Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
TOFAUTI YA UPENDO NA HESHIMA
Alisema Niccolo Machiavelli kwamba "Watu huwa wepesi kumdhuru au kumuangamiza mtu ambaye anayehitaji kupendwa sana kuliko mtu ambaye ametengeneza mazingira ya kuheshimiwa/ kuogopwa.
Kisaikolojia ni kwamba upendo husababisha mtu ana-Relax ,mtu ukijua unapendwa sana ni rahisi kuanza kumdharau, kumjibu vibaya, kumgombeza, kumtukana matusi ya nguoni, kumdhalilisha,kumtishia muachane yule ambaye unajua anakupenda sana na hawezi kuishi bila wewe.
Lakini haiwezekani kumdhalilisha, kumtishia muachane, kumgombeza, kumtukana,kumpiga,kumsema vibaya sana, kumkaripia kwa maneno makali sana mtu ambaye unayemuheshimu.
Kwanini upendo hautakiwi kuwa kipaumbele kwa mwanaume?
Kisaikolojia ni kwamba mwanamke pale ambapo anapogundua anapendwa sana kuliko mtu yeyote hapa ulimwenguni huanza kujenga hisia kwamba huyu mwanaume amemkamata na vilevile mwanaume huyo hana ujanja wowote kwake.
Pale ambapo mwanamke anapojihisi yupo salama kwa 100% kwamba penzi lake lipo imara sana na mwanaume wake hana ujanja wa kumuacha hata akifanya makosa makubwa kiasi gani ..
Basi hapo kwa hulka na asili ya mwanamke husababisha mwanamke anajikuta anaanza kumpuuza mwenza wake kwa makusudi, mwanamke hujikuta anamchukia sana mwenza wake bila sababu zozote.
Na inapotokea mwanaume akizidisha kuwa mwema sana ili kumfurahisha na kumridhisha mwanamke basi husababisha mwanamke anapoteza hisia za mapenzi moja kwa moja,hivyo mwanamke hujikuta anapata hasira sana kila akiona sms ,au simu mfululizo za mwenza wake.
Kunyenyekea sana,kuongea kwa upole sana, kubembeleza sana, kutetemeka sana,kuongea kwa hofu kupitiliza mbele ya mwanamke huwa miongoni mwa sababu zenye kufanya mwanamke anapoteza hisia za mapenzi kwa mwanaume.
Kwanini wanaume wenye kujiamini sana mbele ya mwanamke huwa hawana upendo na mwanamke? Ni kwa sababu uwezo wa kujiamini unapatikana pale ambapo upo na uzoefu juu ya kitu au kazi fulani.
Uwezo wa mwanaume kuongea kitu chochote mbele ya mwanamke huwa unajitokeza pale ambapo mwanaume hana hofu ya mahusiano kuvunjika na uwezo wa mwanamke kuongea kwa ukali sana,ubabe, ubishi, ukorofi, kumgombeza, kumtukana, kumdhalilisha mwanaume huwa unatokana na pale ambapo mwanamke hana hofu ya mahusiano kuvunjika.
Hii maana yake ndiyo sababu mwanamke ambaye huwa mbishi,mbabe,mgomvi mgomvi huwa anapata wanaume wenye huruma kupitiliza, unyenyekevu, uvumilivu,wenye kujali sana,mwanaume ambaye anaweza kukabidhi mshahara wake wote au ATM card yake kwa mwenza wake ili apate upendo wa mwanamke huyo.
Kwanini wanaume wenye kujiamini kupitiliza hupata wanawake wenye huruma kupitiliza, unyenyekevu, kusamehe makosa,kujali sana ni kwa sababu yule ambaye mwenye kujiamini sana huwa hana hofu ya mahusiano kuvunjika hivyo hafanyi uwekezaji wowote isipokuwa a anasubiri ukifanya makosa kidogo tu muachane
Hivyo yule ambaye mwenye hofu ya mahusiano kuvunjika huwa anajituma sana kuokoa mahusiano yasije kuvunjika.
