benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Vitu vichache vya kipekee vinajionyesha katika bajeti ya Tanzania iliyofanyiwa ukaguzi na CAG. Kwa mfano, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwenye miaka ya hivi karibuni, mapato yaliyopatikana yalizidi makadirio ya bajeti.
Kwenye vitabu vyake, CAG ameonesha kwamba ingawa serikali ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 36.681 lakini ikakusanya shilingi trilioni 37.992 – ongezeko la asilimia 4 kulinganisha na matarajio.
Katika hali ya kawaida, kutokana na ukosefu wa usimamizi uliojionyesha huko nyuma, ongezeko hili la mapato lingezua changamoto na huenda lingepotea. Lakini kilichotokea ni tofauti. Fedha zote zilizokusanywa na serikali zimepelekwa kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kiasi kilekile kilichokusanywa ndicho hicho kimekwenda Serikalini.
Kwa mfano, jedwali la CAG linaonesha kwamba jumla ya makusanyo yote yaliyoingia katika Mfuko Mkuu hadi Juni 30, 2022 yalifikia kiasi cha shilingi trilioni 35.486, lakini matumizi yalikuwa shilingi trilioni 36.063.
Itaonekana hapo kwamba matumizi ni makubwa kuliko makusanyo. Ripoti ya CAG imefafanua kwamba nakisi iliyopo hapo, kiasi cha shilingi bilioni 577, inatokana na miradi ambayo wafadhili waliamua fedha zitumike kwenye miradi moja kwa moja au ziingie kwenye akaunti za mashirika yanayojihusisha na mambo yaliyofadhiliwa. Hizo ni pesa ambazo hazikuingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya karibuni ya Tanzania hasa baada ya tukio la “trilioni 1.5” ambapo CAG aliruhusiwa kufanya ukaguzi kwenye Mfuko wa Hazina. Na ukaguzi huo sasa umefichua kwamba lile ‘shimo’ lililokuwepo zamani la kutowiana kwa mapato na matumizi ya serikali, sasa limezibwa.
Matokeo ya hatua hii ni kwamba leo mjadala hauhusu tena wapi zilipo shilingi trilioni kadhaa ambazo zilikusanywa lakini hazijulikani zilipo, mjadala unahusu kilichokusanywa kimetumika vipi. Mjadala sasa unajikita kwenye namna ambavyo mapato yametumika, siyo kwenye mapato yaliyoyekuka kusikojulikana kwa kutoonekana kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na kutoidhinishwa na Bunge.
Hii ni hatua kubwa kwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiyo kwanza ametimiza miaka miwili ofisini. Kama wasemavyo Waswahili, yajayo yanafurahisha.