Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Simbachawene: Sijawahi kuona mchakato wa uchaguzi CCM kama wa mwaka huu.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
"Baadhi ya wagombea walifanya kampeni kama vile ni wanachama wa vyama vya upinzani," alisema Simbachawene.
Simbachawene ambaye hata hivyo aliyetangazwa kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho alijizolea kura 18,158.
Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba.
Jumla ya makada wanane wa CCM waliwania nafasi hiyo katika jimbo hilo huku aliyemfuatia Simbachawene akiwa ni Gabriel Mwikola, aliyepata kura 6,901.
Simbachawene alisema inaelekea mfumo wa wanaogombea uongozi kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa, sasa umepitwa na wakati.
Alisema Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, inaelekeza mtu anayetaka uongozi kwa kupigiwa kura na wananchi, awe mwanachama wa chama cha siasa, sharti ambalo hata hivyo, alisema limeanza kupoteza umuhimu wake ndani ya jamii ya Kitanzania.
Alisema ni bora Katiba inayopendekezwa ambayo ina kipengele kinachoruhusu mgombea binafsi ipitishwe ili wananchi wapate fursa ya kupima ubora wa aina mbili za viongozi; wanaotokana na vyama vya siasa na wale wanaojidhamini wenyewe.
CHANZO: NIPASHE_7th August 2015
Aje chadema tuimarishe vikosi. Milango bado iko wazi.Naperuzi habari za kura za maoni CCM na kusoma kuwa Mbunge wa Tabora Mjini,Ismail Aden Rage ameangushwa kwenye jimbo hilo. Habari za Rage zimenikumbusha bastola yake aliyopanda nayo jukwaani kupiga kampeni.
Ilikuwa ni kule Igunga kwenye uchaguzi mdogo akimnadi Dr. Kafumu. Rage alipanda jukwaani na bastola yake kiunoni. Wapigakura wa Igunga wakaiona na kuiogopa na hata kumpigia kura Dr. Dalali Kafumu aliyemshinda Mwalimu Kashindye wa CHADEMA.
Je,wana wa Tabora Mjini wameiogopa bastola ya Rage na kuamua kujitenga naye?
ukatili wake umeongezea kung'okaRage ni mbunge mjinga kuliko wote waliowahi kutokea kwenye bunge la Tanzania..Anashadadia mavitu asiyoyajua anajipanuapanua tu wakati wa kuchangia miswada hata kama haina maana..
inasemekana dharau , kiburi , nyodo na kulewa madaraka ndio vimemponza adam malima .Baadhi ya wabunge na mawaziri maarufu Walioangushwa hawa hapa:
Peter Msola
Mathias Chikawe
Adam Malima
Pindi Chana
Dr. Titus Kamani
Lediana Mg'ong'o
Said Arfiy
Asumpta Mshama
Pereira Silima
Amos Makala
Terezya Huviza
Said Nkumba
Hasani Ngwilizi
Beatrice Shelukindo
Henry Shekifu
Hebert Mntangi