Upi mtazamo wako kukithiri kwa mada zinazochochea chuki za kidini jukwaani

Nyuzi unazofukunyua nyingi ni za kidini ndio maana system inakulea hayohayo makitu uzidi kuyaona.

Binafsi naona nyuzi mbalimbali, kuna kipindi nilikua mdau wa MMU, basi kila ukifungua jf unakutana na neno "mbususu" kila uzi.

Jaribu kuingia majukwaa upendayo, hizo mada utazikuta sana hapa HHM.
 
Hii ni mbegu ambayo in long run hatujui itazaa nini hata huku jamii forum nawaasa mods wawe makini na vitu kama hivi usiidharau platform kama hii ya jamii forum tumeona Kenya na Libya machafuko yalianzia mitandaon na Afrika ya kati Seleka na ant baraka yalianzia kidg kdg kama hivi juzi kuna mtu alifungua uzi akisema ana endorse Islamophobia .
hakuna haja wala sababu hata moja kuwaziba midomo watu kwa mtazamo hasi kama huo.

Maana yake hapangekua na haja ya kua na platform huru kama hii basi, ikiwa watu wangekua wanazibwa midomo kwa kusema wanayo yaamini katika dini au ushirikina wao, right?

nchi ulizozitaja mbona hakuna hata moja inayopigana kwasababu ya udini gentleman?🐒
 
Watu wasizibwe midomo na wala hauwez kuwaziba midomo tunahitaji wana jamii forum tuwe mfano mzuri wa kuendesha mijadala isiyohamasisha chuki/ kejeli kwa imani nyingine , kwenye mifano ya machafuko hapo nimetaja Afrika ya kati i hope unafaham historia vzr .
 
Nikiri sina miaka mingi sana humu jukwaani ila nilichogundua ni kukithiri kwa mada zinazochochea chuki za kidin kwa kukejeli imani zingine kwa namna moja au nyingine binafsi ni muumin mzuri wa dini yangu japo nina cycle ya watu wengi ambao si wa imani yangu naishi nao vzr na tuna bond nzuri sana plus nimeishi kwenye jamii zenye watu wa imani tofauti tofauti na nimejifunza kwenye maisha utu hutangulia kuliko kabila/imani ya dini au itikadi na yeyote anaweza kukufaa wakati wowote, kulikoni humu kukithiri kwa hizi mada ambazo binafsi sidhan kama zina tija yoyote maana mwisho wa siku kila mtu atabakia na anachokiamini na kwanini ukerekwe na anachokiamini mwingine ?
Chuki zilizozidi ni za kikabila nafuu ya udini. Kipindi cha magu kimepandikiza ukabila na ukanda
 
Watu wasizibwe midomo na wala hauwez kuwaziba midomo tunahitaji wana jamii forum tuwe mfano mzuri wa kuendesha mijadala isiyohamasisha chuki/ kejeli kwa imani nyingine , kwenye mifano ya machafuko hapo nimetaja Afrika ya kati i hope unafaham historia vzr .
chuki utakua nayo wewe tu gentleman dhidi ya dini nyingine isiyokuhusu...

hata hivyo,
ukiulizwa swali na mtu wa dini nyingi kuhusu dini yako, kuna ubaya gani ukamjibu na ukamuelewesha kwa ufasaha?

hata ikiwa hataki kuelewa, unaumia nini au unachukia nini na sisi ni binadamu wenye uelewa na ufahamu tofauti?

sifahamu nchi ya Africa yenye vita vya kidini gentleman, ntafurahi sana nikiijua ili nirudie utafiti tena 🐒
 
Hawa wanaotukana na kukejeli wenzao basi ukiwakuta mtaani ni wanafiki wakubwa kujifanya wanakujali na kucheka na wewe hata kuombana chumvi
Kwanini uhangaike kuishi kwa double life ili iweje kwa mfano
Unatukana dini flani kumbe anaekulipa mshahara na kukufanya uende Choo na wanao ndio huyo mwenye dini unayoitukana
Ila ukiwa nae ni Yes boss tu
Wanafiki wengi sana humu
Ndio maana mtu akisema nina hiki atatukanwa na kukejeliwa kama wanamjua 😄 🤣 wachawi wengi aisee
 
chuki utakua nayo wewe tu gentleman dhidi ya dini nyingine isiyokuhusu...

hata hivyo,
ukiulizwa swali na mtu wa dini nyingi kuhusu dini yako, kuna ubaya gani ukamjibu na ukamuelewesha kwa ufasaha?

hata ikiwa hataki kuelewa, unaumia nini au unachukia nini na sisi ni binadamu wenye uelewa na ufahamu tofauti?

sifahamu nchi ya Africa yenye vita vya kidini gentleman, ntafurahi sana nikiijua ili nirudie utafiti tena 🐒
bro nimeshuhudia mada ambazo mtu analeta swali kama kuchochea tu mjadala hata anapojibiwa unaona kinachofuata ni ubishi na kuanza kum attack mtu personally, binafsi na appreciate pale watu wanapojadiliana kwa hoja makini na kukubaliana hata pale wasipokubaliana.take ur time pitia nyuzi zinazoanza na kuuliza swali la kidin uone mwisho wa siku mjadala ulielekea wap?
 
