Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Afande ( Luteni Kanali ) aliyeuawa jana Kawe Jirani na Baa maarufu ya Bombardier anaitwa Muna.

Marehemu ni Mkazi wa Mkoa wa Singida.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa kapandishwa Cheo na alikuwa anaenda kuwa Mkuu wa Kikosi Mkoani Arusha na leo Ijumaa ndiyo alikuwa anatakiwa Kuripoti tayari kukabidhiwa Majukumu.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna aliuliwa kwa Kuchomwa na Kisu cha Kukunja na Kijana aitwae Kato huku Mkewe na Mwanae wa Kiume wakiwa ndani ya Gari.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa ameenda Kubadili Tairi za Gari lake kwa Mfanyabiashara aitwae Chinga ambaye huwa Wanakunywa wote katika Baa yake ya Maifea Kawe ambayo ndiyo huwa anapenda Kunywa na hata wakati anachomwa Kisu hicho alikuwa amekunya kidogo ila anajitambua.

Afande Luteni Kanali Muna ndiyo alikuwa wa Kwanza kumkabili ( Kuzozana ) na Kijana ( Mchoma Kisu aitwae ) Kato baada ya Kuombwa asogeze Gari lake ili apite ndiyo Marehemu Afande Luteni Kanali Muna kwa Jeuri na Ubabe akamjibu Dogo ( Kato ) vibaya na kwenda Kumzaba Makofi mawili matatu.

Kijana aliyemchoma Kisu kilichopelekea Umauti Afande Luteni Kanali Muna aitwae Kato alikuwa anataka kuwahi Kawe mwisho Maringo ambako aliambiwa kuwa Mwizi wa Bajajj yake kaonekana na kwamba hata hicho Kisu alichokuwa nacho ( alichommaliza nacho Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ) kilikuwa ni cha kwenda Kukabiliana na huyo Mwizi wake ila Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alijiingiza tu mwenyewe katika 18 zake.

Mwili wa Marehemu Afande Luteni Kanali Muna umeagwa leo ( Mchana ) huu Hospitali ya Jeshi Lugalo na sasa uko safarini Kusafirishwa kwenda Kwao kwa Watani zangu Wanyiramba na Wanyaturu Mkoani Singida kwa Maziko rasmi Kesho.

Mchoma Kisu ( Muuaji Kato ) amekamatwa Jana akiwa njiani Kutoroka na Wanajeshi walitaka wapewe Wao, ila Jeshi la Polisi likawakatalia na Kumshikilia wao wakisema hiyo ni Kesi ya Kiraia na siyo ya Kijeshi kama ambavyo Wanajeshi walikuwa wanataka Kuilazimisha iwe hivyo.

Jana Wakazi wa Kawe ( hasa wa eneo husika ) walipokea Kipigo Kikali sana kutoka kwa Wanajeshi ( hasa MP ) kutokea Kambini Lugalo ambapo GENTAMYCINE nimekutana na baadhi ya akina Mama na Wahudumu wa Baa ya Bombardier Kawe wakiwa Wanachechemea, wanatia Huruma huku wakiwa wanatokea Hospitali za Ndahani, kwa Mambo na Shamba ( ya Serikali ) kupatiwa Matibabu kwani Jana walikuwa hawachaguliwi wa Kupigwa kwa Hasira na hakika Kipondo kilitembezwa na Wanajeshi ( MP )

Ahadi waliyoitoa Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ni kwamba Leo kuanzia Saa 10 Jioni wanarejea tena kwa Oparesheni yao Kabambe na kwamba leo watapita / wataingia nyunba kwa nyumba hata kama Unaukweka ( Unakunya ) utachomolewa Chooni uje upokee Kipigo utaje Wahuni unaowajua na ukimaliza huku ukiwa na Maumivu ya Kipigo chao unarejea Chooni kuendelea na Zoezi lako la Kunya ( Kuukweka )

Sifa zilizozoeleka za Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ni ya Ubabe wake wa Kiuanajeshi aliokuwa nao hasa kwa Raia, Kugambeka ( Kulewa ) mno Baa yake Kubwa ya Maifea Kawe ila akiwa anataka Totooz ( Udhaifu mkubwa aliokuwa nao ) alikuwa akipenda kuweka Kambi katika Baa ya Wauza Malaya ( Wachafu na Wasafi ) ya Igole iliyo Mita chache tu na Kituo cha Polisi Kawe ambacho baadhi yao hao Mihemko ya Kibaiolojia ikiwazidia huvuka tu barabara na kwenda Kuponea kwa hao hao Makahaba.

Inasemekana kilichowakera Wanajeshi wa Kawe ( hasa MP ) baada ya Boss wao Marehemu Afande Luteni Kanali Muna Kuuawa hivyo na Kijana Kato ni kwa Polisi kuwanyima / kukataa kuwapa Mtuhumiwa ili waende nae Jeshini Lugalo wakamuadabishe kwa Sheria zao.

