Elections 2015 Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

Elections 2015 Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

laurence masha anakabidhiwa kadi na mbowe
daniel porokwa - katibu wa ccm manyara
robinson mwenyekiti wa uv ccm arusha
sioi sumari
mafuriko ya arusha yamewazoa na kuwatakatisha.

hii safi sana maana hata el akishinda kwa uhakika kabisa ataunda serikali yenye 4u movement wengi pamoja na friends of el. M4c na bavicha watakuwa wachache sana, kwa maana nyingine itaundwa serikali ya ccm ndani ya ukawa. Anaebisha abishe tu.
 
Waliojiunga na CHADEMA:
Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
Sioi Sumari
Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
Mgombea ubunge Simanjiro
Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima

Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu
Gari la taka limeandaliwa uwanjani kwa ajili ya kutupia kadi za ccm
Wazee wa kimila wanamvika uchifu Mh Lowassa
Lau Masha:
Maamuzi magumu yamefanyika hivi leo, lakini ni maamuzi muhimu, sitaongea leo, nitangaze tu kwamba nimejiunga rasmi chadema
Robinson m/kiti uvccm:
Wale Wakristo kuna wimbo unaosema Nimetoka kwa Farao misri sirudi tena.
Kuna kijana moja kazi yake ni kuongea uchafu, anasema oil chafu, anasahau oil chafu ndiyo inayoendesha mitambo.
Anasema Ufalme ukianguka sheria haina budi kubadilika.
Nataka niwaambie tunazijua mbinu zao zote, waandike maumivi maana ikulu tunaenda maana inatuhusu.
Lowassa anasema tumechoka na umaskini, tunakwenda kuwasaidia vijana kuhusu ajira.
Watanzania tuna fimbo yetu ya kuwapiga ccm, nayo ni kadi ya kupiga kura
Ole Medeye:
Anaimba kuwa Mwambie Kikwete nimezinduka, ccm sirudi tena.

Nimejitoa ccm kwa sababu mbili kuu, ya kwanza dhuluma imezidi ndani ya ccm, wanaapa kinafiki kuwa watailinda katiba ya nchi wakati wanaivunga, pili rushwa imekithiri katika taifa hili, nilifikiri kupitia ccm ningeshiriki kupiga vita rushwa, lakini matokeo yake kumbe niliowaamini kupiga vita rushwa ndiyo wanaotoa rushwa.

Hivyo nimejiondoa ccm ili tuweze kurudisha maadili ya nchi

ama kweli saa ya ukombozi imewadia....
hizo ni dalili nzuri za kuwachinjia baharini
magamba wote.....
 
M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
Nataka niseme maneno machache,
Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa
 
Heri wenye MOYO Safi mwana Hao °°°°°°°°°. Huwezi Kumtukana mtu kwa uamuzi wake, ni makosa, freedom of movement, your not satisfied with the situation just choose another one.
 
Mgana Msindai:
Nilikuwa M/kiti mkoa wa Singida na M/kiti wa wenyeviti wa mikoa Tanzania nzima, nimeona ndani ya ccm hakuna demokrasia, nimejiunga na CHADEMA ili niwe moja wa watakaohakikisha kuiondoa ccm madarakani
 
Breaking news from Arusha

Waliojiunga na CHADEMA:
Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
Sioi Sumari
Yona Nko aliyekuwa mkiti ccm mkoa Arusha
Mgombea ubunge Simanjiro
Goodluck Sipira katibu wa ccm Arusha anatokea Longido
Wazee wa kimila wa kimasai nchi nzima

Wazee wa kimila wa kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu
Moto wa mabua tuu huu!
Haunguzi hata handkerchief
Hivi Sioi bado alikuwa CCM? Masha alishinda kura za maoni kule Sengerema kweli?
 
Kumuona na kumpigia kura lowassa ni vitendo viwili tofauti""" umati wa watu sio tiketi ya lowassa kuwa rais,,, kaa ukijua tanzania ni kubwa sana na tuko zaidi ya 15 mil tuliojiandikisha,, je huo umati ni asilimia ngapi ya waarusha waliojiandikisha?? Vipi huo umati ni wangapi wana sifa za kupiga kura,, je huo umati unawageni wangapi ambao waliokuwa dar mbeya na leo ARusha?? Mabadiliko yanahitaji watu wenye dhamira ya dhati,,

kwahiyo wewe ulitaka ukusanyike umati wa " panya " kisha
ndipo uamini ya kwamba magamba wanakwenda kung'olewa meno bila ganzi ??
kura ni watu na watu wenyewe ndio sisi....sasa wewe jifariji tu kisha
uje kuanza kuangua kilio kama cha paka jizi baada ya oct 25,mwaka 2015.
 
Masha ni hasara. Ila ndo hivyo tena.

Atafata Karamagi kesho Mwanza, then Rostamu kisha Manji afu mchezo unamalizwa na JK kumchinjia baharini makomeo....

Jamaa wamejipanga kurudi kupitia mlango wa Chadema. Aibu!!

Hizo zinaitwa conspiracy mkuu, mothing is true..! JK na Edo hawaivi tena...
 
Subiri kampeni zianze.....!! UKAWA mmetangulia na baskeli ya mti......

Haya maneno ulipaswa kuwaambia CCM wakati mgombea wao anazunguka mikoani "kujitambulisha" mbwembwe zilikuwa nyingiii mkadhani mchezo umekwisha.UKAWA wanajibu mmeanza kuomba po!
 
Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
Sioi Sumari
Mafuriko ya arusha yamewazoa na kuwatakatisha.
Karibu sana cdm, hata hivyo chadema mna kazi pia ya kuchukua tahadhari ya kutambua na kuchuja mavumbi na papasi watakaoingia ndani wakati mnapofungua madisha ili kuruhusu hewa safi kuingia ndani. tayarisheni nyavu zenu za madirisha, vitambaa vya kufutia vumbi na dawa za kuulia wadudu mapema. Sio wote watakaomwita bwana bwana watauona ufalme wa mbinguni.
 
kwa hiyo breaking news! CCM Kwisha ndembendembe.
 
Subiri kampeni zianze.....!! UKAWA mmetangulia na baskeli ya mti......
Baiskeli yenye magurudumu ya barafu, jua likiwaka magurudumu yanayeyuka na safari inakuwa na mwisho.
 
Back
Top Bottom