Uchaguzi 2020 Upinzani hizi dakika za majeruhi naona Dkt. Magufuli anatuumiza sana na hoja ya korona, tujipange kumjibu

Uchaguzi 2020 Upinzani hizi dakika za majeruhi naona Dkt. Magufuli anatuumiza sana na hoja ya korona, tujipange kumjibu

Jomba unajua maana ya slogan ya maendeleo hayana chama..?? It means hata ikijengwa hospital, watakaotumia hawabaguliwi kichama, cuf, act, chadema, nccr, CCM, tadea na wengineo woote watapewa huduma pale..ongeza na mifano mingine hapo, nenda madawa, Barabara, madaraja, ndege, meli, pantoon, sgr, etc

Hizo huduma zote watu wanapata kwa hela zao. Uwe una chama au usiwe na chama, uwe raia au usiwe raia utapata huduma kwenye hiyo miradi vya serikali. Na hili sio kwamba liko hapa Tanzania tu, hata ukienda nchi nyingine, bado utapata huduma kwenye miradi ya serikali za nchi hizo, ili mradi uwe na hela.
 
Magufuli alijifungia kwao Chattle wakati wa korona. Watanzania wakawa wanazikwa usiku. Halafu leo anajifanya ni shujaa sana eti!! Bila aibu... Awadanganye wajinga.

Wala hatutapigana. Watanzania wa kawaida hatuna silaha. CCM ndio ina jeshi. Kama ni lazima watawale watupige tu watuue. Wala hakuna vita. Waliamua watuue kama binadamu anavyoua sisimizi kwa moto. Hakuna kupigana. CCM wamejiandaa kuua watu ambao hawana silaha.
Kupigia kura upinzani ni kuchagua vita
 
Minaona viongozi wetu tukiwa tumebakiza siku hizi chache walizungumzie hili wapigakura wetu ambao ni wengi sana kwa sasa watupigie kura nyingi na Korona isiwe ishu tena. Kwa sababu kilamtu anajua kipindi cha Korona hari ilikuwa tete sana.
unataka wazungumzie nini wakati makamanda walijificha,wakaacha wapiga kura wahangaike na serikali yao
 
Kwa jinsi anavyoipiga kwa sasa kila anapopita ni kama anaiweka kichochezi hivi, kwa sababu hadi sasa ni kweli Korona ipo na Ulaya na marekani hari bado ni tete. Yeye anazungumzia mambo yaliyopita kuwa vingozi wetu walikimbia bungeni mara kujilokudouni hii anatuchafua sana, na kibaya zaidi anasema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani wanasema Korona itaendelea kwa zaidi ya miaka 2 hivyo anasema kama hawa jamaa wakichukuwa nchi chakwanza ni kutufungia ndani watu kwani vingozi wetu walitoa povu sana kuhusu hilo na mpaka leo hawajakanusha au kulitolea ufafanuzi.

Mmechelewa
 
Ukaulize daktari wakati mtaa wenu una makaburi na majirani na ndugu unao? Nafikir hayo ndio inhekuwa kipimo kwamba kule makaburini kuna ongezeko la kiasi gani? Je ndugu wamekufa wangapi? Majirani je? Mfanyakazi mwenzio je?
Na hayo unaweza kufanya utafiti kwa kutumia akili zako tu na siyo lazima Lisu aje akwambia.

Mwanasiasa ujali tumbo lake
 
Kwa kuwa yeye ni kiboko ya korona, Kwanini wasiongee na yule wa Madagascar watengeneze kliniki yao, waponye korona, urais Lissu anatosha!
 
Jomba kwa mfano wewe unaweza tuambia Corona haijakupata mpaka leo umetumia Nini Kama kinga, au ndugu zako wameshakufa wangapi ukilinganisha na wale wanaokufa na kuambukizwa ulaya kila siku..tuambie Ni miujiza gani Tanzania imetokea mpaka hata kampeni zimeendeshwa hivi...Marekani waliandamana tu kwa wiki moja wakakuta maambukizi ya watu zaidi ya 50,000..tuambie Siri iliyo nyuma ya pazia kwa nchi yetu ili tuelewe..pls tell us, msituambie maneno ya hovyohovyo Kama watu waliorukwa na akili..
Kama mgombea wenu ni mponya korona Kwanini asijikite huko kwenye tiba, akasaidie mataifa ambayo mpaka sasa wanateseka?! Mbona hata hiyo ni huduma kwa jamii, atuachie nchi yetu, na wewe uende naye ukambebe mikoba!
 
