Upigaji: Vigogo wa Shirika la Bima la Taifa wakabiliwa na mashitaka 365

Bado, tunataka na mawizarani na idara na mashirika mengine ya kiserikali.

Tuanzie na ufisadi uliopo mahakamani na polisi, ziundwe task force huru za kuchunguza na kuchukuwa hatua serikalini.

Ianzwe Mahakama yenyewe.
mahakamani hasa za mwanzo na wilaya zina shida sana
 
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Samuel Kamanga na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka 365 yakiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha.

Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Evodia Kyaruzi na Wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga pamoja na Ipyana Mwakatobe wamesema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kuhujumu uchumi kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ambacho ni mali ya shirika la NIC.

Katika mashitaka hayo 365, yapo ya kughushi nyaraka mbalimbali, kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu, kuchepusha fedha, kuwasilisha nyaraka za uongo na kulisababishia hasara shirika hilo.

Washitakiwa wengine ni Tabu Kingu, Victor Mleleu, Peter Nzunda, Kenan Mpalanguro, Lusubilo Sambo na Mafworo Ngereji.

Kutokana na muda wa mahakama kuisha, washitakiwa hao wamesomewa mashitaka 101 pekee, huku mashtaka mengine wakitarajia kusomewa Jumatatu Juni 5, mwaka huu.
Asali tamu
 
Bado, tunataka na mawizarani na idara na mashirika mengine ya kiserikali.

Tuanzie na ufisadi uliopo mahakamani na polisi, ziundwe task force huru za kuchunguza na kuchukuwa hatua serikalini.

Ianzwe Mahakama yenyewe.
Kuchunguza hizo taasisi ulizozitaja,unahitaji kuleta team ya watu kutoka Nje ya Nchi ndiyo unaweza pata report ya uhakika,lakini ukitoa watu humu Nchini,utapata report ya kupikwa tu na watu wataendelea na Maisha yao Kama kawaida!!
 
Tuna tatizo kubwa sana la ufisadi Tanzania na tunakoelekea ni kubaya zaidi, kama hatuwa za makusudi hazijachukuliwa.

Sasa hivi tutaanza kuwa kama Nigeria, kama bado hatujafikia.
 
Bado, tunataka na mawizarani na idara na mashirika mengine ya kiserikali.

Tuanzie na ufisadi uliopo mahakamani na polisi, ziundwe task force huru za kuchunguza na kuchukuwa hatua serikalini.

Ianzwe Mahakama yenyewe.
Mambo mrembo....🌹
 
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Samuel Kamanga na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka 365 yakiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha.

Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Evodia Kyaruzi na Wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga pamoja na Ipyana Mwakatobe wamesema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kuhujumu uchumi kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ambacho ni mali ya shirika la NIC.

Katika mashitaka hayo 365, yapo ya kughushi nyaraka mbalimbali, kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu, kuchepusha fedha, kuwasilisha nyaraka za uongo na kulisababishia hasara shirika hilo.

Washitakiwa wengine ni Tabu Kingu, Victor Mleleu, Peter Nzunda, Kenan Mpalanguro, Lusubilo Sambo na Mafworo Ngereji.

Kutokana na muda wa mahakama kuisha, washitakiwa hao wamesomewa mashitaka 101 pekee, huku mashtaka mengine wakitarajia kusomewa Jumatatu Juni 5, mwaka huu.
Yani wote hapo wagalatia. Kobaaz mmoja tu. Hongereni kina Accumen Mo Covax adriz Dalmine kimsboy

Wagalatia tumrudieni Yesu natufanye toba jamani.

Kutoka moyoni kabisa bila unafiki nawapa hongera.
 
Back
Top Bottom