Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipoapishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?
Uyo jamaa yako baada ya kuapishwa si mdip alipiga marufuku vikao vya siasa mpaka vya ndan ya chama au mnajosahaulisha
 
Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipoapishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?

Haya uliyosema nimecheka kwa nguvu, nimewahi kukuambia kuwa CCM sio chama cha kizazi hiki bali cha kizazi kilichopita. Sio kwamba haijafanya kitu, bali hiki sio kizazi chake.

Ndio maana umeona kimeteka vyombo vyote vya habari, kimefanya kile kilichoamini kitaipa mvuto na kuua upinzani, lakini wiki tatu za Lisu kuzunguka mikoa kadhaa kumeifanya CCM kujua wakati hauko upande wao. Sasa ile nguvu halisi ya ccm ambayo ni vyombo vya dola iko wazi peupe. Wakati ni ukuta kaka. Ni aidha CCM ikubali kiungwana kukaa pembeni, au ikae madarakani kwa shuruti bila ridhaa ya umma.
 
Uyo jamaa yako baada ya kuapishwa si mdip alipiga marufuku vikao vya siasa mpaka vya ndan ya chama au mnajosahaulisha


Nafikiri mngechukua njia ingine ya kumshauri na kupunguza yale mlokuwa mwazungumza dhidi yake majukwaani nina imani kungekuwa na suluhu.

Ndo maana akaamua kama hali itakuwa hivyo basi hakuna siasa.

Na alisema kabisa kwamba chini ya utawala wake asingependa kuona watu wanaingilia juhudi zake.

Wapinzani mkubali mmekosa mbinu nzuri ambazo twaita kwa kiingereza Constructive ideas and strategies.

Hizi zinajenga na sio kubomoa urafiki na maridhiano.

Nasisitiza, haya ni maoni yangu.
 
Mleta Mada.,,,Naomba nipe jibu !.. Unadhani CCM hawakujipanga dhidi ya hilo?.. unapozungumzia Upinzani kwa sasa unazungumzia CHADEMA NA ACT,,,na ukifatilia ndo wanao minywa na kubanwa,( nahisi wanogopwa) , hivyo vyama vingine kama Tadea,,,TLP, CUF, SAU,,na vingine Havitajitoa na bado uchaguzi utafanyika na vitapewa majimbo ili tu kuhararisha... WAPINZANI WA KWELI MJUE SIO RAHISI KUINGIA IKULU HASA KWA NCHI ZA KIAFRIKA ,,,,HAKI HAIOMBWA,,HAISUSIWI,WALA KUSUBIRIWA, HAKI INADAIWA ,HAKI INATAFUTWA..,... KUWENI IMARA MACHO YA DUNIA YAPO NYUMA YENU
 
Haya uliyosema nimecheka kwa nguvu, nimewahi kukuambia kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki bali cha kizazi kilichopita. Sio kwamba haijafanya kitu, bali hiki sio kizazi chake. Ndio maana umeona kimeteka vyombo vyote vya habari, kimefanya kile kilichoamini kitaipa mvuto na kuua upinzani, lakini wiki tatu za Lisu kuzunguka mikoa kadhaa kumeifanya ccm kujua wakati hauko upande wao. Sasa ile nguvu halisi ya ccm ambayo ni vyombo vya dola iko wazi peupe. Wakati ni ukuta kaka. Ni aidha ccm ikubali kiungwana kukaa pembeni, au ikae madarakani kwa shuruti bila ridhaa ya umma.

Ukisema si kizazi chake wakosea.

Kwani vyama vya siasa ambavyo si vya kizazi cha sasa ni kwa Afrika tu?

Mbona hata huko Marekani mpaka sasa wanachagua wale wazee ambao sasa ni over 70?

So, hawa ndo wako right kwamba kizazi cha sasa cha Marekani kinawafaa hawa mababu?

What are trying to say my friend?
 
Nafikiri mngechukua njia inigne ya kumshauri na kupunguza yale mlokuwa mwazungumza dhidi yake majukwaani nina imani kungekuwa na suluhu.

Ndo maana akaamua kama hali itakuwa hivyo basi hakuna siasa.

Na alisema kabisa kwamba chini ya utawala wake asingependa kuona watu wanaingilia juhudi zake.

Wapinzani mkubali mmekosa mbinu nzuri ambazo twaita kwa kiingereza Constructive ideas and strategies.

Hizi zinajenga na sio kubomoa urafiki na maridhiano.

