Asante mkuu kwa sifa hii mpya uliyonipaPumbavu kabisa kwa makala ndefu Lakini iliyojaa ujinga tu
upinzani wa Tanzania ni dadiadandia kanyaga twende 🐒
Vyama vya upinzani ni changamoto; wakati mwingine huwa najiuliza kama kweli vinajua vinachokitaka.
Huwa nawaza sana kuhusu yaliyotokea katika kipindi cha Hayati Rais John Pombe Magufuli. Magufuli alipigwa vita sana kisiasa, na karibu kila mradi mkubwa aliouanzisha ulikumbana na upinzani.
Kwanza, suala la kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lilipingwa kwelikweli. Zilitolewa hoja nyingi, mara haikutakiwa kununua ndege kwa fedha taslimu, mara hoja nyingine.
Pili, likaja suala la Bwawa la Julius Nyerere. Magufuli alipigwa vita sana kuhusu mradi huu. Mara hoja ilikuwa anaharibu mazingira, mara hoja nyingine. Kwa kifupi, upinzani dhidi ya mradi ulikuwa mkubwa.
Tatu, ikaja SGR. Hapa pia wananchi walipewa hoja nyingi dhidi ya mradi huo. Wakati mwingine hali ilifika mahali ambapo ilionekana kana kwamba baadhi ya wapinzani walitamani hata serikali ikose mikopo ili mradi ushindwe.
Kwa mtazamo wangu, presha hii ilimfanya Magufuli abadili aina ya siasa ili mambo yaende na kupunguza kile alichokiona kama kelele na vikwazo dhidi ya utekelezaji wa mipango ya serikali yake.
Tarehe 17 Machi 2021 mambo yakabadilika
Baada ya kifo cha Magufuli tarehe 17 Machi 2021, Samia Suluhu Hassan akaingia madarakani.
Tukumbuke kuwa Samia ndiye aliyethubutu kwenda kumwona Tundu Lissu hospitalini Nairobi baada ya Lissu kushambuliwa. Kwangu mimi, kitendo hicho kilionyesha utu, upendo na ukarimu mkubwa.
Samia alipoingia madarakani akaamua kubadilisha hali iliyokuwepo na kuanza kutibu majeraha ya kisiasa.
Katika juhudi hizo, Samia akatafuta namna ya kukutana na Lissu. Nakumbuka katika moja ya mahojiano yake akizungumzia kukutana na Lissu kama kaka na dada.
Kwa mtazamo wangu, Samia alijitahidi kuwa karibu na Lissu na kujenga mazingira ya maridhiano, ingawa nakubali kwamba inawezekana kulikuwa na nguvu nyingine ndani ya mfumo ambazo hazikuwa tayari kwenda naye katika mwelekeo huo.
Mwisho wa siku mazingira ya kisiasa yakabadilika, Lissu akahakikishiwa usalama na yeye pamoja na wengine wakarudi Tanzania.
Nakumbuka pia wakati Samia alipohudhuria shughuli ya wanawake wa BAWACHA. Kipindi hicho nchi ilikuwa na matumaini makubwa sana kuhusu maridhiano ya kisiasa.
Naamini inawezekana hata Samia mwenyewe alikuwa anakutana na upinzani kutoka baadhi ya maeneo ndani ya mfumo. Lakini akaona kwamba kama kweli anataka kubadilisha hali iliyokuwepo, lazima athubutu kufanya maamuzi fulani.
Mabadiliko yaliyofanywa na Samia
Kwanza, Samia aliruhusu tena mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iliyokuwa imezuiliwa.
Pili, kuna baadhi ya maeneo ambayo wakati wa Magufuli yalikuwa yakijiona kama yametengwa, hususan baadhi ya mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania. Samia akaweka msukumo mkubwa katika shughuli za kiuchumi na utalii, na biashara zikaanza kwenda vizuri zaidi.
Tatu, Samia akaruhusu ajira mpya serikalini. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya ofisi za serikali ambazo idadi ya wafanyakazi imeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na hali iliyokuwepo mwishoni mwa kipindi cha Magufuli.
Nne, Samia akaruhusu nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma pamoja na kuendelea kwa upandishwaji wa vyeo, maeneo ambayo yalikuwa yameathirika katika kipindi cha Magufuli.
Samia na miradi aliyoiacha Magufuli
Miradi mingi ambayo Magufuli aliiacha haikuwa imekamilika. Baadhi ilikuwa bado katika hatua za utekelezaji.
Tukumbuke kwamba unaporithi mradi ambao, kwa mfano, umefikia asilimia 30, haimaanishi umeachiwa pia asilimia 70 ya fedha zote zinazohitajika kuukamilisha. Serikali mpya bado inapaswa kutafuta fedha za kumalizia mradi huo.