Nikiri sina miaka mingi sana humu jukwaani ila nilichogundua ni kukithiri kwa mada zinazochochea chuki za kidin kwa kukejeli imani zingine kwa namna moja au nyingine binafsi ni muumin mzuri wa dini yangu japo nina cycle ya watu wengi ambao si wa imani yangu naishi nao vzr na tuna bond nzuri sana plus nimeishi kwenye jamii zenye watu wa imani tofauti tofauti na nimejifunza kwenye maisha utu hutangulia kuliko kabila/imani ya dini au itikadi na yeyote anaweza kukufaa wakati wowote, kulikoni humu kukithiri kwa hizi mada ambazo binafsi sidhan kama zina tija yoyote maana mwisho wa siku kila mtu atabakia na anachokiamini na kwanini ukerekwe na anachokiamini mwingine ?

Zitakuwa na mlengo fulani wa kisiasa.

Zimekaa kimchongo mchongo, yabidi kufungua macho zaidi kuweza kuona:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Hautakiwi umoja wetu kwa gharama yoyote!
 
Mijadala ya kidini haina shida kabisa,mtu ukiona hisia zako zinaumizwa unajitoa au usishiriki kabisa. Kuna nyuzi kibao za mambo mengine ambayo yanaweza kuteka attention yako.
 
Si hata huu ni kama hizo , au?
 
Kazi ya huzo dini ni kuwatenganisha watu na Mungu .
 
Nadhani si chuki za kdini, Bali ni ushabiki wa kidini!

Hii mara nyingi hutokea kwa vijana walio 20s kwa sababu ya mitizamo ya kiharakati! Kama unakumbuka mambo ya UKWATA, na TYCS!

Pia dhana kuwa ukishambulia dini nyingine inakuongezea credit kwa "Mungu" wako! Hii inatokana mahubiri yanayofundisha uokovu wa neema bila matendo!
 
Mtoa mada umeandika kitu cha msingi Sana...Kwa kusema kweli hata Mimi ni mfia dini lakini natishwa na kiwango cha kukashfiana,,kudharauliana na husda vilivyoongezeka Sana humu jukwaani baina ya wakristo na waislam...
Sometimes Huwa nawaza Labda kuna mtu au kikundi cha watu wanatuchonganisha...au Sisi wenyewe tumekiwa mahasidi Sana....Kuna vitu watu humu jukwaani wanaandika pasipo woga lakini vinaharibu umoja ukaribu na hata tolerance...,.Tu jiulize sana wafia dini humu na tubadilike wote........Tujue kwamba huu mchicha tunaoupanda tutakuja kufa tuuache ukiwa mbuyu na hakuna wa kuweza kuung'oa,,,,,,Kingine hata kama ni mwenzetu katika dini analeta kashfa tumuangalie kwa makini asijekuwa anatutumia kwa maslahi flani.....Tuwe na hekima ya kufikiria vizuri katika mijadala yetu tumshinde shetani.
 
Kabisa kuna wasaa hata mimi uwa nawaza hivyo au kuna watu wana kazi maalum ya kuchochea udini.
 
binafsi naamini we can do better kama jukwaa la great thinkers sina shida na mijadala/challenge ila tu pale inapokuwa na mlengo wa kukejeli kuliko kujifunza na ndo kinachojidhihirisha mara nyingi humu , tafuta mjadala wa dini ambao watu walijadiliana kiungwana bila kejeli nipo hapa
Mijadala ya dini haipendezi Kwa sababu hakuna anaetaka kuonekana inferior au character flani kwenye kitabu chake cha dini kusemwa/kuandikwa vibaya.....Kwa hio ni mashindano yasio na mwisho,.....Na watu wengine wafia dini huandika maneno makali yenye kuudhi Sana hivyo kuleta mashindano ya dharau kejeli na kashfa kila mmoja akivutia upande wake....Na kila mmoja muwamba Ngoma akivutia upande wake.... Mwisho inaendelea kama reversible reaction.....Wa Yerusalemu vs wa maka na madiña na Karbala...
 
Back
Top Bottom