Upendo ni lugha ya vitendo sio ya maneno matupu, kama huamini mwambie mbwa I LOVE YOU kama atakuelewa

Upendo ni lugha ya vitendo sio ya maneno matupu, kama huamini mwambie mbwa I LOVE YOU kama atakuelewa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Upendo ni jambo adhimu sana ambalo sisi wanadamu ni lazima tulifanye, sio tuliongelee tu.

Mbwa ukimwambia I LOVE YOU hawezi kukuelewa. Ila ukimuonyesha upendo atakuelewa sana, na atakupenda pia.

Je, huyo unayemwambia unampenda, je unamuoneshaje huo upendo?

1 KOR 13​

Karama ya Upendo
1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
 
Hakika umenena, I love you nyingiii.... kumtunza mtoto wa watu lazima uje umwanzishie thread huku.Mi neno nakupenda hata silithamini sikuhizi maana hata kasuku ukimfunza aweza ongea. Ni sawa na kumwambia mwanaume I love you so much afu mbususu humpi si kampende hata kaka Yako bas🚴🚴
 
Do you love me seriously? Hili swali nkiulizwaga natabasam na kisha kuchekaaaa... Then najibuu
Off course, why not?
 
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu
Unaongea upendo upi ? Kwamba I love you, ila ujue mkono mtupu haulambwi
Upendo na udangaji ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Hakika umenena, I love you nyingiii.... kumtunza mtoto wa watu lazima uje umwanzishie thread huku.Mi neno nakupenda hata silithamini sikuhizi maana hata kasuku ukimfunza aweza ongea. Ni sawa na kumwambia mwanaume I love you so much afu mbususu humpi si kampende hata kaka Yako bas🚴🚴
wewe wewe wewe😂
 
Mtume Paulo akifundisha kitu Alafu hujamwelewa basi wewe hutamwelewa mtu yoyote Yule
 
Kwa mwanaume upendo ni kutanua wallet, kwa mwanamke ni kutanua miguu.
 
Back
Top Bottom