Mulokozi GG
Member
- Jul 14, 2021
- 34
- 44
Binadamu kama viumbe wengine duniani ni kiumbe ambaye msingi wa uwepo wake ni mabadiliko au ukuaji, zaidi ya viumbe wengine baadhi ya ukuaji wake lazima aufanye kwa hiyari yake. Ni katika kipengele cha uhiyari katika baadhi ya ukuaji alichonacho na alichopewa binadamu, ambacho endapo akikitumia vibaya maisha yake yanakuwa machungu na endapo akikitumia vizuri anatenda mambo ambayo yanachukuliwa kama maajabu.
Katika kutekeleza shughuli zake binadamu huwa na msukumo ambao huwa unajitokeza kama hali au hisia ndani yake, hali hizi ndani ya mtu zimepewa majina kama upendo, hasira, furaha, woga n.k. Hali hizi huweza kumpa mtu hamasa au huwa chanzo cha kumkatisha tamaa kutokana na anavyo zichukulia.
Upendo kama moja ya hali au hisia ndani ya mtu, ni hisia ambazo zinao mchango wa moja kwa moja kwenye shughuli zote anazozifanya mtu awe anajua au hajui. Ndani ya jamii yetu ni kawaida kumsikia mtu akisema mimi ninapenda au sipendi kitu fulani.
Lakini ni kweli mtu akisema napenda hiki au sipendi kile, anakipenda au hakipendi kweli.?
Upi ni msingi wa mtu kupenda au kutopenda kitu fulani.?
Katika ukuaji mtu hukutana na mazingira tofauti tofauti yanayo mfanya awe katika hali tofauti kulingana na jinsi atakavyo yachukulia. Ni katika tafsiri mtu anayoyapa mazingira, lililochimbuko la yale yote anayo dhani anayapenda au hayapenda.
Mmoja ya msingi wa akili za binadamu ni kulinda chochote kile tunachokikubali na kukipa thamani. Kwa maneno mengine mtu akifahamu na kuthamini kitu(intellect part of the mind) akili hukilinda na kukichukulia kama utambulisho wake(identity/ego part of the mind). Kwahiyo hapa akili inachokuwa inakilinda siyo thamani, umuhimu au ubora wa kitu chenyewe bali inalinda kumbukumbu na jinsi ilivyo zichukulia(identity). Kazi hii inafanywa na akili otomatiki, japo kulingana na uelewa wa mtu anaweza kuiongoza akili yake katika njia anayo itaka yeye.
Tazama video hii kupata maelezo zaidi kuhusu sehemu za akili(mind).[Sudhguru : the four parts of the mind, YouTube, Sudhguru and Bali Vinita, may 27 2015. .]
Kutoka katika msingi huu ni dhahiri asilimia kubwa ya vitu mtu anavyo dhani havipendi au anavipenda ni matokeo ya mazoea na matarajio yake tu. Aina za upendo zinazotengwa tengwa ndani ya jamii zetu siyo upendo bali ni kiwango ilichofikia akili ya mtu katika kulinda inachokifahamu. Iwe mtu amefikia kiwango cha kutoa muda wake, mali zake au uhai wake kwa ajiri ya kulinda vile anavyo dhani anavipenda, anachokilinda ni kumbukumbu na thamani aliyo zipa pamoja na matarajio.
Moja ya sababu ya msingi akili ya binadamu kulinda inacho kifahamu ni kutaka kuendelea kuwepo. Lakini jinsi akili ya mtu inavyo weza kuruhusu hali yoyote kutokea au kuingia katika hali yoyote bila kujali matokeo yatakuwa je, iwe mtu kupoteza vitu/mali, viungo vyake au hata uhai kwa ajiri ya kulinda kumbukumbu na matarajio; ni moja ya mhujiza hai katika uumbaji huu.