Nasisitiza, haya ni maoni yangu.
NENDA kokote Duniani ,WAPINZANI WA kisiasa wowote wale wanajipanga kuchukua dola,,kwa kuangalia Madhaifu ya mtawala na kuwambia Umma,,ambao ndo una legitimacy ya kuwapa dola, kazi ya kushauri na kuisimamia Serikali hapa kwetu Inafanywa na Bunge,,ila kama wewe unamacho na masikio, utakua umeona na umesikia,Jinsi Serikali ilivyo Lisimamia bunge na kulitawala,,(ukaitwa muhimili uliojichimbia zaidi)... ukinijibu nijibu kwa hoja
 
Ukisema si kizazi chake wakosea.

Kwani vyama vya siasa ambavyo si vya kizazi cha sasa ni kwa Afrika tu?

Mbona hata huko Marekani mpaka sasa wanachagua wale wazee ambao sasa ni over 70?

So, hawa ndo wako right kwamba kizazi cha sasa cha Marekani kinawafaa hawa mababu?

What are trying to say my friend?

Huko US watu wanachaguliwa kwa ridhaa ya umma na sio mabavu. Nitajie kwenye hao viongozi kama kuna aliyepita bila kupingwa. Chama kilichoko madarakani ni republican, kiko madarakani sasa kwa miaka 40+ mfululizo? Tume ya uchaguzi inapokea maagizo toka kwa Trump ili aibebe na chama chake? Umeona vyombo vya dola vikiwa sehemu ya republican? Ulikotolea mfano ni kama usingizi na kifo.
 
Kujitoa mpige kimya, ni faida kwa CCM.

Wakijitoa wahakikishe wanalazimisha Maandamo ya Amani ya kudai haki.

CCM na watu wake kwasasa wanaelewa Lugha moja tu...NGUVU YA MATENDO.
Surgeon Hongera Kwa Majukumu!!

Onyesha Ungwana kwa kutupa REPORT ya Post Op Ya Mgonjwa Mana Jana ulituaga Ile saa 6 kuwa u really need a sleep prior to the Op..
 
Lord Diplock MR,

Hivi Chadema kwa Mfano ina Mwenyekiti?

Nilikua kila siku nasema Mbowe ni CCM aliyepo Chadema kwa manufaa yake kibiashara.
Nikawa nashambuliwa kwa maneno makali.

Mbowe amekwapua pesa zote za Ruzuku kwa miaka mitano na kufanya mambo ya hovyo na kujikuta akikiingizia Chama hasara kwa makesi ya ajabu ajabu.

Muda wote hapakuwa na kesi yoyote ya kikatiba dhidi ya matukio ya wazi yaliyokuwa yakifanyika.

Mfano Kuna Mkubwa mmoja wa Polisi alijitokeza wazi kufanya siasa kinyume na katiba ya nchi.

Hatukuona Chama chochote kikitumia ruzuku yake kufungua kesi ya kikatiba kwa hilo juu ya huyo kiongozi.

Miaka yote watu wanapita bila kupingwa na hawapigiwi kura lakini hakuna Chama kilichohoji mahakamani uhalali wa Mbunge wa jimbo kuwawakilisha wananchi bila Kupigiwa kura kinyume na katiba matokeo yake ni kukua kwa hilo joka kuu la kupita bila kupingwa?
Sasa imekua ni kubaki kulalamika tuu kama wanafunzi wa form two.

Miaka mitano bila mikutano ya kisiasa tulitegemea Chama kiwe na fedha za kutosha.

Bila pesa nani atawaunga mkono kwenye mapambano dhidi ya udhalimu. Hata wakati wa kudai Uhuru palikua na matajiri waliodhamini mpambano ule kwa kuchanga pesa.

Nani atakua tayari kufungwa au kuuawa au kujeruhiwa na kuiacha familia yake ikiteseka kwa sababu eti Wapinzani wamekosa ubunge ambao wanufaika wa kwanza ni wao na familia zao.

Hamuwezi kunielewa mana mmeshupaza shingo kama CCM walivyoshupaza japo wao wana nguvu ya dola nyuma yao na kiburi kimewajaa huko wapinzani wakijawa na woga na ubinafsi ulioongozwa na Mbowe kwa miaka 5 na sasa matokeo yake ni kukosekana kwa mikakati insyotekelezeka kwa Chadema. ACT wao bado ni wachanga kifedha.

Kwa sasa Kila Mkurugenzi na msimamizi wa Tume anajitafutia namna ya kupiga pesa toka kwa Wagombea wenye pesa wa CCM ili awaengue wapinzani na mgombea wa CCM apite kirahisi sana. Ni Mradi mzuri sana kwa mwaka huu kuliko miaka yote.