Huyu chakubanga alitusaidia nini ?
Kakimbilia chato kabisa kajificha kamwachia waziri umy kilakitu muoga kama mama yake.
 
unataka wazungumzie nini wakati makamanda walijificha,wakaacha wapiga kura wahangaike na serikali yao
Serikali ilikua mbali, kabombe! Burigi!! Au hujui waziri aliye chukua mikoba ya waziri wa sheria na katiba, aliapishiwa wapi?!
 
Corona aliiondoa Mungu kwa kupitia jitihada gani jomba au unadhani Mungu anachukua hatua na maamuzi Yeye mwenyewe bila wewe kuonyesha jitihada..hahaha hivi una akili wewe ya imani..usimchukulie poa Mungu wetu..Ni lazima unyenyekee na kuomba..kutwa kucha mnatunga uongo..Nani angewaponya na Hilo gonjwa...lazima uelewe kuna mwanamume wa shoka alisimama na kuongoza wananchi kwa kauli moja nakuwasilisha maombi kwa Mungu na Mungu akajibu maombi..mkae huko mkijua bila Magufuli saiz mngekuwa bado lockdown tangu wabunge wenu walivyokimbia bunge eti kaenda caranteen...pumbaa..afff kabisa
Acha ujuaji wewe na kujifanya unamjua sana kuhusu Mungu, Kuna watu wameanza kupiga maombi kabla ya hata huyo baba yako Magu, Kwa hiyo usituletee ujuaji wako hapa wa kujifanya nyie ndio mlimnyenyekea Mungu, Kwanza baba ako alikimbilia mafichoni huko Burigi akaja kutoka huko akaja na fix...
 
Asijigambe. Watanzania tuliomba Mungu akatuiiimarisha na kuondoa hofu huku wenzetu walifa kika siku hospital na majumbani. Nilipoteza ndugu, jirani na marafiki wengi. Nikisikia mtu anasema Tanzania eti hakuna Corona huwa nasikia tumbo likauma. Mmoja niliyepoteza ni Shangazi yangu aliyenipenda sana. Marafiki ZANGU mmoja akiwa Mkuu wa Taasisi moja tulielewana toka mwaka 2000. Tulidanganywa. Data ya waliougua na kufariki ningependa serikali iweke wazi.
 
Kwa jinsi anavyoipiga kwa sasa kila anapopita ni kama anaiweka kichochezi hivi, kwa sababu hadi sasa ni kweli Korona ipo na Ulaya na marekani hari bado ni tete. Yeye anazungumzia mambo yaliyopita kuwa vingozi wetu walikimbia bungeni mara kujilokudouni hii anatuchafua sana, na kibaya zaidi anasema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani wanasema Korona itaendelea kwa zaidi ya miaka 2 hivyo anasema kama hawa jamaa wakichukuwa nchi chakwanza ni kutufungia ndani watu kwani vingozi wetu walitoa povu sana kuhusu hilo na mpaka leo hawajakanusha au kulitolea ufafanuzi.

Minaona viongozi wetu tukiwa tumebakiza siku hizi chache walizungumzie hili wapigakura wetu ambao ni wengi sana kwa sasa watupigie kura nyingi na Korona isiwe ishu tena. Kwa sababu kilamtu anajua kipindi cha Korona hari ilikuwa tete sana.
Yani badala tujadili uchumi mlioharibu kwa miaka 5, vijana kukosa ajira vibaya akiwa miaka 5, jinsi mlivyowafanya wakulima masikini kwa matamko yenu na makatazo yenu ya hovyo kwa miaka 5. Na jinsi mlivyoua watu, kuteka na kubambika makesi kwa miaka 5 ndo tujadili corona ambayo ni sehemu kubwa ya africa si tanzania tu haijaleta madhara????

