Upinzani mkumbuke kwamba ninyi ndio mnaojitoa sadaka kwa ajili ya taifa hili na si CCM. Go on please

Upinzani mkumbuke kwamba ninyi ndio mnaojitoa sadaka kwa ajili ya taifa hili na si CCM. Go on please

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Wasalaam wajumbe!

Ninawaomba sana upinzani katika nchi hii utambue kua mabadiliko ya mifumo ya kiutawala iliyojaa uonevu na ukoloni hayatafanywa na CCM. Hiki chama kilichobakisha sasa ni kugawana vyeo na kurithishana. Bila ya upinzani madhubuti CCM hakiwezi kutoka madarakani leo.

Bila ya upinzani kujitoa sadaka msitegemee kama kutakua na jipya ndani ya CCM. Ukumbuke kwamba unapojitoa sadaka hupaswi kufikiria watoto wako wala mkeo, hupaswi kufikiria magari wala majumba au mashamba yako.

Fikiria zaidi watanzania wanaopoteza maisha kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa,fikilia watanzania wanaotembea na kupotezwa kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa, fikiria kinamama wanaopoteza maisha mahospitalini kwa kukosa huduma nzuri za afya.

Mnapopanga chochote ambacho ni kinyume na na serikali ya CCM msifikirie kua Polisi wataacha. Mnatakiwa hata kujiandaa kisaikolojia kukamatwa ikiwa ni pamoja na kuziaga familia zenu. Hawa Polisi hawafanyi kwa matakwa tajwa yao bali ni maagizo ya CCM ambayo imejaa mwavuli wa serikali kwa sababu kila kiongozi wa serikali ni MwanaCCM.

Mwisho kabisa niwape pole lakini kuamini kua nyuma yenu wapo mamilioni ya watanzania wasiyopendezwa na michezo wanayoifanya CCM.
 
Hili sidhani kama linapaswa kupigiwa chapuo.
Kama wanajitoa sadaka wananchi wataona na watakaa upande wao iwe kwa hei au shari.
Kinachonishangaza ni kuwa viongozi wamekamatwa ila hakuna lolote kutoka kwa wananchi, hapa ndipo viongozi wa upinzani wanapaswa kujiuliza wapi wanakosea.
 
siku mbunge wa CCM akiomba kuongea na wananchi wapinzani waende kwa wingi akianza kuongea ugoro hapohapo wamkatae na maandamano ya kudai haki yaanze.
 
These are trying times for opposition in Tz. Hawa jamaa wanapita kipindi kigumu mnoo na soon tutawajua wapinzani wa kweli. Kwa sasa hamna ruzuku na kwa wao mmoja mmoja hali zitakuwa mbaya na CCM wataanza kumendea hawa waliobakia wenye misimamo. Nawashauri wapinzani esp Chadema warudi kwa wananchi for support.

Hata TAL wanamfuata na kumwambia ona sasa kiko wapi. Soon wapinzani wa maslahi binafsi tutawajua. This is a blessing in disguise.
 
Hakuna mapambano yaliyowahi kua rahisi...



Cc: mahondaw
Mnapambana na nini Makamanda nchi hii ina amani na wananchi anaendelea kufanya kazi.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge NCHI.

URT - JPM
SMZ- Mwinyi

CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom