Upinzani wa Tanzania iko wapi demokrasia ya Kenyatta

Samweli Mathayo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2017
Posts
1,577
Reaction score
1,702
Tanzanian ni nchi inayoongozwa kwa taratibu za kulingana na katiba tuliyonayo,

Kuna watu wanafika hatua wanasema kwamba iko demokrasia ya juu sana nchini Kenya kuliko Tanzania,

1.Kupiga risasi wapinzani na kuwaua ndo demokrasia ya Kenya?

2.Kupiga mtoto wa miaka mitatu risasi kwa masuala ya kisiasa ndo demokrasia?

3. Kuua mwakilishi wa IEBC ndo demokrasia?

4. Kubaguana kikabila ndo demokrasia?

BABA WA DEMOKRASIA AFRIKA NI TANZANIA hakuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania,

Upinzani wa Tanzania una mawenge
 
Sidhani kama watakupa majibu. Wamenywea na kuufyata. Wamejitwika aibu.
 


..hayo mambo yanatokea hata Tz.

..kama utakumbuka wakati wa vurugu za kisiasa Arusha yuko mtoto alipoteza maisha yake.

..pia usisahau Daudi Mwangosi, Aphonce Mawazo, Tundu Lissu, Roma Mkatoliki, ...

..Tumeanza kushuhudia mikutano ya hadhara ikihutubiwa kikabila.

..kwa kweli hatuna cha kuwacheka Wakenya
 
KIONGOZI UTAKOSANA NA WATU MIMI NAONA TANZANIA TUNAITUMIA VIBAYA DEMOKRASIA,DEMOKRASIA YETU INARUDISHA MAENDELEO YA NCHI.
 
Wewe ulisoma hadi darasa la ngapi?, hivi wewe uliyemsifia mtoto wa jirani yako kwamba sio mwizi kama alivyo wako, kesho yake huyo mtoto uliyemsifia amekamatwa akiiba, watu wanakuuliza, imekuaje huyu mtoto mbona ameiba wakati ulisema sio mwizi, jibu unalotoa unasema kwamba "mbona hata mtoto wangu pia ni mwizi", kweli hiyo ni akili au makamasi?

Wewe ndiye uliyesema mwanao ni mwizi, hakuna aliyekupinga, ukamsifia mtoto wa jirani kwamba sio mwizi, sasa watu wanakusuta unakimbilia kurudia kwamba hata mwanao ni mwizi, hakuna aliyekukatalia kwamba mwanao sio mwizi, unachoulizwa ni kikowapi kile ulichokuwa unakisifia, toa maelezo kuhusu mtoto wa jirani yako, sio mtoto wako.
 
Hamna cha demokrasia wala nini, wamevurunda vurunda tu mambo wala hamna anayeweza kusema nii ilikuwa maana ya kufuta uchaguzi na kuitisha uchaguzi mwingine ambao dosari zake ni zaidi ya hata ule uchaguzi uliofutwa??
 


..hoja yangu ni kwamba waTanzania hatuna MORAL AUTHORITY ya kuhoji au kukemea vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya.

..Tusafishe nyumba yetu kwanza kabla ya kuhoji yanayoendelea Kenya.
 
..hoja yangu ni kwamba waTanzania hatuna MORAL AUTHORITY ya kuhoji au kukemea vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya.

..Tusafishe nyumba yetu kwanza kabla ya kuhoji yanayoendelea Kenya.

Ndio kitu nimekisema siku zote humu, kwamba asilimia kubwa ya wanaoponda demokrasia ya Kenya ni makada wa CCM mitandaoni, huwa wanajifanya watetezi wa Wakenya, sasa mimi huwa najiuliza wao wanakandamiza upinzani kwao halafu wakijadili siasa za Kenya wanajiita wanademokrasia wenyewe na wa hali ya juu.

Hebu mtu yeyote anipe uwezekano wa mahakama Tanzania kutengua au kubatili uchaguzi wa urais baada ya rais kutangazwa mshindi na halafu rais aridhie na kukubali kuburuzwa tena kwenye pilikapilka za uchaguzi.
Wengi huwa wanatolea mfano wa kale kakisiwa ka Zanzibar, wanipe uwezekano wa hilo kutendeka Tanzania bara kwa CCM kamili.
 
