Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Mwenyekiti wao aliiba kura 2010 kwa hiyo haya ni muendelezo wa wizi wa kura ambao ni utamaduni wa chama hiki
 
Habari za uhakika ni kuwa yeye Malima alikuwa anahonga wapiga kura kwa dau la 80,000/, yaani ukionyesha kadi ya ccm unalamba misimbazi minane. Hela inamuuma ndio maana analalama.

Maccm hawana thamani hiyo, kura huwa zinanunuliwa kati ya buku tatu mpaka buku kumi.

Maccm wa vijijini umpe wekundu wanane si anaweza kufa papo hapo kwa heart attack?
 
Kama kura za maoni zingechelewa kidogo CDM then hawa waliokula mkasi CCM wangeishia huko.

Ngoja tuone.
 
Tatizo la wabunge wa CCM wamelewa madaraka...

Wanawadharau wapiga kura wao; kama huyu Malima anashangaa nini sasa? Ina maana uchaguzi huwa unakuwa si huru na wa haki wanaposhindwa wao..

Haya bana asubiri kukumbukwa tu na wenzake...
 
Sasa majungu yake akapigie Facebook maana aliona bunge sehemu ya majungu na sio hoja
 
Habari za kuaminika, mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilolo Bw. Venance Mwamoto ameibuka kidedea katika kura ya maoni za CCM, jimbo hilo na hivyo kumwangusha Prof. Msola aliyekuwa anatetea jimbo hilo.

Matokeo ya uchaguzi huo ambao uligubikwa na mizengwe, rushwa na mvutano kwa upande wa miamba hiyo miwili yaliahirishwa kutolewa Jumapili baada ya CCM Wilaya kugundua uchakachuzi wa hali ya juu katika Kata tatu za Uhambingeto, Nyalumbu na Lugalo, hali iliyopelekea uchaguzi kurudiwa katika Kata hizo.

Matokeo haya na idadi ya kura walizopata ilikuwa kama ifuatavyo

  1. V.Mwamoto 11,200
  2. P.Msolla 10,014
  3. D.MBILINYI 2,674
  4. C.Mofuga 1,218
  5. T.Kikoti 1,067
  6. Y.Myenzi 786
  7. M.Luvinga 779
  8. A.Chusi 439
  9. A.Nyamoga 430
  10. T.Kihongosi 350
  11. F.Mkokwa 336
  12. A.Mkakatu 201
  13. L.Mbosa 177
  14. B.Mteleka 172
  15. I.Salufu 106
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Asema hatua ya mbunge Prof Msola kususa kusaini matokeo haisaidii kubadili matokeo ,pia makatibu waliovuruga mchakato kukiona.
 
Safi sana-Asanteni watu wana mapinduzi wa Kilolo,hana mchango wowote tena huyu nina hasira nae sana kwa kuja na mapendekezo ya kutunyima mikopo ya elimu ya juu kipindi akiwa waziri wa elimu.
 
Pamoja na kcheza rafu zote zile pale mwanzoni hatimaye mh gaudencia kabaka aliyekuwa anagombea jimbo la tarime mjini abwagwa vibaya pamoja na mh nyambari nyangwine aliyekuwa mbunge wa tarime naye kapigwa chali jimbo la tarime vijijini. Ama kweli ccm kwishneeeeee. Sasa njia nyeupe kwa ester matik (mjini) na john heche (vjjn)
 
hili ni kati ya majimbo masikini zaidi nchi hii , pamoja na kutoa kokoto zote zinazotengeneza barabara nchi hii lakini liko nyuma sana ! huyu mzee ameshindwa kwenda na kasi , apumzishwe jimbo likombolewe na UKAWA , HUYO mwamoto alipewa muda akauchezea .
 
Huyu re-profesa ailikuwa ana lazimisha mambo tu kama
makongoro mahanga...muda mwingine muwe mnasoma
alama za nyakati na ku "dance according to the tune"
 
Back
Top Bottom