Kadiri unavyokuwa unajituma sana kunusuru mahusiano kuvunjika ndivyo husababisha unashindwa kuvunja mahusiano hayo hata kama unadhalilishwa,kunyimwa unyumba, kusalitiwa kila siku.
Kwanini wanaume wanataka kupendwa sana hupata wanawake wasiokuwa na huruma hata chembe, mwanamke anakuwa hana shukurani lakini anakuwa mwenye kumpelekesha sana mwanaume wake ? Ni kwa sababu upole sana, unyenyekevu, uvumilivu uliopindukia,kusaidia sana, kujitoa mhanga huwa ni kiashiria cha UPENDO WA DHATI,hivyo ukiwa na sifa hizo automatically kipaumbele chako kinakuwa siyo HESHIMA bali KUPENDWA.
Mwanaume kwa asili huwa kichwa cha familia,kwa maana hiyo haiwezekani kuwa KIONGOZI shupavu ndani ya familia kisha uwe na kipaumbele cha kutaka KUPENDWA.
Sifa ya kiongozi huwa anasema kile ambacho ni sahihi bila kujali nani atakwazika.
Kwa asili mwanamke huwa anapenda kujishusha mbele ya mwanaume mwenye mamlaka na nguvu mbele yake.
Hivyo sifa kuu ya mwanaume huwa ni kuhitaji Ukuu,nguvu,mamlaka,kauli ya mwisho.
Hii ndiyo sababu wanaume wenye upendo wa dhati huparamia wanawake wenye kiu ya mamlaka ndani ya familia zao badala ya unyenyekevu na utii kwa waume zao.
Hauwezi kumvutia mwanamke ambaye anataka mwanaume ambaye ni kichwa cha familia ikiwa wewe ni mwanaume ambaye kipaumbele chako ni kutaka kumbadilisha tabia mwanamke,pamoja na kutaka mwanamke akupende.
Mwanamke yeyote akiona unapambana kumbadilisha tabia anajua kabisa unampenda sana kuliko mtu yeyote hapa ulimwenguni na vilevile hauwezi kuishi bila yeye,na hauna ujanja wa kumuacha hivyo hata akiondoka kwenda kwa mwanaume mwengine ambaye anajua ni mwanaume wa HADHI yake bado atarudi kwa yule ambaye alikuwa anataka kumbadilisha tabia kwa sababu anajua muda wowote akirudi milango ipo wazi ni suala la kusingizia shetani alimpitia tu ,na kujifanya amebadilika tabia.
Ukitaka mwenza wako akupende ni wazi kwamba mwenza wako akijifanya amenuna, amesusia chakula,akigoma kukupa unyumba utaanza kujichukia, kujilaumu,kupiga magoti, kutishia kujiua, kumnyenyekea, kuanza kulia, kunung'unika, kulalamika huku unataka huruma yake.
Je mwenza wako anaweza kukuheshimu wakati anakuona unataka huruma yake ? Haiwezekani
Hauwezi kudai HESHIMA sehemu ambayo unapiga magoti, unaomba msamaha kwa kubembeleza sana kila dakika.
HESHIMA inapatikana sehemu ambayo kuna hofu.Mtu anawezaje kujenga hofu juu yako kama anajua hauwezi kuishi bila yeye wala hauwezi kumuacha hata akifanya makosa makubwa sana? Haiwezekani
Mtu ambaye kipaumbele chake ni kupendwa anakuwa amejichimbia kaburi lake yeye mwenyewe.
Mtu ambaye anayekupenda sana anafanya unakuwa na uhakika kwamba hawezi kuishi bila wewe, lakini yule ambaye unamheshimu unakuwa na hofu kitu gani kibaya anaweza kufanya kwako endapo utamkosea HESHIMA.