Updates: Mazishi ya Mama na safari yangu


Mungu akupe faraja
 
Wala sio utabiri, ni kitu kilikua wazi akienda ni lazima arudi, kikubwa wameumbuka wote waliomtilia mashaka na kumdhihaki, atachangiwa tena na kurudi kwenye mapambano yake this time atapata na ajira ya kudumu
ubarikiwe mkuu kwa ujumbe huu, ule uzi dhihaka zilikuwa za kuogofya, nakumbuka nilipofiwa na bi mkubwa kuna dogo nilishawai kumshika mkono alinitumia 300k tzs, sikumwambia hata nimefiwa ila aliambiwa na dogo mwingne, tusaidie watu kama tuna kauwezo ka kusaidia, mengne tuiachie nature itaamua.
 
Hiyo ticket ya AI ina makosa mengi.Sitaki kuongea mengi nimeshaonekana mwenye chuki na wivu..shortly
something smells fishy,amekaa wiki yote aki'compile ticket na picha ya kuokoteza.
Najua haupo bukoba ila tufanye upo bukoba msibani..

Mwisho wa siku tunarudi palepale anataka tena achangiwe pesa ya matumizi akiwa uko pamoja na nauli ya kurudia.as if jamii forum ni baba yake mzazi.
Mtumieni tena nauli ya kurudia ndugu yenu.
Pambana mdogo wangu,una familia ya watoto 4, hapo upo ugenini huna pesa,umeshajiuliza uko dar familia yako inaishi vipi?
Utaishi kwa donation mpaka lini?
 
Wala sio utabiri, ni kitu kilikua wazi akienda ni lazima arudi, kikubwa wameumbuka wote waliomtilia mashaka na kumdhihaki, atachangiwa tena na kurudi kwenye mapambano yake this time atapata na ajira ya kudumu
ubarikiwe mkuu kwa ujumbe huu, ule uzi dhihaka zilikuwa za kuogofya, nakumbuka nilipofiwa na bi mkubwa kuna dogo nilishawai kumshika mkono alinitumia 300k tzs, sikumwambia hata nimefiwa ila aliambiwa na dogo mwingne, tusaidie watu kama tuna kauwezo ka kusaidia, mengne tuiachie nature itaamua.
 
Mburaaaaaaaa ndrrrrrrooooo hivyo babanguuuu
 
Mkuuu kama unataka kuthibitisha ticket njia rahisi ipo... hiyo tiket si ya busbora chukua PRN kajaze kule upate detail za tikeck mbona simpe sana
 
Una kazi ya uhakika umpatie?
 
Pole sana kwa msiba ila hii ni man to man talk acha tabia ya kuomba omba mtoto wa kiume ulioata nauli ya kufika huko inatosha pambana na ww sasa huko si home ... Mwanaume inatakiwa ujue kukaza na kupambana
Nakazia

Yani yupo uwanja wa nyumbani bado anaomba omba huku mjini atatoboa kweli huyu

Kama hana nauli ya kurudi ni bora abaki huko huko
 
Wote wanao mkritisaizi dogo humu ndani ni walala hoi,mafukara wa kutupa,Masikini wasioeleweka,wana matatizo makubwa na lukuki kuzidi hata huyo dogo,Makabwera ambao hata kula yao ni mashaka na kudunduliza mnoo!

Wanakwesheni dogo wengi wao humu ni watu ambao wamepanga kachumba kamoja ambamo humo ndani kajaza vyombo kwenye mabeseni kayaficha chini ya uvungu wa kitanda,ndani humo unakuta kameza ka kuwekea mtungi wa gesi,ndani humo unakuta nyumba imeumuka kwa fangasi,ndani humo unakuta kuna ka friji ambako hakawashwagi mpaka kuwe na tumatunda twa uwongo na ukweli pamoja na juisi ya kubabatiza kwa siku moja baada ya miezi 5.Tundoo twa maji unakuta kaviweka humo humo ndani au nje ya mlango ambako kandoo ka maji ya kunywa ndo kamebaki ndani!,kodi kuanzia Elfu 40 na haizidi Elfu 80 (40 - 80)

Ukiwa na maisha ya namna hiyo acha kabisa kumcheka dogo,Maisha ya Dar es salaam wote anaoishi Dar es salaam wanayajua yalivyo magumu!,yawezekana kwako wewe maisha yakawa mepesi kwakuwa unaishi kwa Kaka yako,Dada yako,Shemeji yako,Shangazi yako,Mjomba wako,Baba yako mkubwa au kwa Baba yako mdogo,ambao wao wanaenda kutafuta na kukuletea wewe unakula tu bila kuona maumivu wanayopitia!

Kuna watu humu ndani wanaomba usiku na mchana matatizo hasa misiba isitokee huko kwao kwasababu wanajua kabisa hawana kitu,ni Hoe Hae wa kutupa!

Ubaya wa Msiba huwa hauna taarifa,ni tofauti kabisa na sherehe,Kwenye sherehe mnakaa chini mnapanga Tarehe na siku ya kuifanya hiyo sherehe,Lakini Msiba unakuja ghafla bin Vuu!,Na msiba huwa ni kama una kumezea mate wakati ambao unajua kabisa uko Apeche alolo ndo wenyewe huja ghafla!

Kuna watu humu ndani wana uwezo mzuri tu wa kimaisha,lakini msiba unapotekea ghafla wao pia huingia kwenye madeni kwasababu unakuta huko mikoani/Vijijini kwao,wao ndiyo tegemezi na unakuta msiba wakati unatokea huwa hawana hela,Hivyo hulazimika kukopa kwa Jamaa na marafiki ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa msibani!

Sasa kwenye situesheni kama hiyo ya ghafla na wewe huna kitu,utafanyaje zaidi ya kuomba msaada?

Hivyo nadhani tuache kumkejeli huyo dogo,masuala ya msiba sote tunayafahamu,Ukiweza kumchangia dogo wewe mchangie tu,Usianze kukebehi na kuuliza uliza mambo ya kijinga!,Una hela mchangie na kama huna hela piga kimya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…