Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Afande ( Luteni Kanali ) aliyeuawa jana Kawe Jirani na Baa maarufu ya Bombardier anaitwa Muna.

Marehemu ni Mkazi wa Mkoa wa Singida.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa kapandishwa Cheo na alikuwa anaenda kuwa Mkuu wa Kikosi Mkoani Arusha na leo Ijumaa ndiyo alikuwa anatakiwa Kuripoti tayari kukabidhiwa Majukumu.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna aliuliwa kwa Kuchomwa na Kisu cha Kukunja na Kijana aitwae Kato huku Mkewe na Mwanae wa Kiume wakiwa ndani ya Gari.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa ameenda Kubadili Tairi za Gari lake kwa Mfanyabiashara aitwae Chinga ambaye huwa Wanakunywa wote katika Baa yake ya Maifea Kawe ambayo ndiyo huwa anapenda Kunywa na hata wakati anachomwa Kisu hicho alikuwa amekunya kidogo ila anajitambua.

Afande Luteni Kanali Muna ndiyo alikuwa wa Kwanza kumkabili ( Kuzozana ) na Kijana ( Mchoma Kisu aitwae ) Kato baada ya Kuombwa asogeze Gari lake ili apite ndiyo Marehemu Afande Luteni Kanali Muna kwa Jeuri na Ubabe akamjibu Dogo ( Kato ) vibaya na kwenda Kumzaba Makofi mawili matatu.

Kijana aliyemchoma Kisu kilichopelekea Umauti Afande Luteni Kanali Muna aitwae Kato alikuwa anataka kuwahi Kawe mwisho Maringo ambako aliambiwa kuwa Mwizi wa Bajajj yake kaonekana na kwamba hata hicho Kisu alichokuwa nacho ( alichommaliza nacho Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ) kilikuwa ni cha kwenda Kukabiliana na huyo Mwizi wake ila Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alijiingiza tu mwenyewe katika 18 zake.

Mwili wa Marehemu Afande Luteni Kanali Muna umeagwa leo ( Mchana ) huu Hospitali ya Jeshi Lugalo na sasa uko safarini Kusafirishwa kwenda Kwao kwa Watani zangu Wanyiramba na Wanyaturu Mkoani Singida kwa Maziko rasmi Kesho.

Mchoma Kisu ( Muuaji Kato ) amekamatwa Jana akiwa njiani Kutoroka na Wanajeshi walitaka wapewe Wao, ila Jeshi la Polisi likawakatalia na Kumshikilia wao wakisema hiyo ni Kesi ya Kiraia na siyo ya Kijeshi kama ambavyo Wanajeshi walikuwa wanataka Kuilazimisha iwe hivyo.

Jana Wakazi wa Kawe ( hasa wa eneo husika ) walipokea Kipigo Kikali sana kutoka kwa Wanajeshi ( hasa MP ) kutokea Kambini Lugalo ambapo GENTAMYCINE nimekutana na baadhi ya akina Mama na Wahudumu wa Baa ya Bombardier Kawe wakiwa Wanachechemea, wanatia Huruma huku wakiwa wanatokea Hospitali za Ndahani, kwa Mambo na Shamba ( ya Serikali ) kupatiwa Matibabu kwani Jana walikuwa hawachaguliwi wa Kupigwa kwa Hasira na hakika Kipondo kilitembezwa na Wanajeshi ( MP )

Ahadi waliyoitoa Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ni kwamba Leo kuanzia Saa 10 Jioni wanarejea tena kwa Oparesheni yao Kabambe na kwamba leo watapita / wataingia nyunba kwa nyumba hata kama Unaukweka ( Unakunya ) utachomolewa Chooni uje upokee Kipigo utaje Wahuni unaowajua na ukimaliza huku ukiwa na Maumivu ya Kipigo chao unarejea Chooni kuendelea na Zoezi lako la Kunya ( Kuukweka )

Sifa zilizozoeleka za Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ni ya Ubabe wake wa Kiuanajeshi aliokuwa nao hasa kwa Raia, Kugambeka ( Kulewa ) mno Baa yake Kubwa ya Maifea Kawe ila akiwa anataka Totooz ( Udhaifu mkubwa aliokuwa nao ) alikuwa akipenda kuweka Kambi katika Baa ya Wauza Malaya ( Wachafu na Wasafi ) ya Igole iliyo Mita chache tu na Kituo cha Polisi Kawe ambacho baadhi yao hao Mihemko ya Kibaiolojia ikiwazidia huvuka tu barabara na kwenda Kuponea kwa hao hao Makahaba.