..hoja yangu ni kwamba waTanzania hatuna MORAL AUTHORITY ya kuhoji au kukemea vurugu za kisiasa zinazoendelea Kenya.

..Tusafishe nyumba yetu kwanza kabla ya kuhoji yanayoendelea Kenya.
JokaKuu Tz tupo mbele sana katika siasa zetu na demokrasia kuzidi Kenya. Ni unafiki tu wa wanasiasa wa upinzani kama kawaida yao ila ukweli Tz tumeendelea sana kwa upande wa siasa za kistaarabu EA.
1) Siasa za hoja, Tz wakati wa uchaguzi wanabishania manifesto, huyu atafanya hichi, yule atafanya kile, yupi muongo. Ukienda Kenya hali ni tofauti kabisa, hadi uchaguzi huu unaishi agenda za kiuchumi hazikuwa mbele, ni mipasho tu na kubishana.

2) Mauaji, Kenya wanasiasa kuuliwa ni kitu cha kawaida kabisa, hakuna anayeona aibu kwa hilo. Mauaji wa kisiasa yaliyofanyika ndani ya hii miezi sita ni ya kutisha. Tunaongelea karibia watu 100 sasa, hadi viongozi wa Dini wakiongea pia wanauliwa. Risasi za moto zimeua hadi watoto, inasikitisha kwa kweli.

3) Uhuru wa mahakama, wakati Tz tuna katiba ya zamani isitoa uhuru mkubwa kwa mahakama, Kenya wana katiba bora zaidi, lakini hali imekuwa tofauti kabisa. Hakuna utayari wa kisiasa Kenya, majaji wanatukanwa na kushambuliwa hadharani, kupigwa risasi kwa gari ya Naibu Jaji Mkuu na kunyimwa ulinzi wa kutosha kwa hawa majaji ujinga huu usingetokea Tz.

4) Ukabila, hii inaeleweka vyema kabisa.

Zaidi ya kuwa na katiba mpya, iliyochochewa kama suluhisho tu la mauaji ya 2007/2008, ambayo wanasiasa hawana utayari. Naiona Tz ipo mbele sana kwa siasa na demokrasia dhidi ya Kenya.
 
Katiba ya Tz kwa sasa hairuhusu matokeo kupingwa mahakamani. Ila bado demokrasia ya Tz ni pana na iiliyo balehe sana kuzidi Kenya. Kenya katiba imeruhusu kupinga matokeo mahakamani, ila mahakama haheshimiwi, Rais anaita majaji wakora, majaji wananyimwa ulinzi wa kutosha na serikali hadi dereva wa Naibu Jaji mkuu anashambuliwa na watu tena wanaodhaniwa ni wa serikali.

Kenya kutandikwa risasi ya moto kwa kosa la kuandamana ni kitu cha kawaida kabisa, mauaji ya ki siasa yamekuwa mengi hadi yamezoeleka kwenu. Angalia Tz Lissu amashambuliwa tu kwa risasi, tukio zima limekemewa na waTz wote, wakati Kenya watu wanadondoshwa kila siku na it's a business as usual.

Kenya kukuta Kenyata anafanya mkutano wa campaign Ikulu si kitu cha kuhoji, tena mbaya zaidi mikutano mingine ni ya kikabila na inaonyeshwa kabisa kwenye Tv bila kificho.Tz kamwe hutoana Magu akiwaita watu wa kabila fulani wafanye mkutano mkubwa tena Ikulu mbele ya Camera akiwaomba kura.

Tz wamestaarabika na wapo mbele sana kwa demokrasia, ni katiba tu ya Kenya ilikuwa inawapa orgasm ila kwa kuwa hakuna utashi na utayari wa kisiasa, hiyo katiba haina maana kwa sasa.
 

..hata Tz kampeni zetu za 2015 zilitawaliwa na mipasho na matusi ya nguoni. tena waliokuwa wanaongoza kwa matusi ni ccm chama kikongwe na chenye hazina ya wasomi wa kila aina.

