Upendo wa bunge umeyeyuka kwa sababu gani ?

Upendo wa bunge umeyeyuka kwa sababu gani ?

jamaikatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
400
Reaction score
1,429
Enzi za Kikwete, Tundu Lissu ananyukana kwa hoja na Mwanasheria Mkuu wa serikali... Lukuvi anaingilia... Mara Chenge naye anaibuka... Watu wanagonga meza, mara kwa mbali unasikia "Kuhusu utaratibu....", mara "Muongozo..."

Halafu Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu anakataa muongozo wala utaratibu...
Anamruhusu Lissu aendelee kutema madini... Deo Filikunjombe anainuka kutoa taarifa... Ghafla John Mnyika anasimama...

Burudaaaaaani!...

Kesho asubuhi, unakutana na picha ya Tundu Lissu, Anne Makinda na Mohamed Mnyaa pamoja na Shukuru Kawambwa wanateta nje ya viwanja vya Bunge...

Kwa mbaaali unamuona Peter Msigwa anacheka na Serukamba, huku Halima Madee na Iddi Azzan wakiwa kando yao...

Hivi, huu UPENDO umeyeyuka kwa sababu gani?🤔
 
Screenshot_20250714-185856~2.png
 
Back
Top Bottom