MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
- Thread starter
- #21
Wewe hujui chochote kuhusu Tz ,labda nikusaidie tu upinzani wamevuna walichokipanda hayo ndio yale matunda ya kupinga kila kitu hata kama cha maendeleo sasa watu kama hao wanafaida gani Kwa wananchi wazidi kuwakumbatia ? Haiwezekani ununuzi wa ndege wamepinga , barabara za juu Dar wamepinga, ujenzi wa reli wamepinga, ujenzi wa barabara kumi na ngapi cjui zike wamesema za kazi gani, ujenzi wa bwawa la umeme rufiji wamepinga wamesema tunayo kidatu , kuzuia mchanga wa madini wamepinga, kubadilisha mikataba ya madini wamepinga , yani hamna hata moja walilokubali sasa watu kama hao kuna haja gani ya kuwarudisha bungeni na Kwa manufaa ya nani ? Watanzania sio wajinga ukituzingua tunakuzingua ndio kanuni iliyotumika, sasa kama ulitaka watu warudi bungeni kwasababu tu ulizoea kuwaona nikukumbushe huu uchaguzi Kwa maslahi ya TZ na sio Kenya .
Wewe huwa nakupuuza maana huwa hauna jipya zaidi ya haya mapambio ambayo huwa mumekaririshwa hapo Lumumba, hizi insha zako huwa sizisomi, ukiwa mtu mwenye akili timamu lazima moyo wako utakusuta kwa hicho mlichokifanya huko.
Mimi binafsi ni aina ya mtu ambaye mnaweza mkaniita mataga wa Kikenya maana huwa naunga mikono juhudi za serikali yetu hapa kenya na kuegemea sana upande wake, ila ninaweza nikachukia hadi kuzimu siku serikali yetu itakuja kufanya hicho mlichokifanya huko, upinzani huwa unahoji sio kupinga, nyie hapo mkihojiwa mnaona kama kwamba mnapingwa. Haipaswi serikali iachiwe neno "ndio" kwenye kila ikifanyacho, kwa namna hiyo mtaliwa hadi mifupa.
Upinzani ulihoji tija ya ununuzi wa mindege kwa pesa taslimu ilhali nchi inateseka kwa ukata, hamzingatii vipau mbele wakati wa kuidhinisha chochote, na pia hamkufuata taratibu zipasavyo kikatiba, kwenye miradi yote hiyo, mumeifanya kibabe babe bila kufuata kanuni, sasa upinzani gani utabaki kimya bila kutolea neno, na wakisema mnawashutumu kwamba wanapinga. Halafu vyombo vyenu vya habari ndio vilishafukiwa kitambo, havina usemi wowote.
Kwa sasa hautaona kama kosa maana akili zako zimeshikiliwa na buku saba unazopewa hapo, ila ndugu zako wasiokua na hiyo bahati watateseka sana.
Kunao wafuasi wa CCM kindaki ndaki ila ni wazalendo, hawajapendezwa na huko kusindika sindika mlikofanya, palikua na umuhimu muachie nafasi ya wapinzani hususan mliposindika na kuhakikisha rais amepita, mngeanza kuachia achia kura za baadhi ya wapinzani haswa wanaofahamika vichwa bungeni.