..mauaji yenye viashiria vya kisiasa yapo Tanzania. kwenye vurugu ya mabomu ktk mkutano wa chadema uliofanyika arusha yuko mtoto mdogo aliuawa kwa risasi. lipo tukio la kuuwawa mwandishi wa habari Daudi Mwangosi aliyelipuliwa kwa bomu mchana kweupe. Shambulizi la Tundu Lissu nalo ni uthibitisho wa siasa za kikatili na kumwaga damu.

..hata mahakama zetu nazo zimeanza kuingiliwa ili kuwakandamiza wapinzani. rejea kesi iliyopelekea kufungwa kwa mbunge wa cdm Peter Lijualikali. Vilevile rejea jinsi Godbless Lema alivyowekwa rumande kwa miezi minne kutokana na michezo michafu iliyokuwa ikifanywa na mawakili wa serekali mahakamani. Mpaka sasa hivi mawakili wale na hakimu aliye-mishandle shauri la Lema bado hawajachukuliwa hatua za kinidhamu.

..Malalamiko kwamba kuna ukabila ktk siasa zetu nayo yameanza kujitokeza.

..Ushauri wangu ni kwamba tusafishe nyumba yetu kabla ya kuanza kuwakoromea majirani na ndugu zetu wa-Kenya.
 
MK254,

..watu wa rika langu tulipokwenda National Service/JKT kuna wimbo tulikuwa tunaimba kuhusu Tom Mboya, Patrice Lumumba, ...

..tulikuwa tunaimba hivyo kwanza kulaani mauaji hayo, lakini pia kujitofautisha siasa za Tanzania na zile za Kenya, Congo, Uganda, etc za miaka hiyo.

..shambulizi la Tundu Lissu kule Dodoma na jinsi alivyoletwa huko Kenya kwa matibabu lilinikumbusha wimbo wa Tom Mboya tuliokuwa tukiimba kwenye makambi ya National Service.

..Nina hakika hata Tundu Lissu naye aliiimba wimbo huo kwasababu na yeye alipita National Service.


Wimbo wenyewe uko hivi:

Kwanza tunawahesabu hao!!

Waliokufa kwa tabu, bila hata ya sababu.

Wengi hawana hesabu waliokufa kwa tabu duniani.


TOM MBOYA wa Kenya huyo!!

Si kiongozi mbaya, kala risasi ya taya.

Maharamia wabaya wala hawaoni haya kumuua.


...

Kwa kweli shambulizi dhidi ya Tundu Lissu lilinirudisha mbali sana mpaka miaka yangu ya JKT na jinsi tulivyolelewa tukijivunia amani yetu wa Tanzania.
 
Hujui unacho ongea au mapenzi yako kwa CDM yamekupofusha ?
Unaongelea mauaji ya Arusha ya 2011 huko, Kenya ukiweka tally ya kuanzia 2010 si utafikisha watu 300 huko. Ndio unataka kulinganisha na Tz kwa namna hiyo, si sahihi kabisa, Kenya wameuana hadi wameshazoea damu sasa, usiweke kundi moja na Tz hawa kwa suala la mauaji, ona hata aibu.

Uhuru wa mahakamani, sielewi kwa nini Lijuakali kushindwa kesi imekuwa mahakama haipo huru, mbona husemi hivyo pindi Lissu anavyoshinda kesi nyingine kila siku, hizi ndimi mbili zinatoka wapi au ni haki tu pale upinzani Tz unashinda kesi na ukishindwa si haki?

Kuhusu kukosa kampeni za hoja hilo lipo wazi, ukimzungumzia Slaa 2010 utasema rushwa, ubadhirifu na katiba mpya, ukimtaja Lowasa 2015 utasema elimu elimu elimu, ukija kwa Magu 2015 utakumbuka elimu bure hadi kidato cha nne, mahakama ya mafisadi, kuondoa usumbufu wa utitiri wa kodi kwa wakulimu nk. Je kwa Kenyatta na Odinga 2017 ni nini unajua, au ni za kutafuta? Kwa yoyote ambaye ameisha hizi nchi mbili tofauti anajua hii tofauti.
 
Unaongelea kushambuliwa kwa Lissu wakati wenzako Kenya wanaua kabisa.
 