Kweli Ccm mmeshikwa pabaya mwaka huu😂😂
 
Kupigia kura upinzani ni kuchagua vita
[emoji16][emoji16][emoji16]

Kwanini ni Vita

1. Kwa sababu itaenda kufukua madudu yote yaliyofanywa kabla???

Ebu tueleweshe iyo Vita itakuaje usisahau na kamfano ka nchi waliochagua upinzani ikatokea vita

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Nasikia kusini hali ni mbaya! Kila mahali ni Tundu Lissu. Wakulima wanahasira haijawahi kutokea, Lindi mtwara na Ruvuma kura za urais ccm wajitahidi kuiba maana ninaimani hazitatosha, na wakifanya ujinga wao kituo kina wapiga kura 400 halafu waliopiga kura 700 patachimbika,wale graduate waliomaliza chuo ndio wasimamizi halafu hawana ajira uwaambie waibe kura moto utawaka.
 
Wafanya biashara mliozoea kuwa mnakwepa Kodi, wizi, madili, utapeli tunaelewa machungu mlionayo Sana..inabidi mumsamehe JPM, maana Hana jinsi..anataka kujenga nchi lakini kwa mapato ya ndani.mapato .yatatoka wapi Sasa Kama sio Mimi na wewe...hatuwez Rudi nyuma kwenye ile enzi ya maisha ya utapeli..ukweli mchungu huu..vumilieni anzisheni kazi halali na mzoee kulipa Kodi..acheni ujinga..maisha ya utapeli mnayoishi mtakuja umbuka..nendeni hata mkapime zabibu dodoma..hayayote uliyoyaandoka ni matokeo ya kuminywa kwa mabiashara yenu ya utapeli na ukwepaji kodi
Jiwe arudi chato atuachie nchi yetu, mtu aliyeshindwa kuongoza hata familia tu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Corona aliiondoa Mungu kwa kupitia jitihada gani jomba au unadhani Mungu anachukua hatua na maamuzi Yeye mwenyewe bila wewe kuonyesha jitihada..hahaha hivi una akili wewe ya imani..usimchukulie poa Mungu wetu..Ni lazima unyenyekee na kuomba..kutwa kucha mnatunga uongo..Nani angewaponya na Hilo gonjwa...lazima uelewe kuna mwanamume wa shoka alisimama na kuongoza wananchi kwa kauli moja nakuwasilisha maombi kwa Mungu na Mungu akajibu maombi..mkae huko mkijua bila Magufuli saiz mngekuwa bado lockdown tangu wabunge wenu walivyokimbia bunge eti kaenda caranteen...pumbaa..afff kabisa
Hivi si ndiye huyu Jiwe alikimbilia chato kwa miezi kadhaa kipindi cha corona?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Watu kibao tunajua ukimwi upo na wala hatuvai kondom. Kutofuata taratibu za kupambana na ugonjwa, hiyo haimaanishi huo ugonjwa umeisha. Mimi ni mwananchi na ninajua serikali wala maombi sio yaliyoondoa huo ugonjwa, bali huo ugonjwa haukuwa na madhara makubwa kwenye ukanda wetu. Mtanzania yoyote anayeamini serikali na maombi ndio yameondoa huo ugonjwa, ni mjinga kama mjinga yoyote. Imeisha hiyo.
Sasa hivi ndio mnasema haukuwa na madhara makubwa ila wakati ule ndio nyie mliokuwa mnasema kuwa hali mbaya watu wanakufa majumbani kimya mkimya sijui serikali inaficha,hata huyo Magufuli akawa anaambiwa kakimbia Dar sababu ya corona. Humu mitandaoni mada za corona zilikuwa haziishi ila et sasa ndio mnasema haukuwa na madhara makubwa.

Kama ugonjwa hauna madhara makubwa kwanini sasa mlikuwa mnatisha watu wakati huo au sasa ndio mmejua kuwa haukuwa na madhara makubwa na ndio maana zile kelele mmeziache tena?
 
Back
Top Bottom