Ni haya tu nimeona niwaletee mjue.
Mkuu GENTAMYCINE ,habari hii uliyoileta, ni ya MASIKITISHO na ndeeeeeefuu! Lakini ulivyo isimulia vizuri, mpaka msomaji anajiona naye alikuwepo kwenye tukio. Pia, tukio hilo, kwa jinsi ulivyotujuza, tunapata elimu ya kujifunza, KUHESHIMIANA, bila kujali wewe ni nani!!
 
Luteni kanali anakunywa bar za usweken na kutembea na wanawake wa ovyo ovyo.
Luteni kanali anatakiwa kunywea kwenye hoteli ya maana au officers mess kwa wenzake.
Ndio ujue hakuna jeshi hapo, ndio maana mnapelekwa pelekwa na jeshi liko kimya. Luteni kanali ni cheo kikubwa sana , kunywea usweken huku kuna officers mess ni aibu kwa JWTZ.
 
Wanajeshi wa Tanzania Bado wanaishi kwenye ndoto za jeshi la kikoloni, ubabe na ukatili Ili kuwaogopesha raia, wanajeshi inabidi wabadilike kuanzia huko kwenye kozi zao waache kuwajaza ujinga nakumbuka nikiwa JKT Kuna nyimbo tulikuwa tukiimbishwa eti ukiwa mwanajeshi unapata demu Bure, unakunywa Bure na ujinga mwingi tu tulikuwa tukiambiwa
Serikali inapenda mambo kama haya. Inataka raia waogope jeshi ili iwe rahisi kuwatawala na kuwafanya waogope kudai haki zao. Kwanza wanajeshi wengi ni walumbikeni ambao hawajui dunia inakoenda. Starehe wanazozijua wao ni pombe na wanawake.
 
Afande ( Luteni Kanali ) aliyeuawa jana Kawe Jirani na Baa maarufu ya Bombardier anaitwa Muna.

Marehemu ni Mkazi wa Mkoa wa Singida.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa kapandishwa Cheo na alikuwa anaenda kuwa Mkuu wa Kikosi Mkoani Arusha na leo Ijumaa ndiyo alikuwa anatakiwa Kuripoti tayari kukabidhiwa Majukumu.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna aliuliwa kwa Kuchomwa na Kisu cha Kukunja na Kijana aitwae Kato huku Mkewe na Mwanae wa Kiume wakiwa ndani ya Gari.

Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alikuwa ameenda Kubadili Tairi za Gari lake kwa Mfanyabiashara aitwae Chinga ambaye huwa Wanakunywa wote katika Baa yake ya Maifea Kawe ambayo ndiyo huwa anapenda Kunywa na hata wakati anachomwa Kisu hicho alikuwa amekunya kidogo ila anajitambua.

Afande Luteni Kanali Muna ndiyo alikuwa wa Kwanza kumkabili ( Kuzozana ) na Kijana ( Mchoma Kisu aitwae ) Kato baada ya Kuombwa asogeze Gari lake ili apite ndiyo Marehemu Afande Luteni Kanali Muna kwa Jeuri na Ubabe akamjibu Dogo ( Kato ) vibaya na kwenda Kumzaba Makofi mawili matatu.

Kijana aliyemchoma Kisu kilichopelekea Umauti Afande Luteni Kanali Muna aitwae Kato alikuwa anataka kuwahi Kawe mwisho Maringo ambako aliambiwa kuwa Mwizi wa Bajajj yake kaonekana na kwamba hata hicho Kisu alichokuwa nacho ( alichommaliza nacho Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ) kilikuwa ni cha kwenda Kukabiliana na huyo Mwizi wake ila Marehemu Afande Luteni Kanali Muna alijiingiza tu mwenyewe katika 18 zake.

Mwili wa Marehemu Afande Luteni Kanali Muna umeagwa leo ( Mchana ) huu Hospitali ya Jeshi Lugalo na sasa uko safarini Kusafirishwa kwenda Kwao kwa Watani zangu Wanyiramba na Wanyaturu Mkoani Singida kwa Maziko rasmi Kesho.

Mchoma Kisu ( Muuaji Kato ) amekamatwa Jana akiwa njiani Kutoroka na Wanajeshi walitaka wapewe Wao, ila Jeshi la Polisi likawakatalia na Kumshikilia wao wakisema hiyo ni Kesi ya Kiraia na siyo ya Kijeshi kama ambavyo Wanajeshi walikuwa wanataka Kuilazimisha iwe hivyo.

