Upinzani hauuliwi kwa mabavu, udikteta, vitisho na ukatili, ukitaka kuua upinzani mpe Hussein Mwinyi nchi aufute upinzani

Upinzani hauuliwi kwa mabavu, udikteta, vitisho na ukatili, ukitaka kuua upinzani mpe Hussein Mwinyi nchi aufute upinzani

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Upinzani ni spirit ambayo kamwe haijawahi kuuawa kwa kuwateka wapinzani, kuwatesa, kuwafunga kwa makosa ya kubambikiza etc.

Njia rahisi ya kuua upinzani ni kupitia upendo na kuwaridhisha watu licha ya kwamba hakiwezekani kuwaridhisha watu wote kwa wakati, lakini hili linawezekana akipatikana rais mwenye akili kama Hussein Mwinyi.

Tayari Mwinyi ameshagundua kuwa kodi kubwa kwa wawekezaji ni mzigo, ambao in future, wote tutakuwa losers, muwekezaji atashindwa kufanya biashara, atafunga. Serikali itapate kodi mfanyabiashara akifunga biashara? Mwananchi atapataje bidhaa na huduma supply chain ikikatika?

Pia tunahitaji watu wenye mitaji waje kuwekeza nchini. Nani yuko tayari kuona diaspora wakileta mitaji yao bila kuulizwa umepataje pesa.

Nachelea kusema kwamba Mwinyi Yuko much visionary kuliko kaka Mandege.

Mwinyi alipita nyumba kwa nyumba akiongea na Wanzibari ana kwa ana wakimjulisha shida na dhiki zao.

Huyu mwingine alikuwa ananunua majogoo kwa laki moja, akipita kwenye msururu wa MAVIEIEITE YA KIJANI. Akimwaga tu sera zake kutoka kwenye kauntabuku la kurasa mia tatu na tatu bila kuwasikiliza wananchi wanataka nini.

Mwaka 2025 nadhani mtu sahihi wa kumshindanisha na Tundu Lissu ni Hussein Mwinyi tu.
 
Ndicho ulichowaza na sina pingamizi maana ndio mtazamo wako
 
..nadhani tuachane na fikra za "kuua" upinzani, au demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

..badala yake tujenge fikra za kuwa demokrasia ya vyama vingi iliyochangamka, na yenye HAKI sawa kwa vyama vyote.

..nadhani harakati za kuua upinzani zina GHARAMA kubwa kwa taifa, wakati mwingine hata DAMU/ROHO za watu.
 
Hussein Mwinyi wachache sana ndio wanamfahamu kwa undani. Ni mtu mwenye roho ya aina yake. Sidhani kama kuna kiongozi serikalini anafikia hata nusu yake (Wengi wanafanya mambo kujionesha na kutafuta hits/kiki).

NOTE THAT; Hussein Mwinyi wakati waziri wa ulinzi ili kuwahamasisha watendaji wake wa kazi kufanya kazi kwa utulivu na weredi, watendaji ambao waliokua wakipatwa na matatizo/ugomvi kifamilia, ilifikia hatua alikuwa akiwashtukiza majumbani kwao usiku mida ya saa moja/mbili kwenda KUWASULUHISHA UGOMVI WA NDOA (Mke Na Mume).

Tafakari Waziri anakwenda nyumbani kwa mwanajeshi mwenye V 2 au 3 mida ya saa moja au mbili usiku, kusuluhisha ugomvi wa kifamilia ili mtu akirudi kazini siku ya pili asiwe na wenge. Huwezi kusikia katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii mambo aliofanya kipindi waziri.

Ila mzee baba akitoa mchango hata wa buku ya kubeti, lazima kesho asubuhi na mapema BREKINI NYUUZZ vyombo vyote vya habari mpaka vyombo vya jikoni. Sasa ole wako usitangaze hio habari, basi TCRA inakuhusu.

Logically Africa,

Huwa kuna tofauti kubwa sana kati ya watu wawili;

1) Mtu alie cheza na kukulia ikulu, akizungukwa na ulinzi mkali na watu wenye vyeo. = Huwa hawana majivuno wala kiburi, kwasababu wamezoea na wanaona mambo ya kawaida (Uhuru Kenyatta, Hussein Mwinyi, Joseph Kabila)

2) Mtu aliekulia katika umasikini na ufukara, akaja akapata utawala kwa kubeti na zali la mentali. = Huwa wana roho mbaya, visasi, chuki (Saddist personality), uongo, ufisadi, majivuno, uzandiki, wanatawaliwa na hofu ya kupoteza madaraka na kuabudiwa. Yani roho mbaya mbaya tu.
 
Naweza kukunga mkono lakini ujue wale jamaa wa vituo vya mafuta kila kilomita moja Dar Chalinze sasa wataweka vivyo hivyo mpaka Dodoma.

GOLO store, Stella Artois, mwanamfalme na Loliondo, sasa ataichukua mpaka Burigi na Meru
Kwanini Nyanda za juu Kusini nao tusiwasikie wale kina mama wenye maumbo wakipewa Wizara nyeti kama Ulinzi itapendeza, huenda tukapumua
😂 😂 😂 😀 🤣
 
Upinzani ni spirit ambayo kamwe haijawahi kuuawa kwa kuwateka wapinzani, kuwatesa, kuwafunga kwa makosa ya kubambikiza etc.

Njia rahisi ya kuua upinzani ni kupitia upendo na kuwaridhisha watu licha ya kwamba hakiwezekani kuwaridhisha watu wote kwa wakati, lakini hili linawezekana akipatikana rais mwenye akili kama Hussein Mwinyi...
Happy new year kamanda bujibuji
 
..nadhani tuachane na fikra za "kuua" upinzani, au demokrasia ya vyama vingi vya siasa....
Kuua upinzani ni kauli za mzee dingi, anawachukia, anawasingizia.

Hivi kama wilaya ya Kisarawe haina maendeleo kabisa, haijawahi kuwa na mwakilishi yeyote wa upinzani, lakini lawama za Kisarawe kukosa maendeleo wanapewa wapinzani, ETI WAMETUCHEREWESHA.

Hivi wakati wenzako wanasoma, hadi wanaongea Kingereza kilichonyooka, wapinzani walikuwa wamekuficha wapi?
 
Upinzani ni spirit ambayo kamwe haijawahi kuuawa kwa kuwateka wapinzani, kuwatesa, kuwafunga kwa makosa ya kubambikiza etc.

Njia rahisi ya kuua upinzani ni kupitia upendo na kuwaridhisha watu licha ya kwamba hakiwezekani kuwaridhisha watu wote kwa wakati, lakini hili linawezekana akipatikana rais mwenye akili kama Hussein Mwinyi....
 
Back
Top Bottom