Mfano chukulia wewe ni kijana mwenye umuri wa miaka 30, uliyekulia katika familia yenye kitu kinacho itwa upendo na mshikamano wa hali juu. Katika hali ya dharura unaitwa kwenye kikao cha familia na wale unaowaheshimu, unaowapenda na kuwajali kama wazazi wako ulio nao sasahivi. Ndani ya kikao wanakuambia kuwa wao siyo wazazi wako bali wewe ni mtoto ambaye baba yako hafahamiki na mama yako ni Mama ntilie unayemchukulia kawaida tu, anaye fanyia biashara yake jirani na mtaa mnao kaa. Ulipo zaliwa walikuchukua na kukulea kama mtoto wao kwani yeye kipindi hicho alikuwa na matatizo ya akili, matatizo hayo alikuwa nayo kabla na baada ya kukuzaa wewe. Hivyo na yeye pia hajui kama wewe ni mtoto wake, haukuambiwa ukweli sababu ulikuwa mdogo lakini umekua wameona ni busara wakuambie ukweli.
Unadhani hisia unazoziita upendo ulizo nazo sasahivi kwa mama aliyekulea lakini wewe ukidhani ndiye aliyekuzaa zitahama moja kwa moja ukiambiwa na kuoneshwa mama halisi aliye kuzaa(kama Mama ntilie kwenye mfano hapo juu)?, Kama unadhani ndiyo; ni ndani ya muda gani.? Majibu ya maswali haya hayako moja kwa moja kwani itategemea na uwezo wa mtu kujitawala.
Kupitia mfano huu na mingine ya hivi ni dhahiri kuwa yale mtu anayo dhani hayapendi au anayapenda ni matokeo ya kile anachokijua (kumbukumbu), mtazamo wa jamii inayo mzunguka, thamani aliyozipa kumbukumbu hizo pamoja na matarajio aliyonayo. Mtiririko huu unafuatwa na akili ya mtu kuanzia kwenye vitu vikubwa hadi vidogo zaidi asivyo au anavyo dhani anavipenda.
Walio wengi kipindi wakiwa kwenye changamoto chochote kitakacho wafariji kina nafasi kubwa ya kupendwa na chochote kitakacho watatiza kina nafasi kubwa ya kutopendwa bila kujali uhalisia wake, kiwe chakula/kinywaji, wimbo, sehemu au mtu mwingine. Ili akili ya mtu iendelee kuthamini na kulinda unao itwa upendo ni lazima iendelee kupata au kuwa na taarifa nzuri kuhusu mtu au kitu husika.
Mahusiano au ndoa nyingi siku hizi siyo matokeo ya upendo bali ni matokeo ya matarajio ya mtu juu ya mtu mwingine, matarajio hayo yanaweza kuwa katika vitu/mwili au hisia. Bahati mbaya matarajio huwa ni makubwa, mengi na yasiyo weza kutimizwa. Baada ya mda matumaini ya matarajio kutimizwa yakianza kupotea wengi huhisi upendo ndiyo ulioisha, lakini katika uhalisia ni akili ya mtu imeona mwelekeo tofauti na ule ilio utarajia. Mtu kutafuta mwenza mbadala akiwa na matarajio yale yale au yaliyo boreshwa kidogo haisaidii kwani tatizo kubwa siyo mwenza, tatizo kubwa ni matarajio mengi na dhahania.
Njia inayo weza kusaidia kuendeleza mahusiano licha ya matarajio kuonekana hayatotimia ni; uwazi kwa mwenza na kujitahidi kufikiria yale yaliyo mazuri kwake, kwani akili inaweza kuzalisha hisia upya pale zilipo toweka au zisipo kuwa kabisa ndiyo maana kuna kutongoza/kushawishi hivyo mtu anakuwa anaishawishi akili yake upya. Mtu akifanya zoezi hili kwa ufasaha hisia zinarudi kama awali, kamwe asitafute mwenza mbadala. Kwani akiipa akili nafasi ya kumuongoza na kutafuta mwenza mwingine bila yeye kujua, matarajio yale yale akili inayahamishia kwa huyo mwenza mbadala. Baada ya mda hali itajirudia ile ile na mahusiano yataonekana machungu au jinsia tofauti na yake wote hawafai. Kumbe tatizo siyo jinsia au mahusiano bali ni matarajio yasiyo weza kutimia anayokuwa ameyabeba mtu.