Samia ameendelea na miradi mingi iliyoanzishwa na Magufuli. Miradi imekamilika na mingine inaendelea. Barabara zinaendelea kujengwa na SGR kuelekea maeneo mbalimbali nchini inaendelea kutekelezwa.
Kwa hiyo, tunapompa Magufuli sifa kwa kuanzisha miradi hii, ni vizuri pia tukatambua nafasi ya Samia katika kuendeleza na kukamilisha miradi hiyo.
Suala la Bandari na TPA
Suala la bandari nalo lilikuwa na upotoshwaji mkubwa katika mijadala ya kisiasa.
Kwa uelewa wangu, kilichofanyika si kuuza bandari kama baadhi ya watu walivyokuwa wakisema. TPA imepunguziwa baadhi ya majukumu ya kiutendaji katika maeneo fulani ili waendeshaji wengine wenye mitaji, teknolojia na vifaa vinavyohitajika washiriki katika shughuli hizo.
Kumbuka, shughuli za kupakia na kupakua mizigo zinahitaji mitambo mikubwa, teknolojia, wataalamu, matengenezo na gharama nyingine nyingi.
Unaweza, kwa mfano, kukusanya Sh bilioni 10 kwa siku lakini ukatumia Sh bilioni 6 kwenye uendeshaji, matengenezo na shughuli nyingine. Mwisho wake unabaki na Sh bilioni 4.
Kwa mfumo wa sasa, Tanzania kupitia TPA inaweza kujikita zaidi katika usimamizi na udhibiti huku shughuli fulani za kiutendaji zikifanywa na waendeshaji wenye uwezo wa kuwekeza kwenye mitambo na teknolojia.
Kwa mtazamo wangu, bandari kwa sasa inafanya vizuri zaidi huku kila upande ukiwa focused kwenye majukumu yake.
Tuje kwa Lissu baada ya kurudi Tanzania
Baada ya Tundu Lissu kurudi Tanzania na kuruhusiwa kuendelea kufanya siasa, mambo yakaanza kubadilika tena.
Kwa mtazamo wangu, upinzani ulidhani kwamba kwa sababu Magufuli ameondoka na Samia anaonekana kuwa mpole zaidi, basi ulikuwa wakati wa kufanya wanavyotaka.
Nadhani wengi mnakumbuka pia yaliyotokea kwa Freeman Mbowe. Mbowe aliingia katika mvutano mkubwa na mamlaka, lakini matukio yaliyofuata yalionyesha kwamba pamoja na kubadilika kwa Rais, nchi bado inaongozwa kupitia sheria, taasisi na mifumo yake.
Lissu naye akaendelea na harakati zake na kutoa hoja nyingi dhidi ya serikali. Kwa maoni yangu, baadhi ya hoja hizo hazikuwa na uthibitisho wa kutosha.
Kuna wakati niliona Lissu akitoa kauli ambazo kwangu zilivuka mipaka ya staha kwa Rais Samia, mtu ambaye hapo awali alikuwa ameonyesha ukarimu kwake.
Nilijiuliza: Je, Lissu alikuwa amesahau yaliyotokea tangu Samia alipokwenda kumwona Nairobi, juhudi za maridhiano zilizofuata, hadi mazingira yaliyomwezesha yeye kurudi Tanzania?
Nakumbuka hata hapa JF kulikuwa na uzi kuhusu baadhi ya kauli za Lissu. Mimi binafsi nilichukizwa na namna alivyoongea kuhusu Samia.
Lissu na Abdul
Pamoja na tofauti hizo, kwa mujibu wa maelezo yaliyowahi kutolewa na Lissu, Abdul, mtoto wa Rais Samia, aliwahi kufanya mawasiliano naye kuhusu namna madai yake yangeweza kushughulikiwa.
Baadaye, Lissu akayazungumzia mawasiliano hayo katika muktadha wa madai ya kutaka kupewa rushwa.
Hapa ndipo nilipoona tatizo kubwa la uaminifu.
Kwa mtazamo wangu, kama mtu amekufuata kwa nia ya kutafuta suluhu ya jambo fulani halafu baadaye mazungumzo hayo yakageuzwa kuwa silaha ya kisiasa dhidi yake na familia yake, inakuwa vigumu kujenga mazingira ya kuaminiana.
Ndiyo maana nikasema: huyu ni mtu ambaye hata ukimbeba mgongoni, anaweza kuchana mbeleko.
Lissu gerezani na siasa za uanaharakati
Yakatokea yaliyotokea na Lissu akaingia gerezani. Chama chake kikaendelea kutumia pia nguvu ya wanaharakati.
