Mtoa mada umeandika kitu cha msingi Sana...Kwa kusema kweli hata Mimi ni mfia dini lakini natishwa na kiwango cha kukashfiana,,kudharauliana na husda vilivyoongezeka Sana humu jukwaani baina ya wakristo na waislam...
Sometimes Huwa nawaza Labda kuna mtu au kikundi cha watu wanatuchonganisha...au Sisi wenyewe tumekiwa mahasidi Sana....Kuna vitu watu humu jukwaani wanaandika pasipo woga lakini vinaharibu umoja ukaribu na hata tolerance...,.Tu jiulize sana wafia dini humu na tubadilike wote........Tujue kwamba huu mchicha tunaoupanda tutakuja kufa tuuache ukiwa mbuyu na hakuna wa kuweza kuung'oa,,,,,,Kingine hata kama ni mwenzetu katika dini analeta kashfa tumuangalie kwa makini asijekuwa anatutumia kwa maslahi flani.....Tuwe na hekima ya kufikiria vizuri katika mijadala yetu tumshinde shetani.