Watanzania tuna uwezo ila changamoto kubwa inayotukabili ni kukosa kujiamini, utulivu wa akili, na kutambua thamani yetu.
Kila kitu kizuri ni lazima kitoke nje. Wakati nipo kwenye shirika moja la kiserikali nchini Tanzania kabla sijahamishiwa Nairobi, tulikuwa na mshauri wa nje mmoja Mzungu ambaye alipiga mpunga mrefu, na kazi aliyoifanya yaani tulijiuliza wenyewe hivi hii kitu uongozi ulishindwa kutuamini sisi na kutupa hizi hela?
Tanzania ni jamii ya watu wa hovyo wenye utumwa wa kifikra mkubwa sana kuanzia ngazi za juu.
Mzungu wa Simba amekuja na aliivuruga SSC na kusababisha sintofaham kubwa na hakuwahi kuleta matokeo na mpunga mrefu alikuwa anaupiga kweli kweli. Tatizo ni rangi au ni nini?
Imani yangu inaniambia kuna uwezekano mkubwa wa kuwa kweli kwamba kocha anayetokea Tanzania kuifundisha SSC au Yanga wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa sababu mbalimbali, mfano;
lugha, ambayo itamsaidia kujua asili ya mpira wa Tanzania na Africa, kusoma tu maoni ya mashabiki inakupa taswira.
Naiona safari ya mgunda kimataifa, hata hawa kina Ibenge walianzia huko huko, Juma hiyo ndiyo njia yako ya kwenda, usiache, engeneza njia yako mwenyewe.
Simba na Yanga tunawashauri mnapotaka kuajiri makocha anzeni kwanza na ndani, mkikosa ndiyo muende nje ya Tanzania.
Wataalam wa ndani wapo, sema mnawachukulia poa na inawagharimu. Toeni hata mkataba wa mwaka mmoja mmoja kuwapima, acheneni na mambo ya uzoefu, historia, na rangi nyeupe, zingatis kwenye maudhui.
Mnafeli, na kuleta watu wasiojua lunga ya ndani wala kimataifa, matokeo yake yale mazungumzo ya moja kwa moja kati wachezaji na kocha na jamii haipo. Kocha hawezi hata kusoma maoni ya mashabiki, anachokitumia ni kile kilicho kwenye akili yake, basi.
Ndani tuna watu, wakuzeni na mtafanikiwa.
Ushauri kwa Mgunda
1. Kibu awe na mbadala wake, Kibu bize sana uwanjani lakini hana madhara wala usahihi, huyu awe anaingia kama anavyoingia sako ambaye ni self centered.
2. Tunampa heshima kubwa Mohammed Hussein, lakini kwa sasa ni kama kichwa chake kimecheza, amekuwa ni uchochoro sana, atafutiwe msaidizi ni muhimu vinginevyo atawagharimu.
3. Kwa sasa kuwa kama meneja, kuwa meneja ni kanuni, ujuzi, uvaaji na kujiamini, kula hivyo.
4. Kuna vikozi vya Management Kkills, pita navyo. Yaani kwa sasa wewe ni wakimataifa, ishi kama chombochombo cha kimataifa.
Kila la heri, hii SSC naiona nusu fainali. Hakika chini ya Mtanzania Juma Mgunda kwa mara ya kwanza kwenye historia. Hata Oscar Oscar baba Mzungu analijua hilo.
GGM , go go Mgunda!