Ni vyema vijiji vipimwe na kufanyiwa tathimini kama ardhi yake inafaa Kwa makazi na shughuli za kibinadamu,Kuna baadhi ya maeneo watu wanaishi kwenye mabonde au karibu na Kingo za mito,Kuna maeneo ambayo kimsingi hayafai Kwa ajili ya makazi lakini mamlaka zipo kimya.Tusingojee mpaka majanga yatokee ndio tuanze kulaumiana.
Alijaribu Mwl. Nyerere na Vijiji vya ujamaa tukamuona hayawani. No Tanzania pekee mpaka ipitisbe sensa ndio ijue watu wake ni wangapi na wako wapi.
Taifa linahitaji sio tu kujua Lina watu wangapi, linapaswa kujua wako wapi, mahitaji yao specific kwa muda wa miaka mitano, kumi na ishirini na tano ni yepi au yatakuwa yepi.
Tunahitaji kujua wamekaaje ndani ya miji au Vijiji vyao, mtawanyiko wa huduma ukoje na utakuwaje kwa baadae. Ikitolea Kijiji kimekuwa sana huduma mpya muhimu zitakwenda wapi ili ziboreshe Mji na sio kuweka pembeni na kuua miji ya asili au chimbuko.
Tunahitaji kujua namna ya kupanga maji yetu, tukianza na maji ya Mvua, ili kuboresha ikolojia ya maeneo ya miji yetu na Hali ya hewa kwa ujumla. Tunahitaji kuboresha miundombinu kama ya maji safi, maji taka, barabara na taka ngumu ili kuchagiza ujenzi wa compact cities. Sio kuatwanyika hovyo tuu mijini ambayo inaathiri gharama za Usimamizi wa miji, na gharama za maisha kwa wakazi wa miji.
Yooote haya ni zao la mipango miji. Mipango miji ni kama Hakimu mahakamani, au refa uwanjani. Japo majina makubwa ni ya mawakili na washitaki kwenye kesi ila kesi ni nzuri tu ikiwa Hakimu ni mzuri. Au wachezaji wa pande mbili, makocha na mashabiki wanaweza kupata sifa kubwa sana ila yote yamewezekana tuu kwasababu Yuko refa au mwamuzi aliyelinda Haki za wote kufurahi.
Kwa kweli kama serikali utaendelea na utaratibu wa kufanya urasimishaji...yaani KUPOKEA maamuzi ya wananchi( uninformed decisions) za kuanzisha miji kiholela na kuzifanyabiuwa formal decisions kuyashinda majanga haya ni ndoto. Na zaidi huko mbeleni tutaona majanga ambayo hatujawahi kamwe kuyaona. Maana haya mazinholela yatakomaa kwenye maeneo hatarishi na Matokeo ya majanga kwenye maeneo hayo baadae yatakuwa ni ya kutisha.
Kwenye hili wananchi lazima wajue matown planner kazi yao ni kuwasaidia kujenga mifumo ya kulinda maslahi yao kwenye matumizi ya Ardhi, na sio kuwapangia ni Cha kufanya. Ila Hilo kutokuwapangia lisifananishwe na kuwapa ruhusu wananchi kuamua tuu kama wanavyotaka, la hasha ila ni kumaanisha kusikiliza matown planner wakiwashauri kwa kuwapa na njia mbadala ya kutumia Ardhi zao kwa namna ambayo sio hatarishi kwao na kwa wengine bila kupoteza uwezo wa kujipatia kipato stahiki.
Ninaliombea taifa hili Leo na kesho yake ikawe yenye heri. Na naliombea kama halitaweza kupata wanasiasa wanaowapenda na kuwatakia mema, angalau lipate wanasiasa wenye kiburi na shauku ya kufanya mambo sawa sawa ikiwemo kupanga miji itakayo shinda majaribu ya muda.