Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Rais Samia aliongea kwa ukali pale bandarini siku ya tarehe 4 mwezi huu wa Desemba. Sina uhakika kama wasaidizi wake walimtegemea kumsikia akiongea kwa kujiamini kiasi kile. Ni kama vile Rais ameanza kutanua makucha yake. Ule muda wa honeymoon ya miezi ya kutambuana kati yake na wasaidizi wake imeshamalizika.
Akamwaga kila kitu hadharani na kuelezea kwa kirefu namna kampuni ya kituruki ilivyogundulika kuwa ni ya madalali na sio yenye uwezo wa kufanya kazi iliyoajiriwa kuifanya. Mpaka kuja kuigundua kampuni hiyo kuwa haina uwezo tayari mikataba ilishaandikwa na kusainiwa mbele ya watu.
Lipo somo la kufanyiwa kazi kwa upande wa serikali. Isiwe ni suala rahisi tu kujivunia kuleta wawekezaji wapya. Isiwe ni kama sifa hivi kwa viongozi wenye mamlaka ya uwekezaji kutaja namba mpya ya wawekezaji walioweza kupatikana ndani ya kipindi fulani.
Kilichofanyika kwa kampuni ya kituruki na kifanyike kwa makampuni yote yanayotarajia kupewa tenda kubwa kubwa. Tusizuzuke tu na rangi za ngozi zao, tusidanganyike tu na masuti pamoja na vitambi vyao, twende mbali zaidi katika kuhakikisha uhalali wa hiyo mikataba tunayoingia. Sio kila anayekuja kuitikia wito wa ziara za Rais wetu huko nje na ujumbe wake, anayo nia njema kwa taifa letu.
Hawa watu hawatupendi kama tunavyojidanganya kama wanatupenda. Wengine wanatuona kama wajinga ambao wamechelewa kutambua ukubwa wa rasilimali walizonazo. Wengine wana hulka tu za kitapeli wamezoea kukusanya utajiri kwa njia haramu.
Hivyo ni jukumu letu la kwenda taratibu na kwa umakini tunapojiandaa kusaini mikataba na wawekezaji.