wenzake walikuwa wananisikiliza. Surveilance ya kufa mtu.
Wakili wa Serikali Kalokola; Ni hayo tu Waheshimiwa majaji.
Wakili Maduhu William amemaliza kuhojiwa sasa muda unaangaliwa kama unatosha. Tayari saa 10 na nusu kwahiyo Wakili wa Serikali ameomba waahirishe tuanze kesho asubuhi.
Majaji wanasema tukutane kesho J'4 tarehe 21/7/2026 saa tatu asubuhi.
Soma pia: Lissu afikishwa mahakamani leo, ulinzi waimarishwa
Soma pia: Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna wa Magereza na Mkuu wa Gereza kuu la Ukonga
Na soma pia:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga tarehe 1 hadi 3 Julai 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.
Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga. Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya...

- Nyakijooga
- Replies: 10
- Forum: Jukwaa la Siasa