Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Manslaughter hiyo kaua bila kukusudia ilikua ni kwenye harakati ya kujitetea sasa unampiga mtu makofi bila sababu kwanini? Vijana wanapambana na hali ngumu ya maisha + msongo wa mawazo na bado unaenda kumpiga bila sababu kwanini asijitetee.
 
Unakumbuka tukio la yule conrad ambrosia,alivyowatandika risasi wale
Walinzi ambrosia
Ilimgharimu sana aise....
Haya mahasira,ambayo hayana mbele wala nyuma hayafai
Mambo ya kijinga tu yanakugharimu uhai wako,sababu zenyewe hazina kichwa wala miguu
Huyo afande na jamaa wa bajaji wote
Wapuz tu

Ova
kama nakumbuka hii mkuu..ilikuaje?
 
Sema ukiwa na broo mjeda hauonewi kizembezembe. Kuna broo wa mshkaji wangu alikua mjeda akatuambia mitaa ya sinza na mwenge atakaetuzingua tumpelekee kesi siku moja kuna mabaunsa walituzingua pale meeda club(sasa hivi inaitwa kitambaa cheupe) tukamsanua broo akatimba unaambiwa aliwatembezea kichapo heavy, kuna siku nyingine jamaa alinipola simu mitaa ya sinza afrika sana pale vibaka wenzake wakamwambia oya unamjua broo ake uyo? Mrudishie tu dogo simu yake, jamaa akanirudishia simu yangu kweli.. Miaka iyo sinza na mwenge yote nazulula muda wowote hakuna muhuni anaenigusa.
Hilo lilikuwa jeshi la zamani siku hizi kidogo Heshima ya jeshi imerudi awapigi sana raia. Kutokana na Sheria kukazwa sana . Japo watu kama wakina marehemu Kanal Bado awajaisha...ilihali Kuna sisitizwa sana kutokutumia Sheria mkononi
 
Mkuu GENTAMYCINE ,habari hii uliyoileta, ni ya MASIKITISHO na ndeeeeeefuu! Lakini ulivyo isimulia vizuri, mpaka msomaji anajiona naye alikuwepo kwenye tukio. Pia, tukio hilo, kwa jinsi ulivyotujuza, tunapata elimu ya kujifunza, KUHESHIMIANA, bila kujali wewe ni nani!!
Asante sana Mkuu kwa Credits zako Kwangu ambazo nimezipokea kwa Mikono yote Miwili na umenipa Nguvu ya kuendelea Kuwajuza kwa mengine pale yakijitokeza.

Kwa huku Kunisifia Kwako jiandae Kuambiwa na Fools Critics wangu hapa JamiiForums kuwa hii ID yako ni yangu ( Mimi Mwenyewe ) na hapa nimejisifia tu ili kupata Umaarufu wakisahau kuwa GENTAMYCINE nilianza kuwa maarufu na mvuto kwa Watu tokea Mwenyezi Mungu alipoanza Kuniumba na ndiyo maana hata Kiasili akanifanya niwe "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" nilivyo.
 
Poleni kwa familia ya mwanajeshi pole kwa kato kwa maana hivyo ndivyo wanajeshi walivyo
Kuna safari moja nikiwa ktk duka langu maneneo flani kitu kilichokuwa kinaniboa watu wenye magari kuja kupaki gari mbele ya duka hili jambo nilikuwa kila siku napambana na watu sasa kuna siku akaja jamaa mmoja akapaki gari lake mbele ya duka langu kibaya hakufunga kioo nikamfata na kumwambia naomba ufunge kioo maaana unaweza ibiwa halafu ukatusumbua wakati sisi hapa tunafatuta hela hatutaki kupoteza muda kugombana na mtu hiyo nguvu naiwekeza kutafuta hela akajibu kwa nyodo eti niibiwe mtafunga maduka wote jeshi lote litaamia hapa
Tukaanza mzozo pale pale maana alikuwa anaongea maneno ya dharau na kukera kuna jamaa pembeni yangu ana duka akanifata akaniambia acha si unajua wanajeshi hao wasije kutupiga hapa akanitoa
Asikwambie mtu kwa dunia hii ya sasa hivi ukiwa na shida sana na huoni mwanga wa maisha yaan yamekupiga aisee una develop Traumatic Psychosis ambayo hautakuwa na chakuchofia wala kuogopa maana unaona hata ukifa sawa maana huna cha kupoteza
Sasa mm nakumbuka miaka hiyo ndio nilikuwa hivyo nipo nipo sina kazi ya maana kula shida kulala shida sina mbele yaan ilibaki tupigane basi pale dukani kulikuwa kuna kisu kikali nikajisemea akanigusa yaan namtoa utumbo njee
Toka siku hiyo yule mjeda alikuwa akija pale dukani akawa ananisalimia sana na akawa rafiki angu maana hakutegemea kukutana na mtu mbishi maana siku tulibishana sana kukosa wale wenye duka wenzangu zamani sana tulikuwa tushazichapa na mm nilikuwa nimejiandaa
Wanajeshi wanataka wabadilike wamezidi ubabe sana maisha yamebadilika vijana wengi hawana kazi hawana kipato cha uhakika hana pakulala pazuri hana uhakika wa kula pazuri na umri unaenda huyu anakuwa kadevelop Traumatic Psychosis ya maisha kwann yeye anakuwa yupo hivyo ukianzisha nae ugomvi kukuuwa ni rahisi
Alivyokuwa kato mm naelewa kwakuwa nilishawahi kupitia mseto mgumu wa maisha ilibaki kidogo nifanye kama kato kwa mjeda yule ila nashkuru hakunigusa hata kidogo ilikuwa maneno ambapo tulikuwa tunaelekea huko ila wauza duka wenzangu walinitoa fasta ndio ikawa salama ya yule mjeda
Pole sana mkuu kidogo tu ungeuwa boya.
 
Back
Top Bottom