Upi mtazamo wako kukithiri kwa mada zinazochochea chuki za kidini jukwaani

Ahsante sana mkuu
 
Nimewaza nikuweke kwenye corner utuambie ni vitabu vya dini Gani vinasema hivyo. Nikapoteza ila nimeshtuka Umeamua kuniuliza. Unanguvu Gani za Kiroho? Au imetokea tu? πŸ™„πŸ™„
πŸ˜‚ mind reader
 
ni vema ukafahamu aina ya mijadala ambayo haina hitimisho, ingawa ni muhimu zaidi ikiwa wanaojadiliana wakawa na sense of peace in minds, kitu ambacho hata kama hawajakubaliana lakini wanaishia kua na peace of mind πŸ’
 
So tuendelee kuitana makafiri,wavaa kobazi n.k si ndio ? Unavyoona hiyo mijadala ina tija gani ?
Unaujua utani.
Utani inaitwa jina lolote lile na isikasirike.
Hii ndio jamii iliyostarabika katika nyakati za Leo.
Sisi hatukasilika kuitwa Wagalatia au Makafiri.
Tunauchulia kama utani tu basi.
Mimi nina ndugu wa damu Waislamu na sijawahi kuwakebehi.
Kwani wewe ukiitwa Kobazi Kuna shida gani?
Kwani wewe ni Kobazi hadi ukasirike.
Mada za Kidini ni za kutaniana tu, na kama unazichukulia kwa usiriazi basi na ujiondoe tu.
 
Lakini una uhakika majibishano huwa yanaishia kiutan utan kwa kila mtu maana kipimo cha uvumilivu au kuhimili kejeli na utani hakifanan kwa watu wote
 
Ungetoa Mifano ya Chuki Unayoipinga Tukaona Kama Mod Wana kazi ya Kufanya Au Laah
 
Hakuna uhuru usio na mipaka.
JF yenyewe wamekuekea code of ethics, wenyewe wanaziita principles. Au hujaona watu wakila ban humu.
Nadhan tatizo linaanzia kwenye nadharia ya jukwaa huru kuna kauli inasema ,"uhuru wako unapoishia ndipo heshima ya mwingine inapoanzia."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…