Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Hili ndilo kosa lililofanyika katika uongozi wa awamu ya nne. Ni kuufanya uwakilishi kuwa rahis kiasi kwamba kila mmoja kujiona anafaa kuwa mwakilishi. Bunge ni sehemu ya kutunga sheria. Unapaswa kusoma miswada na kuielewa, kujenga hoja na kuitetea, kupangua hoja kwa hoja! Jamani!!!!! Hatakiwi mtu wa kwenda kusema NDIOOO! Huo sio uwakilishi!!!
 
Ushetu
Elias Kuandikwa alishinda jimbo hilo jipya, Charles Shigino, alijitoa na kukimbilia Chadema
, baada ya kuona mchakato ndani ya chama hicho kughubikwa na sintotahamu kwa kutuhumiana baadhi yao kutoa rushwa kwa wanachana wa chama hicho.
Elius Kuandikwa (11,550), Isaya Bukakiye (5241) na Elias Mlyasi kura (207).

Kariku Charles Shigino kwenye UKAWA
 
Wakubwa, mwenye matokeo ya kuomba kuwania ubunge kupitia CCM jimbo la Monduli, naomba atupashe.
 
Ni kweli Petro Mselekwa. Na mimi hilo nimeliona ndio dalili za bao la mkono kwamba ccm wameanza kuchapisha kadi fomu za wapiga kura feki.na bvr zingine ziliripotiwa zinaandikishwa majumbani mwa watu. Chadema badala ya kudhibiti hiyo hali wanalumbana.
 
Leo ni August 1,2015 Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima wanakusanyika katika maeneo ya matawi yao kuchagua mgombea mmoja atakayeshindana na wagombea wengine kutoka vyama tofauti na CCM.

Mchakato wa kampeini katika mkoa huu zimetawaliwa na vituko,udhalilishaji kwa baadhi wa wagombea hivyo hata upigaji kura za maoni utakuwa hivo hivyo,hii ndiyo sababu inatufanya tufuatilie live kura hizi.

Updates...






MORE UPDATES:

kondoa vijijini alieshinda ni Ashatu kijaji sio Hasan lubuva ....pia kondoa mjini huyo mbunge alie kua anatetea jimbo hilo amepigwa chini na alieshindi ni Edwin Sanda .


source : wenyeji wa kondoa
 
hebu toa ujinga wako hapa.
Hapa tupo jukwaa la siasa halafu ww unaleta habar mmu!

Ww kama unaniota endelea kuniota ntakutengeneza ipasavyo.
Jitu huna hata aibu nilikuwa sijibizan na ww lakn ww kwa kiherehere chako unaamua kunivamia.

Lakn utambue hicho kiherehere kitakupelekea mimba.

Unaona taarabu hizo ulizoandika hapo juu, mtoto mchelemchele.
 
