Upinzani umekosa hoja na muelekeo, badala kujadili hoja zenye mashiko ili mkubalike mnabaki kujadili takwimu zilizokosewa bahati mbaya


Hao wananchi wa kawaida wao hawawezi kujadili wanasubiri wapinzani tu wawasaidie kujadili ili wawaelewe? Kwahiyo hao wapinzani sio wananchi wa kawaida, ndio maana kuna kikundi cha wananchi wa kawaida, kimelala mahali kinasubiri hao wapinzani wawaeleweshe?
 
Wewe ni zuzu. Ikulu/ofisi ya rais ni taasisi. Inawezekanaje taasisi kubwa namna hiyo kukosea kwa kiwango hicho!??
Wapinzani hao unaotaka waongelee hizo hoja si mlisema mmeshawafuta!!
 

Hao wananchi wao wamelala wanasubiri tu waone wapinzani wanadeal vipi na rais? Kwahiyo hao wananchi wao ni kama ng'ombe hawana wajualo wanasubiri kuongozwa tu?!
 
Wewe ni fanatic unanipotezea muda, usinijibu na kwaheri.
Sasa kama foreign reserve ni usd 6253= Us bil 6.253. Bahati mbaya ikakosewa kutamkwa wewe unaona ishu kubwa ya kujadili utakuwa na akili?
 
Kuweka kumbukumbu sawa tu hapa JF, ni kuwa;

Wapinzani (CHADEMA) kupitia kwa Lissu walitoa hotuba nzito kabla ya hotuba ya mama Samia, na hotuba ya Lissu iligusia mambo muhimu kuhusu Katiba mpya, haki za binadamu, Demokrasia na Uchumi kwa 2021 na katika kuelekea 2022. Ni hotuba yenye majibu ya maswali yote muhimu katika mustakabali wa nchi.

Kuhusu hotuba ya mama Samia, sote tumeisikia, hakuna kipya wala cha ajabu, ni marudio yale yale, yakijaa takwimu za kuokoteza okoteza, nyingine zikiwa ni takwimu zenye kasoro.
 
Umwenyewe mpinzani, ila unavizia vizia, yaani wapinzani ni wengi ukiwafuatilia wanaumbuka vizuri, wenzako ni pole pole, Ngwajiboy, bashiru, yaani wewe tofauti na Nape, Makamba, sabaya, hao ni CCM ila sabaya pia jambazi!
 
Hoja zetu wapinzani zimewasilishwa kwenye hotuba kwa taifa aliyotoa Mh.Tundu Lissu mnamo Tarehe 31.12.2021 hususani kwenye maeneo kadhaa aliyozungumzia kama;
1.Bei ya sukari
2.Bei ya mafuta ya kula
3.Bei ya gas ma nyumbani
4.Bei ya Petrol na Diesel
5.Bei ya mbolea na pembejeo
6.Bei ya nyama
N.k

Hoja zetu wapinzani zimejikita hapo kwenye hiyo hotuba ya Lissu, sasa nyie praise team msijifanye hamjaitazama hiyo hotuba yenye hoja zetu, fanyeni hima kujibu hizo hoja na pia mtoe maelezo ya kutosha kuhusu hizi taarifa za aibu kuhusu akiba ya fedha za kigeni mnazosema mnamiliki 🤣
 
Hao wananchi wao wamelala wanasubiri tu waone wapinzani wanadeal vipi na rais? Kwahiyo hao wananchi wao ni kama ng'ombe hawana wajualo wanasubiri kuongozwa tu?!
Vyama vya siasa vipo kwa niaba ya wananchi hivyo chama kizuri cha siasa lazima kifuate agenda muhimu za wananchi na sio za wafadhili wao.
 
Kwani wenyewe wameshasema walikosea au kiherehere chako tu?
 
Vyama vya siasa vipo kwa niaba ya wananchi hivyo chama kizuri cha siasa lazima kifuate agenda muhimu za wananchi na sio za wafadhili wao.

Hivi unadhani hao wananchi hawaoni ajenda za CDM, au unadhani zile propaganda mfu kuwa CDM wanapewa ajenda na wazungu bado zinawachanganya wananchi? We lazima utakuwa ni mzee ndio maana unadhani zile propaganda mlizofanikiwa kudanganya wananchi zamani, hata kizazi hiki zitawabeba. Hiki sio kile kizazi mliwaonyesha sinema za mauaji ya Rwanda,na visu vya Majita wakajaa.

Kama ni wazungu wamejaa nchi nzima wakiwa na miradi, na kutoa misaada kibao. Sasa sijui hao wapinzani watakutana na wazungu tofauti na hao tunaowaona kwenye hafla za serikali?
 
Wewe kuwa na heshima
Nani alikuambia Rais huwa anakosea?
Rais hakosei
 
Una haki ya kusema hivyo maana upo CCM . Lakini ungepewa wiki moja ya kuwa kiongozi wa upinzani usingeleta hiyo kufuru kwamba Upinzani hauna kitu. Kuna kiongozi yupo jela kwa kesi ya ugaidi na Kuna kiongozi alinusurika kuuawa yupo nje. Wengine walishauawa hata haijulikani walizikwa wapi Kama akina ben sanane, Kuna makomandoo wanateseka jela kisa tu walitaka kuajiriwa na kiongozi wa CHADEMA. halafu wewe unasema upinzani hauna kitu, tujifunze kunyamaza saa zingine.
 
Acha kulisha watu upepo utajuaje upinzani makini wakati sio mpinzani. Wewe Ni CCM lakini unasema hakuna upinzani makini, huo umakini unaupimaje ukiwa CCM?. Wewe Ni daktari halafu unasema wafanyabiashara hawapo making Tena kwa ujumla wake. Acha upotoshaji, wewe Baki na CCM ambayo Ni making kiasi Cha kukopa Deni na kutoza tozo kwa wakati mmoja.
 
Naona unamtumia Dr Slaa kuficha agenda yako. Dr Slaa alipoondoka CHADEMA 2015 ndio upinzani ulipata wabunge wengi, halmashauri nyingi na kura nyingi za urais haijawahi kutokea, mpaka Zanzibar matokeo yakafutwa. Na ili ujue Dr Slaa alikuwa mtu mdogo Sana, hata huko kwao Karatu walimsusia wakaichagua CHADEMA kwenye ubunge mwaka 2015.

Pia naomba nikisahishe kidogo, Dr Slaa hakuwa mtu wa upinzani Bali alikuwa mwana CCM. Alihamia CHADEMA mwaka 1995 baada ya kukatwa kwenye kura za maoni CCM. Hivyo CHADEMA waliposhindwa kumteua kuwa mgombea urais 2015 akahama na kurudi CCM. Hivyo alikuja CHADEMA kimaslahi na Wala hakuwa mpinzani wa kweli. Wapinzani wakweli wanajulikana.

Kuhusu wapinzani kutoadress matatizo yaliyopo nchini naomba utafute hotuba ya Mh Lissu ya Juzi, kaongelea issues nyingi Sana zinazo mgusa mwanachi wa kawaida Kama ajira, mfumuko was Bei na Deni la nje pamoja na miradi mikubwa.
 
Sasa kama foreign reserve ni usd 6253= Us bil 6.253. Bahati mbaya ikakosewa kutamkwa wewe unaona ishu kubwa ya kujadili utakuwa na akili?
Hi ndio shida. Wananchi wanapotoa maoni kuhusu takwimu kukosewa wanatukanwa na kuitwa wapinzani. Yani ikulu ambayo inatakiwa ifanye due diligence inafanya makosa makubwa hivyo, unategemea taasisi za Chini zifanyeje.

Halafu kukosea data sio Jambo dogo Ni Jambo kubwa na lazima lijadiliwe. Unaweza kutoa speech nzuri mbele ya umati wa watu Halafu zipu yako ya suruari ipo wazi. Wewe unazani baada ya speech watu watajadili speech au zip yako kuwa wazi?. Unapotoa speech ya public consumption usilazimishe feedback unayotaka wewe.
 
wanaweza kuachiwa week nzima wanajadili halafu Ijumaa wanapewa press release....J3 next week wanaendelea na Ndugai... baada ya miezi miwili wanaletewa topic nyingine waijadili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…