Upinzani ndani ya CCM waweza kuwa mgumu kuliko vyama vya upinzani

Subiri baadae, ushindani binafsi ktk michakato ya kutafuta the best ni muhimu sana.
 
Fikuria upya serekali hii ni tafauti na ile ya G55 maendeleo kwanza
 
Dar wanahamgaika kujenga shule ubungo huko.
Ingekuwa jimbo la chadema isingejengwa
 
Tukubaliane tu hakuna BUNGE bali pale Dodoma karibu na CBE kuna jengo la bunge na kikundi kilichochaguliwa na Magufuli kukutana pale na kufanya maigizo ya shughuli za Bunge.

Hakuna hata mmoja anayeweza kupinga maagizo ya Magufuli au kuhoji matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na Magufuli.

Yeyote atakayepinga kama hatopotezwa basi atachimbwa kumbukumbu za kodi ya TRA na kisha kutafutiwa kesi uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.
 
Hata hao unaosema walishinda kihalali kumbuka walibebwa na Mwenyekiti kwenye kura za maoni ndani ya Chama..hivyo Bunge zima hakuna wa kusema zaidi ya ndio mzee.
 
Matatizo hayayewezi kutatuliwa na level ile ile iliyoyaunda matatizo hayo - Hayao maneno aliyasema Einstein.

Matatizo/kero za Tanzania yameletwa na CCM, nami namuunga mkono Einstein kuwa CCM haiwezi kutatua matatizo ya watanzania si tu kwa vile hawataki bali level yao ya fikra ni ile ile. Ni lazima uvuke daraja la fikra ili uyatatue matatizo ya wananchi. Mifano michache - Kero za Muungano, Elimu, Ardhi, soko na uzalishaji kwa wakulima na kumalizia na uchaguzi.

Lazima tupate watu wengine wenye mawazo tofauti kabisa ndio wataotatua matatizo ya watanzania. Swali: watawezaje kufika huko hawa wengine ili nao watuongoze?
 
Umenena. Pia ni muhimu tukakumbushana asili ya binadamu, hatuwezi kukaa hata ndugu wawili tukakubaliana kwa kila jambo. Hivyo upinzani/kutofautiana ktk kufikiri na kutenda, kuyaona mambo ni asili ya binadamu.

Kwa upande wa unaoitwa upinzani wa kisiasa kimsingi haupo ktk vyama,rangi za bendera za vyama na majina ya viongozi wa vyama. Upinzani ni maisha..namna watu wanavyotafsiri wanayostahili kuishi, kutendewa na viongozi wao. Bila kujali ni muumini wa chama husika. Hakuna anayepona katika matokeo hasi au chanya ya uwepo wa chama x madarakani.
 
Kumbuka tulikuwa na Bunge la chama kimoja miaka ya nyuma.
 
Hawa wliopo huwezi linganisha na akina njeru kasaka hawa akina msukuma lusinde na yule wa bunda ni takakata kabisa
 
Ni wakati wa wabunge kuwekeza kwa wanachi na sio chama tena. Kwa sasa chama hakina tika sana zaidi ya wananchi. Kuna utamaduni mpya wa SI-HASA unakwenda kuzaliwa hapa...... Muda utasema..... G55, na enzi za SARWAT aliyemtesa mwalimu Nyerere na TANU kule Jimbo la Mbulu zinaweza rejea km wawakilishi wetu watakuwa na akili ya kujiongezea na kuiona picha halisi na matamanio ya wananchi.
 
Nape alisema chama chake huwa na migawanyiko sana ila sio katika wakati wa kuyatafuta madaraka.
 
Wacha kujidanganya,upinzani kwa Wana CCM wenyewe sahau,hakuna atayekua na ubavu huo.
Aliyewafanya wakawa bungeni ni huyo huyo,wataanzaje kuleta upinzani?kwa hoja gani?

Sent from my Lenovo K10a40 using JamiiForums mobile app
 
Baba wa familia ni rahisi kutatua migogoro ya nje.migogoro ya ndani ni mibaya.hata wanasisiemu wenyewe watapigana ngumi.tusubiri muda uongeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…