ccm (chama cha majangili ) waliokubuhu kwa mabaya
 
Na mwandishi wetu.
Kura za maoni za ndani ya CCM zimeisha na maeneo mengi matokeo yake yakiwa yamegubikwa na sintofahamu baada ya matokeo hayo kugomewa na wagombea.
Hili limetokea katika wilaya ya Lushoto ambayo ina majimbo matatu, Mlalo, Lushoto na Bumbuli baada ya matokeo kwenye majimbo yote hayo kuwekewa pingamizi. Katika jimbo la Mlalo mbunge wa siju nyingi Mh Ngwilizi ameshindwa na kijana mpya kwenye siasa za mlalo bwana Rashidi Shangazi ambaye analalamikiwa kuanza kampeni kabla ya muda, wakati jimbo la Lushoto Mh Shekifu akiwa ameshindwa na kada wa chama Bwana Bosinia Shekilindi naye anayelalamikiwa kuwa amebebwa na katibu wa chama wilaya na kuwa alianza kampeni muda mrefu.
Jimbo la Bumbuli ndio limegubikwa zaidi na malalamiko baada ya mgombea Ubunge aliyeshindwa Bwana Abdul Kaniki kuweka pingamizi kwa chama dhidi ya mshindi na mpinzani wake Mh January Makamba baada ya kuwa uchaguzi huo ulijaa hujuma.
Baadhi ya malalamiko yaliyotolea na Bwana Kaniki ambayo yameshafikishwa kwenye chama ni pamoja na mawakala wake siku ya uchaguzi kuamuliwa kutoka katika vituo vya kupigia kura kwa agizo la katibu wa wilaya, makatibu wa kata na matawi walitakiwa kutoruhusu mawakala wote wa kaniki kuingingia kwenye vituo bila barua ya katibu wa wilaya na katibu huyo akiwa hakumpatia barua hiyo bwana Kaniki mpaka ilipofika saa 6 mchana siku ya uchaguzi, hili limechukuliwa kama hujuma kwani kwa wakati wote huo lolote lingeweza kuwa limefanyika, kwahiyo zoezi la kupiga kura likiendelea mpaka mwisho bila mawakala wa bwana Kaniki, pamoja na ushauri wa viongozi wa chama wilaya akiwemo mjumbe wa halmashauri kuu Taifa, mkuu wa wilaya na baadhi ya wajumbe wa kamayi ya siasa ya wilaya kushauri uchaguzi huo haukuwa wa haki tena na kushauri uahirishwe lakini katibu wa wilaya alipingana na maamuzi hayo na kuamuru barua hiyo ipelekwe kwenye vituo na mawakala wa bwana kaniki waruhusiwe kuingia kusimamia kura za mgombea wao, zoezi hilo lilipingwa kutokana na jiografia ya jimbo hilo kuwa ngumu kufika vituo vyote.
Lingine linaloonekana kuchukuliwa kama hujuma na kutokutumika kwa jina Bwana Kaniki ambalo limezoewa na wapiga kura wengi na kuvumishwa kwamba kaniki amejitoa kwenye uchaguzi huo, hiki lilichanganya wapiga kura wengi na wengi waliamua kutoshiriki kupiga kura walipojulishwa bwana kaniki amejitoa.
Akiongelea suala hilo Bwana Kaniki amesema yeye baada ya hayo yote kutokea aliamua kutoa taarifa kwa chama wilaya na mkoa na kuamua kutoendelea na uchaguzi huo,"niliamua kujitoa na kuandika pingamizi lakini wenzangu waliendelea na zoezi lao wakajipangia matokeo na kujipa ushindi ambao hakuna wakala wangu au mimi mwenyewe kusaini matokeo hayo", aliendelea kusema"dalili za hujuma zilianza mapema lakini niliamini mwisho wananchi watapewa fursa ya kuchagua, lakini hata hilo halikutokea"
Bwana Kaniki anasema wakati wa kampeni zikiendelea viongozi wa wilaya walikuwa wakipita kwenye jimbo kukutana na viongozi wa chama na wanachama kuwaambia wamepewa agizo kwamba lazima Mh January ashinde kwa namna yoyote, na kumchafua bwana Kaniki ili asichaguliwe.
Baadhi ya viongozi wa chama jimboni Bumbuli walithibitisha kuwa kulikuwa na maagizo hayo na siku ya mwisho walipewa semina maalum ya kuhakikisha Mh January anashinda.
Nae katibubwa wilaya Bwana Ramadhani Mahanyu alipoulizwa kuhusu sakata la uchaguzi jimbo la Bumbuli, alikuro kupokea pingamizi kutoka kwa bwana Kaniki kama mgombea lakini akasema taratibu za chama zitafuata kusikiliza malalamiko hayo kwani mpaka sasa chama hakijatangaza mshindi katika majimbo yote kwani kuna mapingamizi kila katika jimbo, alipoulizwa kuhusu tuhuma za kupigia debe baadhi ya wagombea alisema yeye kama kiongozi asingeweza kufanya hivyo, japo zipo dalili za wazi kwani hata baadhi ya viongozi wenzake katika ofisi ya chama wilaya ya lushoto wameonekana kutoafikiana na matendo ya upendeleo na hujuma anazofanya katiba wa wilaya.
Uchunguzi uliofanya na chanzo chetu unasema katibu wa wilaya ni "kibaraka" wa Mh January Makamba kwani mwaka 2010 ndio huyo alikuwa kampeni meneja wa bwana January Makamba na alipofanikisha ushindi wa January Makamba mwaka 2010 aliteuliwa na aliyekuwa katibu wa CCM Taifa Mzee Makamba kuwa katibu wa wilaya kama zawadi na malipo ya kunsaidia Mh January kupita, wanaomjua wanasema katibu wa wilaya kaletwa lushoto kufanya kazi ya Mh January tu na yeye amesikika akisema kwake January kwanza na chama Badae.
Chakushangaza ni kwanba hata katibu huyo alikuwa akijua kwamba Mh January alikuwa na wakati mgumu wa kuchaguliwa tena jimboni Bumbuli na alifanya jitihada za kumshawishi bwana Kaniki asigombee akiwa na viongozi wengine wa wilaya ili Mh January apite bila kupingwa lakini ilishindikana na ndipo ukawekwa mkakati wa " bao la mkono".
Wengi wanashangazwa na kura anazoonekana kupya Mh January kwani kuna baadhi ya vituo vina idadi chache ya wapiga kura kuliko kura zinazosemwa amepata.
Akiongea na waandishi wa habari Mh January amesema amepata ushindi huo kwakuwa anakubalika sana na amewafanyia mambo mengi wananchi wa Bumbuli.
Mpaka leo bado utata wa matokeo hayo haujaamuliwa japo kumekuwa na uvumi kwamba huenda ukarudiwa kwani hujuma zimeonekana wazi japo kutokana na muda uliopo suala la kurudia uchaguzi limeonekana kuwa gumu na litategemea uamuzi wa vikao vitakavyoamua.
Kwa sasa katibu wa wilaya na Mh January wamekuwa na jitihada za kutaka kufanya muafaka na Bwana Kaniki ili kunusulu hali iliyopo kwani kuna uvumi kwamba bwana Kaniki huenda akatimkia Upinzani na hali hiyo itakuwa ngumu kwa CCM kwani ni jambo linaloonekana wazi kwamba Kaniki akienda upinzani Mh January atakuwa na wakati mgumu kutetea jimbo hilo. Nipashe#bumbuli
 
