Uchaguzi 2020 Upigaji kura kituo cha Kisauke B, Madale: Mawakala wa vyama wazuiwa kuingia kwa kukosa barua, CCM wadhibitiwa na Wananchi wakitaka kupewa upendeleo

Uchaguzi 2020 Upigaji kura kituo cha Kisauke B, Madale: Mawakala wa vyama wazuiwa kuingia kwa kukosa barua, CCM wadhibitiwa na Wananchi wakitaka kupewa upendeleo

Leo nimefurahi sana na misimamo ya wananzengo baada ya kukuta mawakala wote hawana barua za utambulisho hadi wakala wa chama cha Jembw na Nyundo. Msimamizi msaidizi akawatoa wote nje mpaka hapo watakapok.ilisha taratibu. Huku na huku viongozi wa CCM toka kata wakaja kushinikiza wakala wao aingie, na ndipo raia wakachachamaa kuwa kama wa mataga anaingia basi wote waingie. Ikabidi CCM wakimbie.

Ila nimependa sana hii spirit ya wapiga kura. Kumbe elimu ya mpiga kura imefanikiwa kwa kiasi fulani.

Kila la kheri uchaguzi wa 2020, na Mungu akafanikishe haki na uhuru vikatamaraki.
unafurahia UJINGA et mkuundugu? kamanda uchwala wewe ni mfitina
 
Chadema Endeleeni kijifariji

Huu ni Uchaguzi wa kuwafundisha Wasaliti wa Nchi

Muwe mnatuelewa
Mwenzio kapigwa nyundo
IMG_20201028_134737_889.jpg
 
Msimamizi msaidizi akawatoa wote nje mpaka hapo watakapokilisha taratibu. Huku na huku viongozi wa CCM toka kata wakaja kushinikiza wakala wao aingie, na ndipo raia wakachachamaa kuwa kama wa mataga anaingia basi wote waingie. Ikabidi CCM wakimbie.

Ila nimependa sana hii spirit ya wapiga kura. Kumbe elimu ya mpiga kura imefanikiwa kwa kiasi fulani.
Huyo 'Msimamizi' anastahiri kupata tuzo; na hao wananchi walioonyesha ujasiri huo ni chachu ya kuleta mabadiliko.
 
Sijajua kun tatizo gani na hawa wakurugenzi. Inakuaje wakurugenzi hawatoi barua za utambulisho kwa mawakala. Mtendaji wa kata anahusika vipi kwenye kutoa utambulisho wa mawakala. Tanzania hatuna Tume kabisa
Walijipanga kuiba kwa njia hiyo
 
Back
Top Bottom