Upinzani kwa Tanzania ni kazi ngumu na ya hatari


..dhana ya wapinzani na watawala ni dhana potofu.

..tunachotakiwa kufanya ni kuunda vyama vya siasa ambavyo vitafanya shughuli zake ktk mazingira ya haki na usawa.

..hapa Tz kuna chama kinachoamini kwamba kina haki ya kutawala daima milele, huku vyama vingine vikiwa wasindikizaji na wapinzani.

..kwenye nchi za wenzetu, wanaofanya siasa za haki, chama tawala, na upinzani, hubadilika mara kwa mara. Wakati mwingine vyama huungana kuunda serikali ya mseto
 
TZ hakuna wapinzani, wote wamewekwa na TISS ili kutekeleza matakwa ya wenye dunia kwenye demokrasia, tuendelee kupata mikopo na misaada yao! Kibaraka namba moja wa CCM kwenye upinzani ni Mbowe, inashangaza jinsi gani wafuasi wake wanatoa mapovu humu, siku wakijua ukweli watashangaa! Wameoneshwa signs ila bado ni vipofu
 
Acha kujidanganya, tatizo ni CCM wale wezi wa kura madkteta uchwara
 
Mbona mbowe yeye aliweza kwa kumtumia Mallya tu???¿¿¿
Ina maana serikali ya CCM ni ya kijinga kiasi kuwa wewe mpuuzi ukagundua yenyewe ikashindwa kulibaini hilo?
Kuficha upumbavu na kuonyesha hekima ni jambo jema. Fanya hivyo
 
Ina maana serikali ya CCM ni ya kijinga kiasi kuwa wewe mpuuzi ukagundua yenyewe ikashindwa kulibaini hilo?
Kuficha upumbavu na kuonyesha hekima ni jambo jema. Fanya hivyo
Kuna swali limeulizwa Mallya yupo wapi! Naweka kambi kusubiri majibu.
===
Nyumba yenu ya vioo mjue, hivyo acheni kuchezea mawe.
 
Kweli tupu
 
Wa kulaumiwa ni Nyerere. Yeye kabla ya nchi kupata uhuru alikataa upinzani. Alitaka asisumbuliwe akijenga ujamaa wake. Na mpaka leo CCM wanafata fikra za Nyerere kuwaona wapinzani kama maadui.
Huo ni woga na Ubinafsi, Nyerere alikuwa mchapa kazi mzuri Ila kwenye Engle Demokrasia na uchumi vilimsumbua sana Kama si kumshinda , CCM Imekuwa mwoga sana wa Upinzani wa kweli ,wapo tayari kutengeneza hata Upinzani fake ( vyama vyao) ili mladi tu ku gilibu umma.

Lakini kamataifa Ni hasara sana kuzuia fikra mbadala zinazo weza kulisongesha mbali zaidi na kung'ng'ana na utawala na watawala walewale Koo zilezile.

Tubadili fikra Kama taifa
 
Nakupata mkuu, kuunda serikali ya mseto inaleta maana na tafsiri kwamba vyama vyote vipo kwaajiri ya kulisaidia taifa kizalendo .

Pili Vyama vyote hujioendekeza kwa wananchi kubuni sera na mipango mizuri kwa kushindana huku ikiwa ni faidakwa wananchi na taifa kwa ujumla.
 
Tusiogope Wala kujikoroga , wananchi wanapaswa kupambania kile wanacho kiamini ,ni kma maji ya mafuriko ,siku moja ccm itapisha maji yapite!
 
..Mbowe angekuwa amehusika na kifo cha Chacha Wangwe angekamatwa na Polisi wa CCM na hivi tunavyozungumza angekuwa ameshahukumiwa kifo na mahakama za CCM.
Dereva wa Chacha Wangwe alihukumiwa kifungo lakini haraka sana akapewa msamaha wa Rais !
 
Tusiogope Wala kukikoroga , wananchi wanapaswa kupambania kile wanacho kiamini ,ni kma maji ya mafuriko ,siku moja ccm itapisha maji yapite!
Ni kweli Mkuu, ila hawa wapinzani tulionao ni majanga matupu, ndiyo maana maana Magu aliamua kuwatosa, wanafiki
 
Ni kweli Mkuu, ila hawa wapinzani tulionao ni majanga matupu, ndiyo maana maana Magu aliamua kuwatosa, wanafiki
Chaguzi zinakuja hizi tuzitumie vema kuchambua mabua na nafaka halisi kwenye vyama vyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…