Last edited by a moderator:
Huyo Kaniki ni mpuuzi...
Mawakala wake wanazuiwa yet yeye anaruhusu upigaji kura kuendelea!
 
Hili ndilo kosa lililofanyika katika uongozi wa awamu ya nne. Ni kuufanya uwakilishi kuwa rahis kiasi kwamba kila mmoja kujiona anafaa kuwa mwakilishi. Bunge ni sehemu ya kutunga sheria. Unapaswa kusoma miswada na kuielewa, kujenga hoja na kuitetea, kupangua hoja kwa hoja! Jamani!!!!! Hatakiwi mtu wa kwenda kusema NDIOOO! Huo sio uwakilishi!!!

Kama kaona fursa kwanini asichangamkie! we unaejua kupangua hoja kwanin usingeenda kuchukua hyo nafasi yake?
 
kuna raia wanataman asipite lakin ndiyo hvyo tena

IRENE_UWOYA991.JPG
 
Wanabodi nawasalimu sana.

John d Pallangyo kapitishwa na chama cha mapinduzi kwa idadi ya kura nyingi huku akifuatiwa na wagombea wengine Wa Ccm kama Mh. Siyoi Sumari , William Sarakikya, kamanda huyu Wa vijana ndio ataipeperusha bendera ya Ccm kumngoa mbunge Wa sasa anayemalizia kipindi chake cha ubunge Dogo Joshua Nasary.

Mosi John D Pallangyo amekuwa zaidi mtendaji(performer) kuliko mwanasiasa(politician) na hicho ndicho watanzania tunakihitaji kwa miaka hii , cha msingi niwapongeze sana wagombea wote Wa meru kama.

1: Dr. Daniel Pallangyo (mchumi)
2: William Sarakikya
3: Angela
4:Mh. Siyoi Sumari.
5: elirehema Kaaya.

Mathali hofu kubwa ni kuhama kwa Lowasa kwenda chadema imeleta upepo Wa Nasary ubadilike sana na kuleta hofu kwetu Ccm.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom