Clever505
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 1,183
- 2,256
Mimi ni Mwananchi niishie Dodoma katika walaya ya Mpwapwa, nakaa kijijini naweza kupaita porini kabisa. Tumeishi miaka yote bila huduma muhimu kama maji na umeme ambapo maji tumekuwa tukiyapata mbali visimani.
Tangu aingie madarakani JPM ameweza kusimamia vizuri ambapo umeme pamoja na maji vipo kwa uhakika. Na huku kwetu hamna kabisa habari za upinzani, sasa najiuliza ina maana wapinzani hawaoni kwamba na huku wanahitajika kufika kuongea na wananchi? Huku kila kitu ni CCM. Mfano kuna ofisi ya kijiji ambayo kwa mapenzi ya wananchi juu ya CCM haiitwi ofisi ya kijiji wanaiita ya CCM, huku viongozi wa CCM wanapita tu bila upinzani.
Tundu Lissu huku hawamjui kabisa, ni sisi tu wachache tulio mitandaoni ndio tunaona akizungumziwa, wapinzani mnakosea sana kudili na watu wa mjini tu mnasahau kwamba mnapaswa kuingia kila kona ya nchi. Nashangaa sana ninapoona kuna watu wanaamini CCM itatoka madarakani mpo serious kweli?
Mnatukanana tu mitandaoni kwa mambo yaliyowazi tu, hivi ni Tanzania hiihii ninayoijua mimi wapinzani waitoe madarakani CCM? Mkitaka kuishinda CCM hangaikieni kwanza ngazi zote kuanzia viongozi wa vijiji.
Wanakijiji kwa kijiji chetu wanajua kwamba bila Magufuli hadi leo tusingekuwa na umeme wala maji, mnafikiri watu hawa watamchagua mwingine zaidi ya Magufuli? Hivi nyie watu wa mjini mnahisi nyie huko peke yenu mnatosha kumuondoa Magufuli? Washaurini viongozi wa upinzani wajikite na vijijini pia maana hawajulikani huku.
Upinzani kuitoa CCM madarakani sio kazi rahisi kama mnavyofikiria, endeleeni kufarijiana tu kwamba 2020 Magufuli anang'oka madarakani huku mnasahau kwamba kuna maeneo mengi yana watu wa CCM pekee.
Kuna mambo mengi sana ya ovyo yanafanywa na CCM kwa mfano nasikia kuna watu wanaenguliwa tu na kisha wanamuacha mgombea mmoja tu wa CCM, hii kiukweli inatia hasira lakini hayo mambo ni wachache sana huku vijijini ambao wanaweza kujua kwamba ni hujuma zinafanywa na ccm...kwa mfano kwenye jimbo letu mpwapwa mgombea ubunge ni mmoja tu wa CCM mnafikiri nyie upinzani nani atampigia kura Tundu?
Waambieni viongozi wa upinzani kwenye kampeni wazunguke na vijijini vinginevyo urais mtausikia tu na kuhisi mnaibiwa kura kumbe mna wapiga kura wachache.