tutajiudhi sana matatizo ya mpira wetu ni mengi, maandalizi ya vijana kuazia kule umitashumta, umiseta, timu b za vilabu vya ligi kuu na timu za kids zao zote ovyo. Tumechagua kuwekeza kwenye siasa kuliko kitu kingine chochote; bunge la katiba, kampeni, mikutano hivi vitu ndo vimetujaa vichwani kwetu. viongozi wa michezo wanaigeuza kama madaraja ya kuingilia kwenye siasa. Usishangae Malinzi nae akachukua fomu za ubunge kama wenzake kina Mkamia, Rage, Madega na wengineo.
Hatujali tena kuandaa wachezaji wachanga kwenye vilabu vyetu , tunahangaika na mafather wanaodanganya umri kina Haruna Moshi, Mgosi na wenzao.
Ligi yetu inayolisha Taifa Stars huko ndiko kina Simba, Yanga, Azam wanakoshindana kununua mechi. Wachezaji wanavimba vichwa kumbe ushindi umeshapatikana kabla ya mechi. Huko mikoani ndio balaa uzalendo ni wa kufa mtu kwenye viwanja vya timu zao.
Tutabadilisha makocha mpaka basi, kuna vingi vya kubadilisha. Hata tukijitoa mashindano ya kimataifa kwa miaka 20 haitasaidia kama matatizo ya mpira wetu hayatapata dawa . Tuanze na Viongozi wa soka.