Wakurugenzi wanaosimamia haki wapo kwenye sintofahama kama wanamfurahisha Bashiru na Polepole au laa. Wale wanaowaengua wapinzani ni wazi kuwa wanawafurahisha sana na kuonekana kuwa wanakipigania Chama. Baada ya uchaguzi watapandishwa vyeo na kufurahia udhalimu wao huku familia zao zikiishi kwa raha na furaha na maisha bora na wale waliotenda haki watatolewa na kuishi kwa tabu kwa sababu ya kusimamia haki.

Kama hamuwezi kupambana nao basi unganeni nao tu mule bata.

Kama tungekua na viongozi wa Upinzani waadilifu kabisa kama alivyo Tundu Lisu basi wananchi wangeingiwa na roho za kijasiri kwa uwezo wa Mungu wa haki na kila mtu dhalimu asingepewa nafasi hata dakika moja ya kufurahia udhalimu wake kwa namna yoyote.

Mtu anafanya mambo ya kuhatarisha amani ya nchi kwa makusudi kabisa tena kwa rushwa ya fedha na cheo halafu anawaita polisi ili watumie nguvu kuwadhuru wenye haki yao na yeye anarudi nyumbani kwake kwa furaha na Kitita cha Pesa na kupongezwa na familia kuona kumbe kutumikia matakwa ya CCM inalipa sana.

Nani atawatendea haki wapinzani kwa hali hiyo?

Eti mnataka kujitoa kwenye uchaguzi kabla ya kuwatoa waliovuruga uchaguzi kwa tamaa zao za kutaka vyeo na fedha!!
Jambazi hata akiwa rafiki yako hua hafai kuachwa mana siku ya kutenda ujambazi akikukuta kwenye tukio hakuachi ,unakua wa kwanza kuuawa.

Kuwaacha salama madhalimu ni kuzidisha kizazi cha madhalimu. Kama wahuni walipewa 20000 ili washambulie mkutano wa Chadema inakuaje MTU akipewa million 100 dhidi ya dhalimu.

Bora mjitoe tu watu waendelee na shughuli zao.

Mana huu woga wa CCM iliyofanya makubwa hatuelewi unatokana na nini?

Bila shaka ni nia ya dhati ya kuondoa upinzani wa kivyama yaani upinzani usiwepo Bali ubaki ni watu wanajipendekeza kwenye Chama kimoja.

Nchi itarudi utumwani na huenda hata nchi ikatawaliwa kifalme na ukabila ukawa mkubwa sana.
 
Wapinzani lengo lenu kuu ni kuleta vurugu na si kushiriki uchaguzi.

Kama mngetaka kushiriki uchaguzi mngajipanga upya tangu raisi John Magufuli alipoapishwa Novemba 2015.

Lakini leo hii hata Mbowe anatoa ujumbe kwa manati kupitia mitandao na hata John Mnyika ni mkimya sana.

Hivi kuna nini?
Kosa kubwa walilofanya Chadema ni kumrudisha Mbowe madarakani.

Mbowe ni pandikizi la makundi ndani ya CCM.

Mbowe yupo Chadema kwa maslahi yake kwanza ukimtoa kwenye uenyekiti kesho anarudi CCM ?
Yupo kimya kabisa
 
Upinzani wanashiriki kuonyesha dunia ukweli. Magufuli na CCM wataaibika dunia nzima. Watakuwa kama Maduro wa Venezuela. Magufuli hataweza ongea mbele ya dunia ba kuheshimika. Huu ndo mipango ya Lissu.

Hana nia ya kushinda, yeye ni kupinga siku zote kama CCM wanavyosema.

Sent from my SM-G935W8 using JamiiForums mobile app
 
Siungi mkono wapinzani kujitoa bali washiriki kampeni, na kuzitumia kampeni hizo kuamsha ari ya watu kugomea dhuluma.

Mikutano ya kampeni itumike kuwaandaa watu kwaajili kuitumia nguvu ya umma kudai katiba mpya, tume mpya ya uchaguzi, kudai utawala wa sheria na kupinga udikteta.

Kampeni za mwaka huu zitumike kuanika uovu wa utawala huu, na kuuunganisha umma dhidi ya udikteta, upendeleo na uonevu.