Sawa mkuu, lakini angalau Kenya wana Katiba bora kuliko yetu, iweje inyanyase watu wake, iweje iuwe mpaka mtumishi wa tume? Hivi wameonyesha mfano gani kwa nchi yenye katiba bora na ya kusifika? Yaliyotokea Kenya si mambo ya kuungwa mkono
 
Unaongelea kushambuliwa kwa Lissu wakati wenzako Kenya wanaua kabisa.


..risasi 30++ za smg.

..ametolewa risasi 11 mwilini.

..lengo lilikuwa Tundu Lissu afe.

..lakini kama hilo halikusumbui, what about Mwangosi, Alphonce Mawazo, au yule kijana aliyeuwawa morogoro??
 

Hehehe huwa nacheka mnavyo andaa hoja zenu na kujiliwaza, mpo mbali sana kujlinganisha na Kenya.
Bora kwetu maandamano yanaruhusiwa, mara nyingi vurugu huibuka pale waandamanaji wanakiuka taratibu na kuanza kujihusisha na mambo yasioruhusiwa. Kama tukio la juzi pale waandamanaji walithubutu kuvamia kituo cha polisi.
Nyie kwenu maandamano hata ya amani hayaruhusiwi, hata wapinzani kuhutubia wananchi ni hatia, kuhoji takwimu za kiuchumi ni hatia, juzi Zitto Kabwe mumemtia ndani.

Mwengine kahoji mambo ya madini, leo hii tunamuuguza Kenya baada ya kupigwa risasi 38, halafu unanichekesha sana ukisema eti Watanzania walipigia kelele tukio za Lissu kupigwa marisasi. Nyie kituko kweli......

Yaani hata nashindwa nianzie wapi kutaja jinsi mlivyo nyuma, nafikiri kitu ambacho huwa kinawasaidia hamuanikwei ni kwasababu mumejifcha nyuma ya Kiswahili. Huwa kinaficha sana matukio yenu hivyo wadau nje wanasubiri kutafsiriwa taarifa zenu.
 
Sawa mkuu, lakini angalau Kenya wana Katiba bora kuliko yetu, iweje inyanyase watu wake, iweje iuwe mpaka ntumishi wa tume? Hivi wameonyesha mfano gani kwa nchi yenye katiba bora na ya kusifika? Yaliyotokea Kenya si mambo ya kuungwa mkono


..nalaani mauaji yaliyotokea Kenya.

..baada ya hukumu ya supreme court ya Kenya nilitegemea waendesha uchaguzi wa marudio kistaarabu na kwa namna ambayo mataifa mengine yatapenda kuiga.

..Kwa hiyo Kenya wametuangusha Waafrika wengi ambao tulikuwa na matumaini makubwa juu yao.

..lakini pamoja na hayo ningependa kutumia nafasi yangu hapa JF kutahadharisha kuhusu muelekeo na hali ya kisiasa Tanzania.

..Tusipokuwa makini waTanzania tunaweza kuangukia mahali pabaya kuliko ndugu zetu wa Kenya.
 
Hayo maandamano yanayoruhusiwa ndio police wanakuja kutandika risasi za moto, mbaya zaidi hadi Mungiki na wao wanavalishwa jezi za police kwenda kuua Jaluo, nyie ni jamii isiyo na huruma kabisa.

Ndio, Tz mikutano ya kisiasa inayoruhusiwa ni viongozi wa sehemu husika, kama wewe ni Mbunge wa Kajiado, fanya mkutano na wananchi wako wa Kajiado, hakuna haja ya kwenda kufanya uchochezi Nairobi. Huo si utaratibu mbaya na unaleta utulivu wa kisiasa.

Tz kuna sheria ya takwimu, mtu akionekana anafanya maksudi kupotosha takwimu ataenda kujielezea mahakamani, wao ndio watamuhukumu na takwimu zake za kupika. Kuruhusu wanasiasa waropoke uongo wowote kwa jina la uhuru si ushujaa, ni ujinga. Mwanasiasa anageuza takwimu kwa maksudi ili tu atengeneza chuki, hii si uhuru wala demokrasia, acha wakufundishwe adabu mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…