Mimi nadhani watu wanaotaka kupewa dhamana ya kuongoza nchi hawawezi kujenga siasa zao katika uanaharakati pekee, matusi ya mitandaoni au kufurahia kila tukio baya linalotokea nchini.
Tukubali au tukatae, chama kilichoshika dola hakiwezi kuwa katika mazingira sawa kabisa na chama kisichoshika dola.
Pamoja na siasa za vyama, mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi ina nafasi ya kuhakikisha Tanzania haiingii mikononi mwa watu wanaoweza kuhatarisha maslahi ya taifa.
Hivyo, vyama vya siasa navyo vina wajibu wa kuonyesha kwamba vina sera, viongozi, uwezo na uzalendo wa kutosha kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Tatizo la kupinga hata maridhiano
Tumeona baadhi ya wanaharakati wakionekana kutopenda dalili za maridhiano.
Pale wanapoona ishara ya mapatano, hata kama ni salamu za pole kutoka kwa Godbless Lema au Tundu Lissu kwenda kwa Rais Samia, baadhi yao wanaanza kulalamika.
Hapo ndipo ninapojiuliza: Tunataka nini?
Kama viongozi wa pande mbili wakitukanana tunalalamika, halafu wakianza kusalimiana na kuonyeshana utu bado tunalalamika, tunataka nchi iende katika mwelekeo gani?
Tanzania inahitaji ushindani wa kisiasa, lakini pia inahitaji amani na uwezo wa viongozi kuzungumza hata kama wanatofautiana.
Suala la Oktoba 29
Nikifikiria yaliyotokea Oktoba 29, huwa napata shida sana kuyaita yote yaliyotokea kuwa maandamano ya amani.
Unaishi bondeni, gari haliwezi kufika nyumbani hivyo unaliacha kwenye kituo cha mafuta, halafu unarudi unakuta kituo kimechomwa moto pamoja na mali zilizokuwepo, kisha unaambiwa hayo ni maandamano ya amani.
Vituo vya mafuta vikachomwa.
Ofisi za serikali zikachomwa.
Vituo vya polisi vikashambuliwa.
Mali zikaporwa.
Halafu mtu anasema hayo yote yalikuwa maandamano ya amani?
Nasikitishwa sana na vifo vilivyotokea. Maisha ya Mtanzania yeyote yanapopotea ni jambo la kusikitisha.
Lakini wakati huohuo najiuliza: Ni njia gani ingeweza kutumika kudhibiti hali ya watu kuchoma na kupora kila kilichokuwa mbele yao?
Nadhani wengi tuliona picha na taarifa za watu wakibeba mali mbalimbali.
Je, hali ile ingeendelea bila kudhibitiwa, nini kingetokea?
Hili ni jambo ambalo tunapaswa kulijadili bila ushabiki. Tukemee matumizi yasiyo ya lazima ya nguvu pale yanapotokea, lakini pia tukemee wazi uchomaji, uporaji na uharibifu wa mali.
Je, Watanzania tunajua tunachokitaka?
Mimi nipo tayari kukosolewa pale ambapo nilichoandika si kweli au hakina ushahidi.
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kila siku:
Hivi sisi Watanzania tunajua tunachokitaka?
Niwaombe vijana wa taifa hili: amkeni.
Msikubali kugombanishwa.
Msikubali kuaminishwa kwamba kila mtu tajiri ameiba na hivyo tunapaswa kumchukia.
Badala yake tujiulize: Amefikaje hapo? Mimi nifanye nini nifike hapo?
Ukweli ni kwamba tunapaswa kutafuta namna ambayo na sisi tunaweza kuingia kwenye mzunguko wa watu wenye mafanikio. Tutafute maarifa, tufanye kazi, tuwekeze na tujifunze mbinu zilizowafikisha wengine walipo.
Mbinu zilezile zinazotumika kuwafundisha vijana kwamba kila tajiri ni mwizi zinaweza pia kutumika kuwafundisha vijana kuichukia CCM bila kwanza kuchambua mambo.
Na hili lisieleweke kwamba CCM haina makosa. CCM inapaswa kukosolewa pale inapokosea, kama ambavyo CHADEMA na vyama vingine vinapaswa kukosolewa pale vinapokosea.
Lakini tusifanye maamuzi kwa sababu tu tumeambiwa mtu huyu au chama hiki ni kibaya.
Ewe kijana, soma. Chunguza. Pambanua. Tafakari. Kisha fanya uamuzi wako mwenyewe.
Mzee Jakaya Kikwete ana kauli yake maarufu:
“Ya kuambiwa changanya na ya kwako.”
Asanteni.
Hatutaki mauaji na utekaji kila siku. Tunataka ulinzi wa kila mwananchi ili tufurahie kuwa huru