Leo nimefurahi sana na misimamo ya wananzengo baada ya kukuta mawakala wote hawana barua za utambulisho hadi wakala wa chama cha Jembw na Nyundo. Msimamizi msaidizi akawatoa wote nje mpaka hapo watakapok.ilisha taratibu. Huku na huku viongozi wa CCM toka kata wakaja kushinikiza wakala wao aingie, na ndipo raia wakachachamaa kuwa kama wa mataga anaingia basi wote waingie. Ikabidi CCM wakimbie.
Ila nimependa sana hii spirit ya wapiga kura. Kumbe elimu ya mpiga kura imefanikiwa kwa kiasi fulani.
Kila la kheri uchaguzi wa 2020, na Mungu akafanikishe haki na uhuru vikatamaraki.