Kampeni za mwaka huu zitumike kusafisha siasa chafu zilizodumu kwa miaka 5 za kuwadanganya watu kuwa utawala wa awamu hii umefanya mambo makubwa sana kuliko awamu zote ziluzopita, wakati ukweli ni kuwa awamu hii, katika kila sekta imepata ufanisi mdogo zaidi kuliko awamu zilizotangulia:

1) barabara za lami zilizojengwa hazifikii hata 25% ya zile zilizojengwa wakati wa awamu ya 4

2) Ujenzi wa miundombinu ya afya, katika thamani, awamu hii haijafikia hata 40% ya awamu iliyopita

3) Kwenye sekta ya kilimo, awamu hii imeshindwa kabisa kiasi cha kuangusha mapato ya sekta hii kwa 50%

4) Mapato yatokanayo na mauzo ya mazao ya uvuvi yameanguka kwa zaidi ya 50%

5) Ukuaji wa uwekezaji umeanguka kwa zaidi ya 75%

6) Ukuaji wa sekta ya utalii umeanguka kwa zadi ya 60%

7) Ujenzi wa demokrasia umekuwa na negative growth ambapo utawala huu umeanzisha sheria za hovyo, sheria za kidikteta zinazowazuia watu kuhoji chochote

8) Utawala huu umekuwa ukiongoza bila kufuata katiba na sheria nyingi za nchi

9) Utawala huu unaendesha mambo yake kwa ubaguzi kwa kuwabagua watu kwa msingi ya kanda, kabila na dini

10) Utawala wa awamu hii umekuwa ukiua mihimili ya Taifa, na kutoweka mipaka ya mihimili mikuu ya nchi kwa kufanya mbinu ya kuwapindikiza watu wa serikali kwenye kila muhimili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, wapinzani mkijitoa mtaonyesha kutokomaa kisiasa.

Kumbuka uchaguzi wa mwaka huu si wa kwanza kwenu.

Mkubali mmekosea kwa kuweka jitihada na nguvu zenu zoote kwa Tundu Lissu.

Ningekuwa mimi ndo Mbowe ningeshughulikia wagombea wote kabla ya kurudisha fomu na Lissu angeendelea tu na shughuli zake anazofanya sasa hivi.

Pia mkijitoa mnaonyesha kweli mna kitu kingine na hila zilizojificha.
Watakayemuonyesha kuwa wana hila zilizojificha ni nani. CCM au wananchi!? So far wenye hila zilizojificha ni CCM na NEC. Mchezo wanaokufa ya kwa sasa bora Mseveni na Uganda yake.
 
Lord Diplock MR,

Ujinga ndio tatizo,walishaambiwa tokea mwanzo kuwa itakuwa maajabu ya Musa CCM kubariki vyama vya upinzani, bila kufanya mabadiliko ya msingi katika sheria za kuleta haki sawa kwa vyama vyote .Pia haki ya mtu binafsi kugombea nafasi hizo bila kupitia chama cha kisiasa.

Wakapata kihindi kihindi kufikiri yatanyooka tu bila initiative, kisa ruzuku,wakafikiri wamepata kumbe wamepatikana,na hizo kelele zinakuja siku za uchaguzi.
 
Upinzani tulionao hawawezi kujitoa maana nao wanapigania vyeo si mabadiliko. Wako tayari kushiriki uchaguzi wanaouita uchafuzi, batili na haramu ilimradi waambulie ubunge na kura za urais za kuongezea ruzuku za vyama vyao. Wanagombea maslahi yao si maslahi ya umma!

Mara kadhaa nimewahi kushauri tupiganie tume huru kwanza, katiba mpya kwanza, wagombea huru kwanza na mifumo mingine mipya kwanza ndiposa tuingie kwenye uchaguzi, lakini wapi. Bila uwanja sawa wa kisiasa, bila kuwa na refa (tume huru) asiyeegemea upande wowote ni kushiriki kwa hiari uchafuzi, ubatili na uharamu. Wasilalamike!

Kenya na Malawi walimwengua rais aliyepitishwa na tume za upendeleo kwasababu walibadili mifumo ya uchaguzi na kuruhusu matokeo kuhojiwa mahakamani. Lakini wapinzani wetu wanataka vyeo kwanza na marupurupu yake!

Nawaomba baada ya uchaguzi wakae kimya, wasilalamikie dosari zozote maana wamekubali kushiriki uchaguzi chini ya tume na mifumo mingine wanayodai batili na haramu. Ukikubali kushiriki kula chakula unachojua kina sumu na haramu, usilalamike utakapoanza kuharisha!

Lord Diplock MR
 
Umenena ukweli mtupu, huko ndio kupigania mabadiliko ya kweli si vyeo - udiwani, ubunge na urais
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu.

Kama tume itakataa kuwarudisha wagombea ubunge zaidi ya 150 wa upinzani hususani ACT na CHADEMA waliowaengua kwa sababu moja ama nyingine basi upinzani ukubali tu kuwa kujitoa kushiriki uchaguzi ndiyo njia pekee sahihi na muafaka.
 
Back
Top Bottom