Hivyo katika jamii yetu hisia za upendo zimegeuzwa kama bidhaa au biashara fulani, ambapo mtu anapenda kitu fulani sababu kinampatia kitu au hisia fulani. Sababu anategemea mtu au kitu kupata hisia fulani matokeo yake ni mazoea na mwisho wake ni uraibu(addiction) bila yeye kujua, mtu anaweza kuwa na uraibu wa ngono, uraibu wa vyakula/vinyaji, uraibu wa michezo n.k.
Tatizo la uraibu, hudumaza uwezo wa mtu na siku mtu au kitu kilicho mletea na kinachomfanya awe na uraibu huo kikienda tofauti na alivyo kizoea au kisipo kuwepo kabisa, mhusika anaweza kufanya chochote ili tu aondokane na maumivu ya kihisia anayo yahisi mda huo.
Upendo halisi ni nguvu au kani ya ulimwengu inayojieleza kupitia mtu kama msukumo wa kufanya kitu flani kwenye mazingira yanayo mzunguka. Kwenye kila anacho kifanya mtu kuna kitu anacho KITAKA kama msukumo wa kufanya kile anacho kifanya. Mtu anaweza akadhani amefanya kitu kwa sababu ya hasira, woga, wivu n.k, ndiyo hisia nyingine zina mchango wake lakini nyuma ya hisia zote kuna hisia ya KUTAKA hali fulani iwe tofauti na hali ilivyo.
Upendo ni nguvu halisi ndani ya mtu ambayo haijaelekezwa kwa mtu au kitu chochote, bali ipo kama ilivyo na mtu yeyote anaweza kuitumia nguvu hiyo kufanya kitu chanya au hasi kwenye jamii.
Mfano umeme ni nguvu na kupitia nguvu hii mtu anaweza kuwasha taa usiku akapata mwanga, kupitia umeme mtu unaweza kuwasha injini za viwanda na kutengeneza bidhaa zinazo fanya maisha ya watu yaende kwa urahisi. Lakini umeme huo huo unaweza kuondoa uhai wa maelfu ya watu ndani ya dakika chache ukitumiwa vibaya.
Hivyo hivyo na upendo ni nguvu na siraha isiyo na mfano kwa mtu anaye utumia vizuri pia upendo ni hatari kwa mtu anaye utumia vibaya iwe kwa kujua au kwa kutokujua.
Mtu yeyote anatumia vibaya upendo au kwa neno lililozoeleka hana upendo kama hamuoni mwanamke yeyote njiani na kumpa heshima sawa na anayompa mama yake mzazi. Mtu yeyote hana upendo kama hawaoni watoto mtaani apitapo kama watoto wake au wadogo zake. Mtu yeyote hana upendo kama njaa ya matumbo na machungu ya watu sehemu fulani hayamugusi kama njaa ya tumbo lake na maumivu yake mwenyewe.
Japo upendo siyo matumizi mabaya ya hisia kwa kuwahurumia wanao kataa kutumia akili yao kujisaidia wenyewe, upendo ni msingi wa kutambua kuwa sote tupo kwasababu ni zao la nguvu moja(Muumba) na sote tupo katika msitari mmoja kuzaliwa na kufa.
Zipo njia nyingi za kuwa na kinga ya milele na kuepukana na maumivu kama msongo wa mawazo, hasira na hisia nyingine hasi na kuuishi upendo. Mmoja ya njia hizo ni uwezo wa mtu kujitofautisha yeye na vitu vinavyo mzunguka. Mtu kutambua kwa undani kabisa(inner realization) kuwa ana akili lakini yeye siyo akili, mtu kutambua kuwa ana mwili na hisia lakini yeye siyo mwili au hisia, kutambua kuwa ana wazazi, watoto, ndugu na marafiki lakini yeye siyo wote hao, kutambua kuwa ana mali lakini yeye siyo mali alizo nazo.
Watu wengi ndani ya jamii yetu wakiweza kuhisi na kufikia hatua hii ya ufahamu mabadiliko yatakuwa mepesi sana kufanyika na hakika jamii yetu tutakuwa na tunao uwezo wa kuigeuza paradiso, kwani upendo hautakuwa ndani ya matarajio yetu bali upendo utakuwa ndani ya ufahamu wetu.

Upvote
5