Sasa kama mnafahamu hilo nafikiri badala ya kulaumu wanawake tuanze kulaumu wazazi ambao bado wanaamini tamaduni hizo maana hata wanawake nao ni victims tu wa hizo imani, kuna makabila hadi leo binti akisema anataka akaolewe tu bila mahari kisa kampenda mwanaume ukoo mzima wanashika vichwa, na kifuatacho ni vikao visivyoisha vya kuwasema binti pamoja na wazazi au walezi wake
Naelewa unazungumzia nini.
Wanawake ndio wahanga wakubwa wa hizo mila sema wengi hawajui kwa sababu hawana macho ya kuona Mbele.
MÃmi silaumu mabinti wala silaumu wazazi. Nitajilaumu mwenyewe ikiwa nitafanya jambo ambalo ninaona kabisa hili ni uongo, unyanyasaji, ukandamizaji wa haki za ninayempenda na anayenipenda.
Siwezi kutoa mahari. Hiyo ni moja.
Pili ninatafuta mwanamke ambaye anamuona na mtazamo kama wangu. Sitaki kumuumiza mtu kisa mtazamo na mila na desturi zao.
Yeye kama anataka kutolewa mahari basi nitamuacha atafute wanaume wenye mitazamo na muono wa aina hiyo.
Nimeshuhudia mamia ya wanaume wanaonyanyasa wake zao kwa kisingizio cha kutolewa Mahari.
Nimeona mamia ya wanawake waliolaghaiwa kutolewa mahari kwa kudanganywa kisha wakaachwa Solemba.
Nimesikia na kuona maelfu ya wanaume wakilalamika kuhusu kutoa mahari wengine ni kubwa wengine ni ndogo. Mara sijui mahari huimalizi yaani mambo ya ajabu sana.
Binti yangu kamwe sitachukua mahari kama ambavyo mimi sikutoa mahari nilipomchukua Mama yake.
Umepata Mwanamke, mmeelewana. Kinachofuata ni kwenda kutambulishana nyumbani kwa Mwanamke na kwa mwanaume. Maswala ya pesa sijui mahari sijui wanipangie sijui niwapangie huo upuuzi haufanyiki.
Ni mambo ya aibu.
Yaani Watu wazima na akili zenu mnakaa mnapanga ati binti yetu mahari iwe ngapi? Kweli!
Huko tunapoenda itafahamika mbivu na mbichi. Mambo yote ya kijinga yatapuuzwa. Ukweli utashinda. Na uongo uongo wa kizamani utajitenga