Updates: Kukamatwa kwa Wanachama wa CHADEMA Kanisani Mwanza

Mkuu mbona unajiuliza maswali magumu hivyo, utadhani Jeshi letu limetoka Pluto? Wakati ndio watu wale wale waliokuwepo Mwangosi akipoteza maisha n.k n.k
Dah! Na walikuepo wakati Alphonse Mawazo anauwawa! Mungu awape mwisho mbaya
 
Naona mleta mada kaamua kumlisha maneno baba askofu kwa maslahi ya chama. Sifikirii kama chama cha upinzan Zambia kingeweza kushinda kwa kutumia propanga chovu za aina hii.
 
Swali ni moja kwa wanachama na wafuasi wa CHADEMA na waTanzania wengine wanaokataa manyanyaso.

Je, kuwekwa mahabusu ndiyo iwe sababu ya kuogopa kuendeleza mapambano haya ya kutafuta Uhuru na HAKI?

Jibu ni lazima liwe, HAPANA, na ningeshauri CHADEMA wajipange vizuri kuyaeneza mapambano ya aina hii kila sehemu ya nchi yetu.

Hawa wapambanaji wanaowekwa mahabusu kwa uonevu hivi ingefaa pawe na utaratibu wa chama kuwatambua na kuwatunuku heshima maalum ya kujitoa kwao kutafuta uhuru kwa wengine wote.
Chama kiwe na njia nzuri ya kuwapongeza, hata kama ni kwa kuwatambua tu mchango wao kwa kuwatunuku SHAHADA inayoeleza kukaa kwao mahabusu, tarehe, mahala, n.k.
 
hatangaze tu kuwa hakuna kwenda kanisani na gwanda
 
Kwanini mvae nguo za chama kanisani? Acheni ujinga
 
Ndiyo, walikuwa wamevaa sare za chama.Taifa huongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria na wala siyo kwa mujibu wa hisia za watu au matamanio ya watu.Kwani kuna sheria wamevunja kwa kwenda kanisani wakiwa wamevaa sare za chama?
Yaani Pro-Ccm ni wajinga sana na hapa wanajifanya wao ndio Polisi eti! Wapuuzi sana
 
Ushauri murua sana huyu! Barikiwa
 
Maswali yote haya ni ya nini?

Polisi, kama jeshi lolote wanafuata amri wanazopewa na wakuu wao, usilaumu polisi kiujumla hivyo!

Pili, unaweza kuwa unalalamikia usichokijuwa.

Je, unajuaje kwamba polisi wanafanya wanayofanya ili kuharakisha anguko la hao wanaowatuma?
 
Askofu Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya Wana Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula.

Je hiyo kanisa waumini wanawajibika kutaja vyama vyao?
 
Acha waopate kwanini wanapeleka ushabiki wa vyama makanisani! Viva Polisi
 
Hapo ndipo kuna shida wala tusilaumu polisi ila chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…