Jana Wakazi wa Kawe ( hasa wa eneo husika ) walipokea Kipigo Kikali sana kutoka kwa Wanajeshi ( hasa MP ) kutokea Kambini Lugalo ambapo GENTAMYCINE nimekutana na baadhi ya akina Mama na Wahudumu wa Baa ya Bombardier Kawe wakiwa Wanachechemea, wanatia Huruma huku wakiwa wanatokea Hospitali za Ndahani, kwa Mambo na Shamba ( ya Serikali ) kupatiwa Matibabu kwani Jana walikuwa hawachaguliwi wa Kupigwa kwa Hasira na hakika Kipondo kilitembezwa na Wanajeshi ( MP )

Ahadi waliyoitoa Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ni kwamba Leo kuanzia Saa 10 Jioni wanarejea tena kwa Oparesheni yao Kabambe na kwamba leo watapita / wataingia nyunba kwa nyumba hata kama Unaukweka ( Unakunya ) utachomolewa Chooni uje upokee Kipigo utaje Wahuni unaowajua na ukimaliza huku ukiwa na Maumivu ya Kipigo chao unarejea Chooni kuendelea na Zoezi lako la Kunya ( Kuukweka )

Sifa zilizozoeleka za Marehemu Afande Luteni Kanali Muna ni ya Ubabe wake wa Kiuanajeshi aliokuwa nao hasa kwa Raia, Kugambeka ( Kulewa ) mno Baa yake Kubwa ya Maifea Kawe ila akiwa anataka Totooz ( Udhaifu mkubwa aliokuwa nao ) alikuwa akipenda kuweka Kambi katika Baa ya Wauza Malaya ( Wachafu na Wasafi ) ya Igole iliyo Mita chache tu na Kituo cha Polisi Kawe ambacho baadhi yao hao Mihemko ya Kibaiolojia ikiwazidia huvuka tu barabara na kwenda Kuponea kwa hao hao Makahaba.

Inasemekana kilichowakera Wanajeshi wa Kawe ( hasa MP ) baada ya Boss wao Marehemu Afande Luteni Kanali Muna Kuuawa hivyo na Kijana Kato ni kwa Polisi kuwanyima / kukataa kuwapa Mtuhumiwa ili waende nae Jeshini Lugalo wakamuadabishe kwa Sheria zao.

Ni haya tu nimeona niwaletee mjue.
Baadhi ya wanajeshi wetu katika jeshi letu wanaliaibisha jeshi....Yaani kupata mafunzo ya kijeshi tu na kuvaa sare iwe ndo sababu ya kuwa mbabe mtaani!? Wanajeshi wengi ni wababe wanapokuwa uraiani na hasa wakiwa kwenye sare zao wanasahau wao ni sehemu ya jamii na wana jukumu la kutunza Amani...Najiuliza hao wajeda wanapata wapi nguvu ya kupiga wananchi wasio na hatua kisa mwenzao kauawa na wanajua suala hilo lipo kwenye mikono ya polisi? Enyi wanajeshi msijisahau sana, jeshi sio kuvaa sare tu na kutumia nguvu mahali pasipohitajika!
 
sasa tupo zaidi ya Saa kumi jioni mtoa mada vipi kutupatia uvunjifu wa amani kati ya jeshi na raia hapo Kawe
 
Maisha ya cheo yanakutaka uongozwe sana na hekima na kujitambua huku ukiwa mwepesi wa kuelewa mazingira kwamba wapi utumie cheo chako wapi usikitumie.

Kwa case ya huyu marehemu unaweza ukaona huyu alinyimwa vitu hivi ndiyo maana cheo chake (sizungumzii hicho kipya alichokuwa anaenda kukitumikia bali chochote alichokuwa nacho) kimekuwa mlango wa kumuondoa duniani,hauwezi ukaambiwa tu sogeza gari halafu ukaanza kupiga watu makofi huo ni ulimbukeni afe tu.
Kabisa. Our home boy Kato atatoka tu. Huyo mbuzi muonevu akawaonee sasa na malaika wa motoni. Nachukia sana mtu anayenyanyasa watu kwa cheo chake. Ni ushamba wa kiwango cha juu sana.
 
Ogopa sana kuingia mtaani na ukataka kutumia cheo chako kunyanyasa raia! Huyo jamaa Kato naamini atatoka tu! Wajeshi wakivaaga magwanda akili zinahama na kujiona miungu mtu! Pole yake na pole kwa familia kwa msiba!
 
Wanajeshi wa Tanzania Bado wanaishi kwenye ndoto za jeshi la kikoloni, ubabe na ukatili Ili kuwaogopesha raia, wanajeshi inabidi wabadilike kuanzia huko kwenye kozi zao waache kuwajaza ujinga nakumbuka nikiwa JKT Kuna nyimbo tulikuwa tukiimbishwa eti ukiwa mwanajeshi unapata demu Bure, unakunywa Bure na ujinga mwingi tu tulikuwa tukiambiwa
Mafunzo mengi vita hakuna ss hapo unafikiri nani apigwe!!??
 
Back
Top Bottom