Libya
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 790
- 1,968
Wasalaam
Jamani leo mvua imeanza asubuhi sana na bado inanyesha kama yote wakati huu.
Tunaokuja na mwendokasi mjini panapitika Jangwani au ndio imetoka tukutane kesho?
======
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya mrejeo kuhusu uwepo wa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinaendelea kusambaa katika maeneo ya Pwani ya kaskazini pamoja na kanda kati.
Hivyo, tahadhari ya kuendelea kwa vipindi vya mvua kubwa inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Hali hiyo imetokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea katika maeneo hayo kutokana na mwenendo wa mkondo baridi katika eneo la kusini mwa Afrika. Hali hiyo ya vipindi vya mvua kubwa inatarajiwa kuendelea hadi alasiri ya leo tarehe 17 Disemba, 2019.
Aidha, Angalizo lililotolewa la vipindi vya mvua kubwa zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa), Mikoa wa Ruvuma, Lindi, Mtwara pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro liendelee kuzingatiwa.
USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua.
UPDATES:
Hali ya barabara siku ya Leo sio shwari:
1. Jangwani kutokea Fire - Magomeni na Magomeni - Fire barabara imefungwa
2. Jangwani kwa nyuma kutokea Kariakoo - Kigogo imejaa Maji
3. Umoja wa mataifa, kutokea Almuntazir mpaka Muhimbili Primary kumajaa Maji
4. Scout - Upanga barabara ya Malik pamejaa maji kuja junction ya Muhimbili
5. Barabara ya Fire hapa ktk hospital ya Regency pamejaa Maji
6. Kamata ktk barabara ya Byerere ktk Flyover ya Treni pamejaa Maji
7. Kamata kutokea kariakoo kuja barabara ya Nyerere pamejaa Maji
8. Waterfront kuelekea Central Police pamejaa Maji
9. Barabara ya Mwamunyange kuja Main road ya barabara ya White Sands pamejaa Maji
10. Barabara ya Afrikana - White Sands kuja round about ya White Sands/Mbezi beach ya chini hali si shwari
11. Basihaya kuelekea Nyaishozi hali sio nzuri
12. Mbozi road Chang'ombe pana Maji ya kutosha
13. Makutano ya kwa Sokota napo pamejaa Maji
14. Sinza Legho darajani hapa pamejaa maji pia
Hapa ni hali ilivyo katika mtaa wa Sinza Kumekucha. Mitaro ya maji imeziba
\

TAARIFA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA)