Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, na Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Nyambari Nyangwine, wamebwagwa katika kura za maoni (CCM) katika Jimbo la Tarime mjini na Tarime Vijijini katika nafasi ya Ubunge.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Tarime, Mathias Lugora, ametangaza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Christopher Rioba, ameibuka mshindi kwa kupata kura 15,928 akifuatiwa na John aliyepata kura 12,205.
Katika Jimbo la Tarime Mjini, Maiko Kimbaki, amembwaga Waziri wa Kazi na Ajira, (Gaudensi), kwa kupata kura elfu 3908 dhidi ya kura 2411 alizopata Waziri Kabaka.
Uchaguzi katika Jimbo la Tarime mjini na Tarime Vijijini uliahirishwa juzi kutokana na kupatikana kwa kura zilizokuwa zimewekwa alama ya tiki kwa baadhi ya majina ya wagombea kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza.