Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Nimepokea simu kuwa Waziri mtarajiwa wa Nishati na Madini, ndg yetu mpendwa Prof. Sospter Mhongo kashinda Musoma Vijijini (Butiama) japo sija ambiwa idadi ya kura.
 
Jama kama kuna mtu ana habari za igunga naomba zirushe hapa
 
Wakati vyama vikiwa kwenye mchakato wa kuwachagua watia nia wao ili kuwasimamisha kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo ya chaguzi, chama cha Mapinduzi kipo katika hali mbaya zaidi. CCM ni chama kikongwe zaidi Tanzania ambacho historia yake inaanzia tangu Tanganyika African Association (1929) kisha Tanganyika African National Union (1954) na baadae chama cha Mapinduzi baada ya kuungana TANU na Afro-Shiraz Party 1977. Licha ya kuwa chama kikongwe, CCM haina jipya la kujivunia katika kuwaletea watanzania maendeleo.

Hii imepelekea watanzania wengi hasa wanaojitambua kuamua kutafuta vyama vingine kuviunga mkono ili vichukue dora na kuwaletea watanzania maendeleo yanayoendana na karne ya 21. Katika hili, ndipo Waziri mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, Mzee wamatumaini alipoamua kuungana na CHADEMA katika mbio za kuchukua dora tarehe 25/10/2015.

Hali hii ya kuhama kwa Lawassa imepandisha homa ya uchaguzi kwa upande wa CCM baada ya kugundulika kuwa Lowassa amewaacha baadhi ya wana-CCM kuendelea kufanya kazi ndani ya chama kwa maslai ya upinzani (Lowassa). Wenyeviti na Makatibu wa kata wa CCM wanaofanya kazi kwa maslai ya Lowassa waliweka utaratibu wa kupiga kura za kuwachagua wagombea Ubunge na Udiwani. Utaratibu huu uliangalia zaidi majina yaliomdhamini Lowassa wakati anatafuta wadhamini CCM kugombea Urais ndiyo yalipewa kipaumbele kupiga kura kuchagua mgombea Ubunge na Udiwani ambaye tayari walishamuanda. Kitendo hiki kimepelekea kuchaguliwa wagombea Ubunge na Udiwani ambao hawakubaliki kwa wanainch ili washindwe na wapinzani (Team Lowassa & UKAWA) washinde kiurahisi uchaguzi. Hii imesababisha hata mmoja kati ya wagombea Udiwani kutoruhusiwa kuingia kupiga kura kwasababu jina lake halipo kwenye daftari.

Pia, wana-CCM wanadhihilisha kukumbwa na homa kali ya uchaguzi kwa kutumia mda wao mwingi kumjadili Lowassa (upinzani) badala ya kumjadili Magufuli (CCM)

Naomba kuwasilisha!
 

anajisumbua....
 

Wengine wanazitiki kabla hazijapigwa, mmeyasikia ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini?
 

Wewe hujui strategy ya EL na Ukawa. EL anataka Ukawa iwe na Wabunge wake wengi kutoka upande wa pili. EL ana akili sana!
 
kwani huyu anatafuta nini CCM, baba yake alipotezea yeye yupo bado?
 
Tuliwaambia hawa watoto wetu wasiojua siasa zinavyofanywa lakini hawakutaka kutuelewa wazee wao.

Mtoto nani? Hizi ID fake hizi unaweza jikuta unamuita baba yako mtoto, Kuwa makini dogo
 
Jamani kuna mtu anaitwa asumpta mshama ccm wssipomkata ukawa tunakuja kumfyeka kwa aibu
 
matokeo kata ya Sejeli Jobu Ndugai kapita aisee kapta kura 807 na palingo 434
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…