Daima upendo una sura mbili, japo wengi wanaijua moja, wakati wa raha,
faraja na nyimbo na zawadi kedekede, wanaridhika na upendo huo,
ila upendo una kipimo chake wakati wa shida,
karaha na wakati wa magonjwa wakati ambapo waona
tabia, kasoro na mapungufu; hapo ndipo upendo hupimwa,
Yule anayeweza kusimama nawe, wakati wengine kawaida wangekukimbia,
tena awezae kukufichia aibu wakati wengine kikawaida wangekutangaza,
Yule ambaye hapendi kuona unaharibikiwa,
hata mkikosana hapendi kuona unateseka
Huyo ndiye mwenye upendo wa kweli
Huyo ndiye mwenye upendo wa kweli
Upendo Upendo
(upendo) haupo (haumo) katika maneno
(unaonekana) Unaonekana (onekana) kwa matendo
Yeh yeh yeh
(Hauonekani) hauonekani (honekani) kwenye raha
(wathibitika) wathibitika wakati wakati wa shida
Wathibitika (wathibitika wakati wa shida)
Watu duniani wanahangaika, kupenda Vinavyopendeza,
wanasahau kupenda vinavyo Pendeza,
hakuna thamani isipokuwa kupenda Visivyo pendeka,
Kama mkiwapenda wale wapendao mwafanya
Ziada gani, wapendeni waombeeni wanao Waudhi,
Baba yenu Mbinguni atawapa thawabu,
na watu watasemaa huu ndio upendo wa kweli,
Jipime kama kweli wewe una upendo, Ulifanyaje,
ndugu yako alipokukosea Ulimsengenya,
au ulimuombea ulimpenda bure, au ulimpaka matope
Ulimsengenya, au ulimuombea
Ulimpenda bure, au ulimpaka matope
Jijibu kama una upendo wa kweli
Jijibu kama una upendo wa kweli
Countrywide soma hiyo