Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Huu mwaka watu watauelewa tu. Yani mpaka huyu bwana mdogo mwenye maneno mengi ameshindwa kuwadanganya wananchi kwa mara nyingine?

Ama kweli asemaye mwaka kesho muongo.
 
Angeshinda angesemaje maana akiwa naibu waziri thamani ya fedha ikiporomoka uwezo wa kununua unapungua alikuwa anachukulia poa
 
Huu mwaka watu watauelewa tu. Yani mpaka huyu bwana mdogo mwenye maneno mengi ameshindwa kuwadanganya wananchi kwa mara nyingine?

Ama kweli asemaye mwaka kesho muongo.
Huyu bwana alisha wahi kuwaambia wapiga kura wake wa kijiji cha VIANZI, kuwa mi hii cheni yangu ya shingoni nikiiuza mnakula miezi 3!!!,na hata msiponichagua lazima nitapita tu!!!
 
figganigga

Hivi kila anayeshindwa CCM anasema uchaguzi haukuwa wa haki dah!hatari poor Tanzanian
 
Last edited by a moderator:
hahahaaaaa...
si the green wenzake hao..
hawafaiiiii..
 
Habari za uhakika ni kuwa yeye Malima alikuwa anahonga wapiga kura kwa dau la 80,000/, yaani ukionyesha kadi ya ccm unalamba misimbazi minane. Hela inamuuma ndio maana analalama.
 
Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima , amesema kuwa kura za maoni zilizopigwa jimboni humo hazikuwa huru na haki kwa madai kwamba waliopiga kura walikuwa wachache lakini kura za matokeo zikawa nyingi. Amekuwa nafasi ya pili kwa kupata kura 8, 212 na mshindi wa kwanza kapata kura 16, 294

“Mchakato uligubikwa na udanganyifu mkubwa, kura haziendani na uhalisia, pia mawakala hawakutia saini baada ya kumalizwa kwa upigaji kura katika vituo vyao, lakini ninaviachia vikao vya maamuzi vifanye kazi yake,” alisema Malima.

Chanzo: IPP Media

Tumsaidie nini siye ???
 
Yeye badala ya kuwatumikia wananchi alikuwa anatembea na mabunduki tu na kuwatumikia machangudoa! alitegemea nini?

Amevuna alichopanda!

Tangu awe mbunge hajatatua tatizo hata moja kati ya matatizo mengi yanayosibu wana Mkuranga, mfano ni tatizo la maji!

Pia kilichomponza ni kauli zake chafu na kudharau wananchi. Nitatoa mifano michache:

1. Aliposhindwa kura za maoni na Mtembei mwaka 2010 hata hivyo akateuliwa kugombea ubunge kwa msaada wa Kikwete, alikuwa anawananga wana Mkuranga kwamba hawezi kutatua kero zao kwani hawakumchagua!

2. Mapema mwaka huu akiwa Kisiju baada ya wananchi wengi kususia mkutano wake, mbele ya wananchi wachache waliofika kumsikiliza alitoa kejeli akisema hawamtishi na hana shida. Akasema pia kiatu chake thamani yake inatosha ku-feed wananchi wa Kisiju!

3. Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita kwenye kitongoji (Kiguza) anachokaa Malima alishinda Patu wa CUF. Kwa hasira Malima alipiga marufuku wananchi kuendelea kuchota maji nyumbani kwake hadi leo hii. Pia alitishia kukata maji msikitini ambayo alifadhili.

Kukataliwa kubaya! Pamoja na kugawa hela wananchi wamekukataa, ulizovuna (pesa) zinakutosha!

Kikwete akurudishe kama alivyofanya 2010, aone kama jimbo haliendi UKAWA!

Wana Mkuranga wameamka jamani, hongereni sana!
 
Back
Top Bottom