Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Uyu bibi si ndo wa ajira! Afadhali maana recruitment agencies zinawanyonya watoto wa maskini na anajua bt anazipotezea pia mfumo wa ajira serekalini ni mbovu sasa sijui amesimamiaga nn!! Ata ukawa hatumtaki.
 
amegombea ubungo makusudi ili amalizie dili lake la kuuza kituo cha mabasi ya mikoani , lakini baada ya sisi kushtuka tumemuweka kubenea , masaburi atafute kazi , kwa kubenea hatoki .

We subiri uone kitakachomkuta Said kubenea. Yule ndo masaburi aliyewaambia wabunge wa dar es slaam wanatumia makalio kufikilia
 
hebu tusaidiane..
Baada ya zoezi la uandikishaji nani anatunza mashine za BVR nani anahakikisha kuwa hazitumiwi kutengeneza kadi mpya kwa wapiga kura wasiofahamika?!

Hakuna wa kuzuia bao la mkono
 
Usiogope UKAWA ni mpango wa mungu, hivyo hakuna goli la mkono wala kisigino
 
Hilo nalo neon,ila sioni wakifanya hivyo, we need to keep the spirit
 
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, na Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Nyambari Nyangwine, wamebwagwa katika kura za maoni (CCM) katika Jimbo la Tarime mjini na Tarime Vijijini katika nafasi ya Ubunge.

Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Tarime, Mathias Lugora, ametangaza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Christopher Rioba, ameibuka mshindi kwa kupata kura 15,928 akifuatiwa na John aliyepata kura 12,205.

Katika Jimbo la Tarime Mjini, Maiko Kimbaki, amembwaga Waziri wa Kazi na Ajira, (Gaudensi), kwa kupata kura elfu 3908 dhidi ya kura 2411 alizopata Waziri Kabaka.

Uchaguzi katika Jimbo la Tarime mjini na Tarime Vijijini uliahirishwa juzi kutokana na kupatikana kwa kura zilizokuwa zimewekwa alama ya tiki kwa baadhi ya majina ya wagombea kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza.




Naomba Kujua Mtoto Wa Aliyekuwa Gavana Wa Benki Kuu Hayati Mzee Nyirabu Anaitwa Masero Nyirabu AMEPITA au Na Yeye Ni Bila Bila?
 
Nipo ofisi za C.C.M wilaya, kulikuwa na vijana wengi hapa ofisi ya c.c.m wilaya wakilaani mbunge wao Aeshi Hilary kukatwa. Na hakuna kiongozi yeyote wa c.cm alothibitisha kama ni kweli ama laa. Kama kuna mtu anaweza tuthibitishia tafadhali.
 
​Kwani mwenye mamlaka ya kukata jina lake ni hapo ofisi za Mkoa au Kamati kuu???
 
Back
Top Bottom