Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu.

Kama tume itakataa kuwarudisha wagombea ubunge zaidi ya 150 wa upinzani hususani ACT na CHADEMA waliowaengua kwa sababu moja ama nyingine basi upinzani ukubali tu kuwa kujitoa kushiriki uchaguzi ndiyo njia pekee sahihi na muafaka.

Mpaka sasa kwa mujibu wa Zitto Kabwe wagombea ubunge wa chama hicho zaidi ya majimbo 45 Tanzania bara na Zanzibar wameenguliwa. CHADEMA mpaka sasa ni karibia majimbo 25 kwa Tanzania Bara sijajua huko Zanzibar na bado uenguaji unaendelea. Na hapo kuna wagombea pia wa CUF, NCCR wameenguliwa, ukijumlisha unapata idadi ya wagombea wasiopungua 150 kwa vyama vyote vya upinzani nchi hii.

Hapo bado sijazungumzia udiwani, majimbo ambayo wagombea ubunge wa upinzani wameondolewa kuna wagombea udiwani at least wasiopungua 10 wanaondolewa. Sasa idadi ya madiwani ni makumi kwa mamia wanaondolewa.

Je upinzani bado unaamini una haja ya kuendelea kushiriki uchaguzi huu? Je upinzani utaendelea kujilisha upepo mpaka lini?

Upinzani kuendelea kushiriki uchaguzi huu ni kujiaibisha wenyewe. Sisi sote ni watu wazima na wenye uelewa. Hatutakiwi kujidanganya, kujipa matumaini hewa na kujilisha upepo. Kusema eti watanzania watakubali kuandamana kupinga udhalimu huu ni uongo, watanzania ni waoga sana, hivyo mwitikio mdogo wa hayo maandamano utapelekea hao wachache watakaoitikia kuumia na hiyo itawavunja moyo na kuendelea kuwaogopesha wengi.

NI ATHARI ZA KUENDELEA KUSHIRIKI HUU UCHAGUZI?

Ni kuwasindikiza CCM, kuendelea kubariki uhuni wanaoufanya, kuendelea kushiriki dhuluma yao na najisi kwa umma.

Kushiriki huu uchaguzi na wakati unajua mwenzako ana majimbo 25 Zanzibar na 30 bara ambayo amejitwalia mezani. Halafu unaenda kugombania majimbo 200 ambayo pia uhakika wa kutangazwa hauna ni kujidanganya big time.

Ishu isiwe Lissu tu, hapo ndipo tunapodanganywa tunang'ang'ana na Lissu huku wenzetu wanajizolea ubunge na udiwani wa dezo mpaka ikifika siku ya uchaguzi na huyo Lissu naye wanamuibia kura tunabaki na kitu gani?

Tujitoe mapema sana kabla hatujafika hata mwisho mwa kampeni. Najua watasema tunamwachia fisi bucha ni heri tuonekane tulimwachia fisi bucha kuliko tukaonekana tulishiriki pamoja na fisi kula nyama buchani kumbe tuliambulia mifupa michache tu.

Magufuli anataka kuthibitisha ile kauli yake kwamba ameufuta upinzani na hapo anajiona mjanja sana maana aliteua wana ccm kwenye ukurugenzi makusudi na matokeo yake yanaonekana sasa hivi. Sasa sisi tusiwe sehemu ya kumsindikiza Magufuli kwenye hiyo project yake.

Narudia tena utakuwa uzalendo na ushujaa kususia uchaguzi huu kuliko kujidanganya na kujilisha upepo kuwa tutashinda pamoja na mwenendo mzima unavyoonekana katika hizi hatua za mwanzo.
 
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu.
Wazo lenye afya sana ni vyema kuwasusia tupate na katiba mpya kuwepo na serikali ya shirikisho. Bila kufanyiana vitimbwi hakuna kitakachowaogopesha wenye mamlaka
 
Vyama vikuu vingeungana na kuhamasisha ya kudai tume huru ya uchaguzi, this is the right time kufanya hivyo wasusie uchaguzi na wadai tume huru basi. Watu wengi watawaunga mkono hata mimi nitaunga mkono na huo utakuwa mwisho wa udhalimu huu. Hakika JK na Ben walitukosea sana sisi Watz.
 
Naunga mkono hoja , wawahamasishe wananchi mass kudai uchaguzi huru na haki , pia kudai matokeo halali sio ya kupika wananchi nguvu ya umma huwa haishindwi na utawala dhalimu wa aina yoyote ile , umma ujue wao ndio wenye mamlaka yote sio yoyote yule na wayadai waache woga hutu litaiangamiza hii nchi .
 
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu...

Hapana, wapinzani mkijitoa mtaonyesha kutokomaa kisiasa.

Kumbuka uchaguzi wa mwaka huu si wa kwanza kwenu.

Mkubali mmekosea kwa kuweka jitihada na nguvu zenu zoote kwa Tundu Lissu.

Ningekuwa mimi ndo Mbowe ningeshughulikia wagombea wote kabla ya kurudisha fomu na Lissu angeendelea tu na shughuli zake anazofanya sasa hivi.

Pia mkijitoa mnaonyesha kweli mna kitu kingine na hila zilizojificha.
 
Mm pia nimestuka. Tusubiri uchaguzi uishe wakiiba kura, tukinukishe Ila si kujitoA.

Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipoapishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?
 
Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipopishwa Novemba 2015.
Kwa hili uko sahihi kabisa, maandalizi ya uchaguzi mwingine mpya huanza rasmi baada ya kumalizika uchaguzi uliopo kwa wakati huo.

Ila kumbuka toka mwaka 2015 walizuiliwa kufanya shughuli za kisiasa hasa kukuza na kuimarisha vyama vyao kupitia mikutano ya hadhara kwa kisingizio kwamba "muda wa siasa umekwisha sasa ni muda wa kunyoosha nchi" ila chama tawala (Ccm) wao hawakuhusika na hilo katazo hivyo waliendelea kufanya siasa kwa miaka yote mitano mfululizo.
 
Wewe jamaa ni mnafiki sana unaongea kama ni mgeni kutoka Toronto hujui kwamba upinzani ulikatazwa kufanya siasa kwa miaka mitano? Unaongea kama vile hujui kwamba walipothubutu kuongea tu kesi za uchochezi ziliwahusu? Eti wakimya sana daaa!
Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipopishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?
 
Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipopishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?
Wanafiki utawajua tu .
 
Back
Top Bottom