Inasemekana kilichowakera Wanajeshi wa Kawe ( hasa MP ) baada ya Boss wao Marehemu Afande Luteni Kanali Muna Kuuawa hivyo na Kijana Kato ni kwa Polisi kuwanyima / kukataa kuwapa Mtuhumiwa ili waende nae Jeshini Lugalo wakamuadabishe kwa Sheria zao.

Ni haya tu nimeona niwaletee mjue.
Naogopa hata kukomenti jamani
 
Kwa mwanaume anayejitambua hapo palikuwa siyo pakuonyesha ubabe,ukiwa na familia epuka shari huyo unayemletea shari anaweza kuwa yupo vizuri kuliko wewe ukaumbuka mbele yao.

Tuachane na kumuua tu-assume kwamba Bajaj driver Kato angekuwa yupo vizuri kwenye kurusha mkono akampasua hiyo familia yake ingemuonaje?mkewe wangepishana kauli siku amwambie mwanaume gani unajifanya una mafunzo ya kijeshi unapigwa na dereva Bajaj asiyejua hata kushika bastola?
Mambo mengine ukikutana nayo ni ya kuyapuuza tu unaachana nayo

Ova
 
Kwa mwanaume anayejitambua hapo palikuwa siyo pakuonyesha ubabe,ukiwa na familia epuka shari huyo unayemletea shari anaweza kuwa yupo vizuri kuliko wewe ukaumbuka mbele yao.

Tuachane na kumuua tu-assume kwamba Bajaj driver Kato angekuwa yupo vizuri kwenye kurusha mkono akampasua hiyo familia yake ingemuonaje?mkewe wangepishana kauli siku amwambie mwanaume gani unajifanya una mafunzo ya kijeshi unapigwa na dereva Bajaj asiyejua hata kushika bastola?
Umeongea vzr sana
 
Haya mambo ya kutunishiana misuli
Kutaka kuoneka nani zaidi huko uraiani,itakugharimu tu maisha yako
Mambo mengine ni kuachana nayo
Tu

Ova
Mie niliwahi poteza wana kwa ubabe wa kijinga jinga ,pale Ambrosia ,kawe ya chini
Pale Bar one ,enzi zile za kinje

Ukiwa na familia kuwa mpole kuwa mwanadiplomasia
 
Mie niliwahi poteza wana kwa ubabe wa kijinga jinga ,pale Ambrosia ,kawe ya chini
Pale Bar one ,enzi zile za kinje

Ukiwa na familia kuwa mpole kuwa mwanadiplomasia
Unakumbuka tukio la yule conrad ambrosia, alivyowatandika risasi wale
Walinzi ambrosia
Ilimgharimu sana aise....

Haya mahasira, ambayo hayana mbele wala nyuma hayafai
Mambo ya kijinga tu yanakugharimu uhai wako, sababu zenyewe hazina kichwa wala miguu
Huyo afande na jamaa wa bajaji wote.

Ova
 
Hivi wale wapiga debe wa kawe mkwamani na kawe tanganyika packers bado wapo ?
Wale ndiyo chanzo cha wizi wa kawe .
Vilevile kuna asilimia kubwa ya Bajaji na Bodaboda wanashirikiana na wezi au wao vilevile ni wezi .
Huyo dogo atakuwa anatumia bangi au ni mwizi
 
Hivi wale wapiga debe wa kawe mkwamani na kawe tanganyika packers bado wapo ?
Wale ndiyo chanzo cha wizi wa kawe .
Vilevile kuna asilimia kubwa ya Bajaji na Bodaboda wanashirikiana na wezi au wao vilevile ni wezi .
Huyo dogo atakuwa anatumia bangi au ni mwizi
Alomuua washamkamata sijui wanaenda kuwapiga raia kwasababu gani tena

Sent from my SM-A725F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom