econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Udhaifu wa vyama vya upinzani ni kugeukana kwenye critical times baada ya uchaguzi mkuu kupita.
1. Critical time ya kwanza ni 2015 baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar. Baada ya Tume ya uchaguzi Zanzibar kufuta matokeo ya uchaguzi chama Cha CUF kupitia Maalim Seif walipinga na kujitoa kwenye uchaguzi wa marudio.
Cha kushangaza wakati Maalim seif akipambana ili haki ipatikane Zanzibar, akaibuka Prof Lipumba ambaye alikuwa amejiuzulu na kuanza vioja dhidi ya Maalim Seif na kurudi kwa nguvu kwenye uongozi wa chama. Mpaka zikawepo CUF mbili ya Maalim Seif na Lipumba aliyekuwa anasaidiwa na Msajiri wa vyama.
Hivyo, katika critical moment ambayo CUF ilikuwa inapigania haki ya uchaguzi kule Zanzibar, akaibuka mpinzani Prof Lipumba na kuanza kufifisha hizo harakati na hatimaye zikafa. Muda mwingi ukatumika kwenye kesi mahakamani na hoja ya uchaguzi Zanzibar ikafa.
Leo Prof Lipumba anawaomba msamaha wa Zanzibar na kuwaomba warudi CUF na wasahau yaliyopita. Cha kujiuliza kipindi kile aliwageuka wenzake wa Zanzibar kwa sababu gani? Na kwa lengo gani?
2. Critical time ya pili ni mwaka 2020, baada ya madhaifu yalionekana kwenye uchaguzi Mkuu, chama Cha CHADEMA kilipinga matokeo na kudai kutoyatambua. Baadhi ya madhaifu wagombea wengi wa Upinzani kuenguliwa bila sababu za msingi,. Wakurugenzi kuonesha ushabiki wa wazi, Tume kuwafungia kufanya kampeni wagombea wa upinzani, kupatikana kwa kura feki, majimbo karibia yote kupelekwa CCM hata Kama mshindi hakuwa CCM na kuzimwa kwa mitandao ili kupunguza kupashana habari kuhusu kinachoendelea kwenye uchaguzi.
Wakati CHADEMA wakiwa katika Hali ya kuonesha msimamo wa kutokuukubali uchaguzi huo na kuupinga likaibuka kundi la wanawake 19 wa viti maalum CHADEMA ambao wengi wao waligombea majimboni na kwenda kuapishwa bungeni mbele ya spika Ndugai. Hivyo wakaondoa kabisa ile nguvu ya kupinga uchaguzi mkuu, ingawa chama kilikataa kuwatambua na kuwavua uanachama lakini bado wapo bungeni.
Ushauri wangu kwa vyama vya upinzani, tusigeukane kwenye critical time baada ya uchaguzi mkuu , bali tushikamane mpaka kile tunachopigania kipatikane.