Vangigula
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 852
- 2,739
Moja ya makundi yaliyojeruhiwa kimaslahi kwa hii miaka 5 iliyopita ni kundi la Wafanyakazi wa Umma. Bila ongezeko la mshahara, ambalo lilikuwepo kisheria, kila mfanyakazi wa umma amejikuta akipoteza maslahi ya kutosha.
Kwa mfano binafsi, mwaka 2015 nilikuwa nina annual increment ya shilingi 120,000. Bila kujali kama ningepanda notch au madaraja, kila mwaka nimekuwa nikipoteza (nachelea kutumia maneno kama kupunjwa au kuibiwa) shilingi 120,000 x 12 ambazo ni sawa na shilingi 1,440,000 kwa mwaka na shilingi 7,200,000 kwa miaka mitano.
Na kwa vile hata kwenye budget ya sasa hakuna ongezeko, ina maana ninaweza poteza 14m kwa hii awamu. Na hili litakuwa na cascading effect mpaka kwenye mafao ya kiinua mgongo changu.
CHADEMA, kama mtakuja na ahadi ya kuwarejeshea watumishi wa umma kile walichopoteza, hebu fikirieni ni kura ngapi mtazivuna?