Elections 2015 Updates Kutoka Arusha: Mkutano wa kumtambulisha mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA

laurence masha anakabidhiwa kadi na mbowe
daniel porokwa - katibu wa ccm manyara
robinson mwenyekiti wa uv ccm arusha
sioi sumari
mafuriko ya arusha yamewazoa na kuwatakatisha.

hii safi sana maana hata el akishinda kwa uhakika kabisa ataunda serikali yenye 4u movement wengi pamoja na friends of el. M4c na bavicha watakuwa wachache sana, kwa maana nyingine itaundwa serikali ya ccm ndani ya ukawa. Anaebisha abishe tu.
 

ama kweli saa ya ukombozi imewadia....
hizo ni dalili nzuri za kuwachinjia baharini
magamba wote.....
 
M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
Nataka niseme maneno machache,
Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa
 
Heri wenye MOYO Safi mwana Hao °°°°°°°°°. Huwezi Kumtukana mtu kwa uamuzi wake, ni makosa, freedom of movement, your not satisfied with the situation just choose another one.
 
Mgana Msindai:
Nilikuwa M/kiti mkoa wa Singida na M/kiti wa wenyeviti wa mikoa Tanzania nzima, nimeona ndani ya ccm hakuna demokrasia, nimejiunga na CHADEMA ili niwe moja wa watakaohakikisha kuiondoa ccm madarakani
 
Hivi Sioi bado alikuwa CCM? Masha alishinda kura za maoni kule Sengerema kweli?
 

kwahiyo wewe ulitaka ukusanyike umati wa " panya " kisha
ndipo uamini ya kwamba magamba wanakwenda kung'olewa meno bila ganzi ??
kura ni watu na watu wenyewe ndio sisi....sasa wewe jifariji tu kisha
uje kuanza kuangua kilio kama cha paka jizi baada ya oct 25,mwaka 2015.
 
Masha ni hasara. Ila ndo hivyo tena.

Atafata Karamagi kesho Mwanza, then Rostamu kisha Manji afu mchezo unamalizwa na JK kumchinjia baharini makomeo....

Jamaa wamejipanga kurudi kupitia mlango wa Chadema. Aibu!!

Hizo zinaitwa conspiracy mkuu, mothing is true..! JK na Edo hawaivi tena...
 
Subiri kampeni zianze.....!! UKAWA mmetangulia na baskeli ya mti......

Haya maneno ulipaswa kuwaambia CCM wakati mgombea wao anazunguka mikoani "kujitambulisha" mbwembwe zilikuwa nyingiii mkadhani mchezo umekwisha.UKAWA wanajibu mmeanza kuomba po!
 
Laurence Masha anakabidhiwa kadi na Mbowe
Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara
Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha
Sioi Sumari
Mafuriko ya arusha yamewazoa na kuwatakatisha.
Karibu sana cdm, hata hivyo chadema mna kazi pia ya kuchukua tahadhari ya kutambua na kuchuja mavumbi na papasi watakaoingia ndani wakati mnapofungua madisha ili kuruhusu hewa safi kuingia ndani. tayarisheni nyavu zenu za madirisha, vitambaa vya kufutia vumbi na dawa za kuulia wadudu mapema. Sio wote watakaomwita bwana bwana watauona ufalme wa mbinguni.
 
kwa hiyo breaking news! CCM Kwisha ndembendembe.
 
Subiri kampeni zianze.....!! UKAWA mmetangulia na baskeli ya mti......
Baiskeli yenye magurudumu ya barafu, jua likiwaka magurudumu yanayeyuka na safari inakuwa na mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…